Thursday, January 27, 2022
Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
“Eleweni Changamoto za Wananchi katika Maeneo yenu, na Muwe Watatuzi”- RC KAFULILA
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa wa Halmashauri ya Bariadi Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kilichofanyika hivi karibuni.
Mhe.Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kikao kazi hicho alisisitiza umuhimu wa Watendaji kupewa mafunzo ya mara kwa mara nje ya eneo la kazi pamoja na mafunzo kazini.
“Kila Mtendaji kata,kijiji na mtaa lazima ajue Sheria ambayo imemfanya awepo kazini. Unapaswa kujua 'ABC' za uendeshaji ofisi. Lazima vikao vyote vya kisheria vifanyike, kuwe na ajenda za vikao na kumbukumbu za vikao hivyo.Lazima muwe na mpango kazi,hizo ndio zana za kazi.Lazima upange kazi zako na uje wiki ijayo utashughulikia nini? Mkiwa viongozi mnapaswa kuelewa changamoto zinazowakabili wananchi wa kwenye maeneo yenu,na kuwa watatuzi wa changamoto hizo.".Ameeleza Kafulila.
Akielezea agenda nne za Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake.Mhe. Kafulila amezitaja ajenda hizo kuwa ni makusanyo, kilimo, ukame/chakula na upandaji miti.
Akizungumzia agenda namba moja ambayo ni Makusanyo, Mhe. Kafulila amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kushindanisha Vijiji kwa asilimia za makusanyo na mashindano hayo yafanyike kila robo mwaka na hatimae kuzitambua halmashauri zilizofanya vizuri aidha kwa kuwapa vyeti au barua ya Pongezi. Hili lifanyike katika Halmashauri zote. Kila Halmashauri iwe na lengo la makusanyo.
Kuhusu kilimo,Mhe. Kafulila amewataka wakuu hao kujipanga na killimo cha alizeti. "Matumaini yetu ni kuzalisha alizeti tani 200,000-250,000 ikilinganishwa na tani 81,000 ambazo zilizalishwa Mwaka Jana. Suala la kilimo cha Pamba na Alizeti linatakiwa kuwa agenda ya eneo lako.Kila kitongoji ni vyema kuwa na majina ya wakulima na kujua wamelima nini kama ni alizeti au pamba".Amesisitiza Kafulila.
Aidha ili kukabiliana na changamoto ya chakula kutokana na ukame ambao umesababisha bei za chakula kuwa juu,Mhe. Kafulila amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa kilimo cha mazao ya chakula ambayo hayahitaji mvua nyingi. "Nimeshaongea Mamlaka ya kilimo Morogoro, baaada ya kutoa Pamba shambani itabiidi wakulima walime dengu.Mamlaka ya kilimo itatoa mbegu, zana na pembejeo za kuwawezesha ili waweze kishiriki kilimo bora.
Akizungumzia ajenda ya tatu, Mhe.Kafulila ameitaja ajenda hiyo kuwa upandaji wa miti. Simiyu ni miongoni mwa mikoa 5 Tanzania Bara inayoongoza kwa ukataji wa miti, hivyo ili kuepukana na janga la jangwa ni vyema kila kijiji kiwe na agenda ya upandaji wa miti. Akitaja ajenda namba nne, Mhe.Kafulila ameitaja ajenda hiyo kuwa ni Elimu," fuatilieni na kusimamia kikamilifu agenda ya Elimu. Wiki ijayo tutakutana kuzungumzia kwa kina kuhusu matokeo.Watendaji wa kata na vijijini wekeni macho yenu kwenye suala la Elimu."Amesisitiza Kafulila.
Mhe. Kafulila amewapongeza watendaji wa kata, vijiji, mitaa, mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri hizo mbili kwa uchapakazi. Aidha amewahakikishia wakuu hao imani kubwa aliyonayo kwao ya kwamba wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi makubwa zaidi wakiamua."Mnachohitaji ni kuwatambua watu wa chini kwa kazi nzuri wanazofanya.Wapeni hata barua au cheti cha kuwapongeza. Maeneo yote wanayofanikiwa wapeni moyo na wanapokosea wachukulieni hatua kali.Wanaofanya vizuri wapeni hamasa kubwa.Uwezo wa kubadilisha vijiji, Wilaya, upo mkononi mwetu.”
Akizungumzia kusudi la kikao kazi hicho, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange ameeleza nia ya kikao kazi hicho ni kujengeana uwezo na kuzindua kauli mbiu ya Halmshauri ya Bariadi Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi isemayo: "Serikali mlangoni Mwako". Mwisho.
Tuesday, January 25, 2022
WAKURUGENZI, WAKUU WA WILAYA ELIMISHENI WANANCHI KUHUSU FURSA MBALIMBALI ZA MIKOPO - RC KAFULILA.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila (kulia) akikabiidhi hundi ya Mfano kwa wawakilishi wa makundi ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu. |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila (Kulia) akiteta jambo pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange wakati wa tafrija hiyo. |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na washiriki wa tafrija hiyo leo katika ukumbi wa Bariadi Conference -Bariadi Simiyu |
Makundi mbalimbali ya washiriki kwenye hafla hiyo. |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila,ameyasema hayo leo, wakati wa hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi. Akizungumza, Mhe.Kafulila ameeleza lengo la Serikali katika utoaji wa mikopo ya aina hiyo ni kuwawezesha wananchi wasiokidhi vigezo vya kukopeshwa na benki, kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa fursa mbalimbali yakiwemo makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwa kuwapatia mikopo ya fedha za asilimia 10 ya mapato ya ndani yaliyokusanywa na halmashauri za miji.
Friday, January 14, 2022
RC- Kafulila Atembelea na Kutoa pole Kwa Familia za Wafiwa Wilayani Busega
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Gabriel Zakaria,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Bracius Chatanda na OCD wa Busega,leo wamewatembelea na kuwapa pole familia ambazo zilipoteza ndugu zao,kwenye ajali iliyotokea 11/1/2022 katika Kijiji cha Kalemela, Wilayani Busega na kusababisha vifo vya watu 15 kufikia leo.
Wakazi wa kijiji cha Kalemela pamoja na maeneo ya jirani wamepoteza watu 9 na kufanya Mkoa wa Simiyu kupoteza watu 9 kupitia ajali hiyo.
Aidha Mhe.Kafulila ametumia fursa hiyo kuwapatia wakazi hao Salaam za pole toka kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na pamoja na ubani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mwisho.
Mhe. Kafulila akitoa neno la faraja kwa Wafiwa
Ndugu,jamaa na marafiki wa wafiwa |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyi ACP. Bracius Chatanda pamoja na OCD Busega wakiwafariji ndu za marehemu |
Ndugu, jamaa, marafiki na majirani wa Wafiwa |
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria akizungumza na kutoa pole kabla ya kumkaribisha mkuu wa Mkoa wa Simiyu |
Mhe. Kafulila akitoa mkono wa pole kwa Wafiwa |
Mhe Kafulila akitoa neno la faraja kwa wafiwa |
Mhe. Kafulila akitoa mkono wa pole kwa Wafiwa |
Mhe.Kafulila akiagana na wafiwa |
Mkoa wa Simiyu Wafanya Kongamano la Maombi, Kuuombea Mkoa!
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akitoa neno la shukrani kwa Viongozi wa dini zote Mkoani Simiyu mara baada ya kongamano la kuuombe Mkoa wa Simiyu. |