Thursday, January 12, 2017

RAIS MAGUFULI AMEAGIZA KIWANDA CHA CHAKI MASWA KUONGEZA UZALISHAJI

Na Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ameagiza  kiwanda cha kutengeneza Chaki kilichopo wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu kuongeza  uzalishaji  ili kiweze kukidhi mahitaji ya chaki ya nchi nzima.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa mara baada ya kutembelea kiwanda hicho siku ya pili ya Ziara yake Mkoani Simiyu ambapo  baadaye ameweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.

Rais Magufuli amewapongeza Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Maswa kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya Tanzania ya Viwanda na jitihada walizozifanya katika kuanzisha kiwanda hicho kwa kuwa kimekuwa msaada hasa katika kuwapatia ajira vijana.

“Kuanzisha kiwanda hiki mmetengeza ajira na chaki nimezijaribu mimi mwenyewe kuandikia nimeona ni nzuri kwa sababu hata mimi nilikuwa mwalimu, hongereni sana Maswa kwa kuwa na kiwanda hiki, hii ndiyo dhamira yetu ya kuwa na viwanda, kiwanda siyo lazima kiwe na ghorofa ishirini, hata ukiwa na chumba kimoja kinaweza kuwa kiwanda” alisema Magufuli.

Rais Magufuli amesema kikijengwa kiwanda kikubwa na  kikaongeza uwezo wa kuzalisha chaki za kutosheleza mahitaji ya nchi nzima, chaki hizo zitanunuliwa na kutumika nchi nzima kwa kuwa kwa sasa kinaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa 10.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema uwepo wa kiwanda cha chaki Maswa uwe ni kichocheo cha vijana na wanawake wa wilaya na mkoa wake kwa ujumla,  kujiunga katika vikundi kubuni miradi ya maendeleo, ili Serikali iwawezeshe kupata mikopo kwa ajili ya mitaji kwa kuwa hata kiwanda hicho kilianzishwa na kikundi cha vijana ambao wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya kwa sasa.

Wakati huo huo Rais Magufuli amewataka wananchi wa Wilaya ya Maswa na mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuitimia vizuri barabara ya Maswa-Mwigumbi ambayo ameiwekea jiwe la msingi leo pindi  itakapokamilika,  kwa lengo la kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kufanya biashara mbalimbali, kwa kuwa itarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pia.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof.Makame Mbarawa  amewataka wakandarasi na wahandisi washauri wanaojenga barabara hiyo kuhakikisha wanaijenga kwa viwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na kuimaliza kwa muda uliopangwa.
Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wasimamizi wa barabara hiyo kwa viwango  vilivyopo katika mkataba vinginevyo hawatapewa kazi tena hapa nchini.

Sambamba na hilo Mhe.Rais aliahidi kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Maswa zilizowasilishwa na Wabunge wote (Maswa Mashariki na Maswa Magharibi) moja baada ya nyingine kulingana hali itakavyoruhusu ikiwepo tatizo la maji,  ambapo aliwahaakikishia kuwa mwaka fedha zimetengwa jumla ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa chujio la maji katika Bwawa la Sola(Zanzui)

Vile vile Mhe.Rais amewataka viongozi wa serikali kutowapangia bei ya mazao wakulima na badala yake wawaache wajipangie wenyewe, ambapo amewataka kuuza mazao yao katika bei itakayowanufaisha huku wakitunza akiba wa ajili chakula chao.

Mhe.Rais Magufuli amekamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo ameweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa kilomita 50.3.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi wilayani Maswa, yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi wilayani Maswa, yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia mamia ya wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi barabara ya Maswa-Mwigumbi  yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu,( kulia)Mkuu wa wilaya hiyo,Mhe.Dkt.Seif Shekalghe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akwahutubia mamia ya wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wilayani Maswa mara baada ya kutembelea kiwanda cha chaki na duka la maziwa ya Meatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akionesha maziwa ya Meatu kwa  mamia ya wananchi wa Maswa mara baada ya kutembelea kiwanda cha chaki na duka la maziwa ya Meatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu akitoa Salamu za Mkoa huo na kutambulisha wageni ngazi ya Kimkoa na Kitaifa wakati wa ziara ya Mhe.Rais wilayani Maswa , ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt.Seif Shekalaghe  akitambulisha  wageni ngazi ya wilaya wakati wa ziara ya Mhe.Rais wilayani humo , ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof.Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Maswa katika uwanja wa Benki ya CRDB kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
:Mbunge wa Maswa Mashariki,Mhe.Stanslaus Nyongo akiwasilisha kro na matataizo ya Wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Waziri wa TAMISEMI wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Omary Haji  akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa wakati wa ziara ya kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli mkoani Simiyu ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Waimbaji wa Kwaya ya Walimu wilaya ya Maswa wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, ambaye aliweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe.Zainab Taleck akipanda mtipamoja na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu kama ishara ya ujirani mwema  mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, kuweka  jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na baadhi ya wabunge wa mkoa huo wakipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo la jiwe la ufunguzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kuweka  jiwe la msingi la barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na baadhi ya wabunge wa mkoa huo wakimwagilia Mti wa kumbukumbu walioupanda katika eneo la jiwe la ufunguzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi,  mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, kuweka  jiwe la msingi la barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia mamia ya wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa,  kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa barabara (TANROADS) Simiyu, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa barabara (TANROADS) wa Simiyu na mikoa jirani, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi,  baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wakandarasi wanaojenga barabra ya Maswa-Mwigumbi baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo, yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami , wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Baadhi ya Watumishi wa Wilaya ya Maswa na Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakimsilkiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Kikundi cha Ngoma cha Simba Mchawi cha Wilayani Maswa wakitoa burudani kwa wananchi wa wilaya hiyo kabla Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Maswa wakimsilkiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!