Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Gabriel Zakaria,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Bracius Chatanda na OCD wa Busega,leo wamewatembelea na kuwapa pole familia ambazo zilipoteza ndugu zao,kwenye ajali iliyotokea 11/1/2022 katika Kijiji cha Kalemela, Wilayani Busega na kusababisha vifo vya watu 15 kufikia leo.
Wakazi wa kijiji cha Kalemela pamoja na maeneo ya jirani wamepoteza watu 9 na kufanya Mkoa wa Simiyu kupoteza watu 9 kupitia ajali hiyo.
Aidha Mhe.Kafulila ametumia fursa hiyo kuwapatia wakazi hao Salaam za pole toka kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na pamoja na ubani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mwisho.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Daavid Kafulila akiwa ameambatana ma Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria wakitembelea na kutoa pole kwa familia ambazo zimepoteza ndugu zaokutoka na aksidenti iliyotokea 11/1/2022 Wilayani Busega na kusababisha vifo vya watu 15 kufikia 13/1/2022/ |
|
Mhe. Kafulila akitoa neno la faraja kwa Wafiwa |
|
Ndugu,jamaa na marafiki wa wafiwa |
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyi ACP. Bracius Chatanda pamoja na OCD Busega wakiwafariji ndu za marehemu |
|
Ndugu, jamaa, marafiki na majirani wa Wafiwa |
|
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria akizungumza na kutoa pole kabla ya kumkaribisha mkuu wa Mkoa wa Simiyu |
|
Mhe. Kafulila akitoa mkono wa pole kwa Wafiwa |
|
Mhe Kafulila akitoa neno la faraja kwa wafiwa |
|
Mhe. Kafulila akitoa mkono wa pole kwa Wafiwa |
|
Mhe.Kafulila akiagana na wafiwa |
0 comments:
Post a Comment