Tuesday, January 31, 2017

WAZIRI WA BIASHARA ATOA WITO KWA SERIKALI KUWEKEZA KATIKA HISTORIA YA NCHI

Na Stella Kalinga
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Zanzibar,Mhe Amina Salum Ali ametoa wito kwa Serikali kuwekeza katika historia ya nchi na kurahisisha utaratibu wa kutembelea makumbusho ili wananchi wapate taarifa za kina na kujua historia ya nchi.

 Mhe.Waziri ameyasema hayo leo walayani Butiama alipotembelea makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere na kuona kaburi lake katika eneo la Mwitongo wilayani humo.

Mhe.Waziri amesema ipo haja kwa Watanzania kufahamu historia ya nchi ili wailinde na kuienzi.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwa kudumisha Armani,umoja na mshikamano ikiwa ni njia ya kuendeleza muungano aliouasisi kwa ushirikiano na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Sheikh  Abeid Aman Karume.

Mhe.Balozi Amina Salum Ali amepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyumba alizoishi Hayati Mwl.Nyerere kabla na baada ya kuwa madarakani,makumbusho ya Mwl.Nyerere,makaburi ya wazazi wa Mwl.Nyerere, msitu wa Mwl.Nyerere,nyumba ya chifu wa Wazanaki,vihenge vya kuhifadhia mazao na maeneo mengine ambapo alipewa taarifa juu ya maeneo hayo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe Anthony Mtaka ametoa rai kwa viongozi hapa nchini kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba Taifa,Mwl.Nyerere kwa kuendeleza mema aliyoyaanzisha kwa maslahi ya wananchi naTaifa kwa ujumla.

"Viongozi na hasa sisi vijana tunao wajibu wa kutekeleza kwa vitendo siyo Maneno mambo mema ya Mwl.Nyerere, mwalimu alikuwa mzalendo, hakupenda rushwa na ufisadi, alipenda haki, na sisi tunapaswa kumuenzi Mwl.Nyerere" amesema Mtaka.

Mhe.Waziri Balozi Amina Salum Ali amefanya ziara kwenye makazi ya Mwl.Nyerere wilayani Butiama akitokea mkoani Simiyu ambako alikuwa na ziara ya siku tatu yenye lengo la kutembelea na kuona maeneo mbalimbali yanayohusu sekta ya viwanda na biashara.

Akiwa Mkoani Simiyu Mhe Waziri ametembelea viwanda vidogo na vya kati vikiwemo kiwanda cha chaki (Maswa) na cha kusindika Maziwa(Meatu) pamoja na maeneo ya wawekezaji katika mazao ya biashara(Pamba)na chakula(mchele).

Mhe.Waziri amehitimisha ziara yake mkoani Simiyu kwa kuihakikishia Serikali ya Mkoa huo kuwa Zanzibar iko tayari kufanya biashara na mkoa huo hususani katika mazao ambayo yanaweza kutumika kama malighafi ya viwanda vya Zanzibar na mazao ya chakula kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla;jambo lililoungwa mkono na viongozi wa mkoa huyo.

 
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka  (kushoto) wakiwa katika eneo alizaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere wakati alipotembea makazi ya Mw.Nyerere Mwitongo Wilayani Butiama.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (wa pili kushoto)  akiwasha mshumaa katika kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere wakati alipotembelea makazi ya Mw.Nyerere Mwitogo Wilayani Butiama
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakipewa maelezo kuhusu kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl.Nyerere na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Mwl.Nyerere lililopo Mwitongo wilayani Butiama.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini  akiwa na baadhi ya wataalam wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar wakiwa katika moja ya maeneo ya kumbukumbu yaliyotembelewa na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali alipotembelea makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Nyerere
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (mwenye suti nyeusi), viongozi na baadhi ya Wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiingia katika eneo la Makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere Mwitongo Wilayani Butiama

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akiwasha mshumaa katika kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere wakati alipotembelea makazi ya Mw.Nyerere Mwitogo Wilayani Butiama.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini, Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali , wataalam wa wizara hiyo na Wataalam  wa Mkoa wa Simiyuwakienda kuona moja ya nyumba ya Mwalimu Nyerere.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali , wataalam wa wizara hiyo, Viongozi na Watalaam wa Mkoa wa Simiyu wakipewa maelezo juu ya zana za asili mara baada ya kutembelea Makumbusho ya Hayati Baba wa Taifa,Mwl.Nyerere.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakipewa maelezo kuhusu moja ya nyumba za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Nyerere na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Mwl.Nyerere iliyopo Mwitongo wilayani Butiama.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (kushoto), akiwa nafimbo aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka  (kulia) kama zawadi walipotembea makazi ya Mwl.Nyerere eneo la Mwitongo Wilayani Butiama.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali  akiwa na viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika moja ya nyumba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere.
Sehemu ya moja ya nyumba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere aliyoishi baada ya kuondoka madarakani.
Baadhi ya vihenge vilivyotumika na Hayati Mwl.Julius Nyerere kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya nafaka.
Nyumba lilimo kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwl.J.K. Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa huo, Ndg.Frank Kasamwa  zawadi ya fimbo aliyonunua Katika Makumbusho ya Mwl.J.K Nyerere.
Baadhi ya vitu vilivyopo katika Makumbusho ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere Mwitongo Butiama.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali, viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Makumbusho la Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (mwenye suti nyeusi), viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika moja ya miradi ya ufugaji wa samaki wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe.Tano Mwera akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (mwenye suti nyeusi) wilayani humo.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali (wa nne kushoto),, viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri huyo kuhitimisha ziara ya siku tatu mkoani Humo.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  wa Serikali za mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Balozi Amina Salum Ali akizungumza na viongozi na wataalamu wa mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu Mkoani humo..

1 comment:


  1. Hello.
    Mimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.

    ReplyDelete

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!