Wednesday, January 11, 2017

RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI HAITATOA CHAKULA CHA MSAADA

Na Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa Serikali yake ya awamu ya tano haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na wananchi wa Nyashimo, Masanzakona, Lamadi, pamoja na Nyamikoma wilayani Busega na Somanda Bariadi Mjini Mkoani Simiyu kwa nyakati tofauti, wakati wa  ziara yake ya siku mbili Mkoani humo.

Aidha, Rais Magufuli amesema kutokana na maeneo mengi nchini kutopata mvua za kutosha, wananchi walime mazao yanayostahimili ukame na yale yanayokomaa ndani ya muda mfupi kama vile  mtama,uwele,ulezi na viazi.

Ameongeza  kuwa serikali haiwezi kutoa chakula cha msaada kwa watanzania zaidi ya Milioni 50 nchi nzima, badala yake itaboresha miundombinu ikiwemo barabara pamoja na huduma za jamii  kama vile elimu, afya,maji na umeme.

“Nasema sitaleta chakula, nataka Watanzania wafanye kazi, nimeona niwaeleze ukweli ili mnielewe, maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu, najua wapo wanasiasa watawaambia kuwa watawaletea chakula, hakuna chakula fanyeni kazi” amesema Rais Magufuli.

Aidha,Mhe.Rais amewataka wakazi wa wilaya ya Busega hususani wale walio pembezoni mwa Ziwa Victoria kujipanga kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiliaji ambao umeanzishwa na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Busega,  wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka na akaahidi kuwa Serikali itawasaidia katika miundombinu ya umwagiliaji.

Akizungumzia gharama za ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo, Rais Magufuli ameugiza uongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Wakala wa Majengo (TBA) kukaa na kurejea upya gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo ya shilingi bilioni 46 kwa kuwa haiendani na hali halisi ya jengo litakalojengwa.
  
“Haiwezekani majengo ishirini yenye ghorofa nne kila moja ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujengwa kwa shilingi bilioni 10 na jengo hili moja la ghorofa moja kujengwa kwa shilingi bilioni 46” amesema Mhe.Dkt. Magufuli.

Pia Mhe.Rais ameahidi kutoa jumla ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo ameelekeza kuwa ikamilike kabla ya kumalizika kwa kipindi chake cha uongozi ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu wapate huduma za afya zinazohitajika.

Wakati huo huo Rais Magufuli ameutaka uongozi wa Mkoa wa Simiyu kusimamia na kuhakikisha ujenzi wa tenki la maji ya Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria(Katika Mlima Ngasamo) ambao utatekelezwa na Serikali yake unaendelea ili wananchi wa Mkoa huo kupata maji badala ya kukwama kutokana na Mwekezaji kutaka kuchimba madini ya Nikeli katika mlima huo

Rais Magufuli amesema  hayuko tayari kuona wananchi zaidi ya milioni moja  na laki tano wa mkoa wa Simiyu wanakosa huduma muhimu ya maji  kutokana na mwekezaji huyo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini hivyo amemtaka Waziri wa Nishati na madini kumfutia leseni mwekezaji huyo.

Rais Magufuli yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo leo amepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Busega na Bariadi pamoja na kuweka Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa Kilomita 71.8.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkta John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ambaye yuko mkoani humo kwa ziara ya siku mbili.
Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe.Prof.Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kuzungumza na wananchi hao wakati wa ziaa yake mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Masanzakona (hawapo pichani) Wilayani Busega mara baada ya kupokelewa na Viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu akikagua jengo la Hospitali ya Mkoa huo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo  wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda,kabla ya kuwahutubia wananchi na kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi mjini wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.

Wanafunzi kutoka katika baadhi ya shule za Msingi na Sekondari za Mjini Briadi wakiimba wimbo maalum wa Mkoa wa Simiyu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu akikagua jengo la Hospitali ya Mkoa huo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo  wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo, (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo ,Mhe.Anthony Mtaka.
Baadhi ya wananchi wa Bariadi wakimsilikilizaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alipowahutubia wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kata ya Nyashimo (hawapo pichani) Wilayani Busega mara baada ya kupokelewa na Viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.
: Baadhi ya wananchi wa kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsilikilizaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe.Andrew Chenge mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu wakati waziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu na Wakala wa Barabara wakimsilikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alipowahutubia wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  wakiwa katika jukwaa kuu kabla ya kuwahutubia wananchi wa Bariadi wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani Simiyu katika eneo la Masanzakona wilayani Busega wakati wa ziara yake Mkoani humo.
Waimbaji wa kwaya ya Walimu Bariadi mjini wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi,Mhe.Andrew Chenge (kushoto) akiwasilisha matatizo na changamoto za wananchi wa jimbo lake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, (kulia) Mkuu wa mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Bariadi mara baada ya kuwahutubia  katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!