Na Stella Kalinga
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Zanzibar,Mhe Amina Salum Ali ametoa
wito kwa Serikali kuwekeza katika historia ya nchi na kurahisisha utaratibu wa
kutembelea makumbusho ili wananchi wapate taarifa za kina na kujua historia ya
nchi.
Mhe.Waziri ameyasema hayo leo walayani Butiama alipotembelea makazi
ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere na kuona kaburi lake
katika eneo la Mwitongo wilayani humo.
Mhe.Waziri amesema ipo haja kwa Watanzania kufahamu historia ya nchi ili
wailinde na kuienzi.
Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwa
kudumisha Armani,umoja na mshikamano ikiwa ni njia ya kuendeleza muungano
aliouasisi kwa ushirikiano na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Sheikh
Abeid Aman Karume.
Mhe.Balozi Amina Salum Ali amepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na nyumba alizoishi Hayati Mwl.Nyerere kabla na baada ya kuwa
madarakani,makumbusho ya Mwl.Nyerere,makaburi ya wazazi wa Mwl.Nyerere, msitu
wa Mwl.Nyerere,nyumba ya chifu wa Wazanaki,vihenge vya kuhifadhia mazao na
maeneo mengine ambapo alipewa taarifa juu ya maeneo hayo
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe Anthony Mtaka ametoa rai kwa viongozi hapa
nchini kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba Taifa,Mwl.Nyerere kwa kuendeleza mema
aliyoyaanzisha kwa maslahi ya wananchi naTaifa kwa ujumla.
"Viongozi na hasa sisi vijana tunao wajibu wa kutekeleza kwa vitendo
siyo Maneno mambo mema ya Mwl.Nyerere, mwalimu alikuwa mzalendo, hakupenda
rushwa na ufisadi, alipenda haki, na sisi tunapaswa kumuenzi Mwl.Nyerere"
amesema Mtaka.
Mhe.Waziri Balozi Amina Salum Ali amefanya ziara kwenye makazi ya
Mwl.Nyerere wilayani Butiama akitokea mkoani Simiyu ambako alikuwa na ziara ya
siku tatu yenye lengo la kutembelea na kuona maeneo mbalimbali yanayohusu sekta
ya viwanda na biashara.
Akiwa Mkoani Simiyu Mhe Waziri ametembelea viwanda vidogo na vya kati
vikiwemo kiwanda cha chaki (Maswa) na cha kusindika Maziwa(Meatu) pamoja na
maeneo ya wawekezaji katika mazao ya biashara(Pamba)na chakula(mchele).
Mhe.Waziri amehitimisha ziara yake mkoani Simiyu kwa kuihakikishia Serikali
ya Mkoa huo kuwa Zanzibar iko tayari kufanya biashara na mkoa huo hususani
katika mazao ambayo yanaweza kutumika kama malighafi ya viwanda vya Zanzibar na
mazao ya chakula kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla;jambo lililoungwa
mkono na viongozi wa mkoa huyo.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (kulia), Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (kushoto)
wakiwa katika eneo alizaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere wakati alipotembea
makazi ya Mw.Nyerere Mwitongo Wilayani Butiama.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akiwasha mshumaa katika kaburi la Hayati
Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere wakati alipotembelea makazi ya Mw.Nyerere
Mwitogo Wilayani Butiama.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini, Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe.
Balozi Amina Salum Ali , wataalam wa wizara hiyo na Wataalam wa Mkoa wa Simiyuwakienda kuona moja ya nyumba
ya Mwalimu Nyerere.
Waziri
wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali , wataalam
wa wizara hiyo, Viongozi na Watalaam wa Mkoa wa Simiyu wakipewa maelezo juu ya
zana za asili mara baada ya kutembelea Makumbusho ya Hayati Baba wa
Taifa,Mwl.Nyerere.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali na baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakipewa maelezo kuhusu moja ya nyumba za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Nyerere
na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Mwl.Nyerere iliyopo Mwitongo wilayani Butiama.
Waziri
wa Biashara,Viwanda na Masoko wa
Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (kushoto), akiwa
nafimbo aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (kulia) kama zawadi walipotembea makazi ya Mwl.Nyerere
eneo la Mwitongo Wilayani Butiama.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwa na viongozi na wataalam wa Mkoa wa
Simiyu wakiwa katika moja ya nyumba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere.
Sehemu ya moja ya
nyumba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere aliyoishi baada ya kuondoka
madarakani.
Baadhi ya vihenge
vilivyotumika na Hayati Mwl.Julius Nyerere kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya
nafaka.
Nyumba
lilimo kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwl.J.K. Nyerere.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari ya Mkoa huo, Ndg.Frank Kasamwa zawadi ya fimbo aliyonunua Katika Makumbusho
ya Mwl.J.K Nyerere.
Baadhi ya vitu
vilivyopo katika Makumbusho ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere Mwitongo Butiama.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali, viongozi na wataalam wa
Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Makumbusho la Mwl.Julius
Kambarage Nyerere.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (mwenye suti nyeusi), viongozi
na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika moja ya miradi ya ufugaji wa samaki
wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega,Mhe.Tano Mwera akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Biashara,Viwanda
na Masoko wa Serikali za mapinduzi ya
Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (mwenye suti nyeusi) wilayani humo.
Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali
za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (wa nne kushoto),, viongozi
na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
Waziri huyo kuhitimisha ziara ya siku tatu mkoani Humo.
Waziri
wa Biashara,Viwanda na Masoko wa
Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali akizungumza na
viongozi na wataalamu wa mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kuhitimisha
ziara yake ya siku tatu Mkoani humo..