Wednesday, January 23, 2019

Waziri wa Afya Aitaka TBA Kurejesha Fedha za Ujenzi wa Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Wakala wa Majengo nchini TBA kurejesha fedha ilizokabidhiwa na wizara yake kwenye ofisi za TBA mjini Bariadi ili zitumike kukamilisha mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambao kasi ya ujenzi wake kwa sasa hairidhishi.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya siku moja mjini Bariadi, mkoani Simiyu kukagua ujenzi wa jengo litakalotumika kutoa huduma za maabara, upasuaji na mionzi na kusema kuwa serikali imejiwekea malengo ifikapo Julai  Mosi wananchi waanze kupata huduma kwani tayari fedha zote za mradi huo zimekwishalipwa.

 “Wizara tayari imeshalipa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa TBA lakini cha ajabu wao wameleta shilingi milioni 430 tu, na matokeo yake ndio haya, ukiangalia muda tuliopewa kukamilisha kazi hii si rafiki, sasa ninawaagiza TBA walete hiyo pesa site ili kazi iendelee”.

“ Hivi jamani kwa kasi hii kweli tunaweza kuendelea kuweka matumaini kwa hawa ndugu zetu, ukiangalia mheshimiwa Rais ametupatia shilingi bilioni 2.5 tujenge jengo la mama na mtoto sasa kwa utaratibu huu wa kusuasua mnadhani tutafika kweli, mimi nadhani umefika wakati tutumie force account kwenye mradi huu, Bariadi kuna mafundi wengi wazawa wenye uwezo mkubwa wa kutufanyia kazi hii”, alisisitiza Waziri Ummy.

Kuhusu mpango wa serikali wa kuboresha huduma za rufaa katika hospitali zote za mkoa nchini, Waziri Ummy amesema wizara imedaa utaratibu ambapo kila hospitali itapata madaktari bingwa 16 katika fani 8 yaani madaktari 2 kila fani wakiwemo madaktari bingwa wa akina mama, watoto, Mishipa ya fahamu, mifupa, njia ya mkojo, dawa za usingizi na mionzi.

“ Tunataka tuwe na maabara kubwa za kisasa pamoja na jengo la mionzi kama tunalojenga hapa Simiyu katika kila hospitali ya rufaa ya mkoa, tunamshukuru sana mheshimiwa rais kwa kutupatia shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo uchunguzi, ninaomba kila mmoja wenu kwa nafasi yake ahakikishe miradi yote inayotumia fedha za serikali inatekelezwa kwa ufanisi”, aliongeza Waziri Ummy.

Akijibu maombi ya viongozi wa chama na serikali wa mkoa wa Simiyu kuhusu tatizo la usafiri kwa watumishi watakaopangiwa kufanya kazi katika hospitali ya rufaa ambayo kwa sasa haina nyumba za watumishi, Waziri Ummy amewahakikishia kuwa Wizara itaangalia uwezekano wa kuipatia hospitali hiyo basi maalumu la watumishi halikadhalika itaweka bajeti ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika mwaka wa fedha ujao.

Akiwa katika hospitali ya wilaya ya Bariadi ya Somanda, Waziri Ummy alielezea kutoridhiswa na utaratibu wa kutoa huduma katika wodi ya wazazi na kumwagiza mganga mkuu wa mkoa kuzifanyia marekebisho kasoro zote zilizobainika ili huduma zinazotolewa ziendane ni miongozo ya wizara.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amemhakikishia Waziri Ummy kuwa,  mkoa utasimamia kikamilifu utakelezaji wa mradi huo na kusisitiza kuwa pale ambapo pamebainika kuwa na dosari atahakikisha zinarekebishwa ili kuongeza ufanisi katika mradi huo.
“Mhe Waziri mimi nina amini kukamilika kwa hospitali hii ni mkombozi kwa maelfu ya wananchi wetu wa mkoa wa Simiyu,  sasa wajiandae kupata huduma bora zikiwemo za bima ya afya ambazo zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa, kwa ujumla tunaamini zitawahamasisha watu wengi zaidi kujiunga na  huduma hiyo”, alisisitiza RC Mtaka.  

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekamilisha ziara yake mkoani Simiyu na Kuelekea katika mikoa ya Geita na Shinyanga.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika eneo la Nyaumata Kilomita chache kutoka mjini Bariadi
Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Watumishi wa Ngazi mbalimbali kutoka mkoani Simiyu Wakisikiliza Maelekezo ya  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Wakati wa Ziara yake Katika Eneo la Nyaumata inapojengwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka Akimpa Maelezo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipewa maelezo kuhusu Ujenzi wa Jengo jipya litakalotumika kutoa huduma za maabara, upasuaji na mionzi katika eneo la Nyaumata Wilayani Bariadi.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa maelekezo katika eneo la ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu eneo la Nyaumata Wilayani Bariadi.
Mafundi wakiendelea na Shughuli ya ujenzi wa jengo litakalotumika kutoa  huduma za maabara, upasuaji na mionzi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu eneo la Nyaumata wilayani Bariadi.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka wakielekea kukagua Jengo la hospitali ya rufaa ya Mkoa lililokamilika katika eneo la Nyaumata Wilayani Bariadi.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka Mkuu Wakiwasili katika Jengo Jipya la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Eneo la Nyaumata, Wilayani Bariadi.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipewa maelezo katika moja ya chumba cha wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu iliyopo eneo la Nyaumata wilayani Bariadi, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka


Monday, January 21, 2019

Viongozi wa Riadha Kanda ya Ziwa Washauriwa Kuziandaa Timu zao Mapema


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni rais wa chama cha riadha nchini Anthony Mtaka amewaagiza viongozi wa riadha kanda ya ziwa kuweka mpango mkakati endelevu wa kuwatambua na kuwaandaa kikamilifu wachezaji watakaoshiriki katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mhe Mtaka ametoa kauli hiyo katika kikao na viongozi wa vyama vya riadha kanda ya ziwa kilichofanyika mjini Bariadi ambapo amesema chama cha riadha kinakabiliwa na mashindano mbalimbali ikiwemo mbio za nyika za dunia zitakazofanyika nchini Denmark, mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Morocco pamoja na mashindano ya relay yatakayofanyika nchini Japan hivyo ni muhimu maadalizi yakafanyika mapema ili kuwaandaa wachezaji kisaikolojia na hatimaye waweze kurejea na ushindi.

Adha Mhe Mtaka amesema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa kuwapata wachezaji wenye viwango ambapo yatafanyika majaribio nchi nzima ili kuwawezesha viongozi na makocha kubaini vipaji vipya ili wachezaji hao waweze kujumuishwa kwenye timu ya Taifa.

“ Naomba niwahakikishia hatuwezi kupata wachezaji wazuri kama tutakaa tunalalamika, nendeni mkafanye majaribio katika ngazi za mikoa yenu, chagueni wachezaji wazuri ambao tutakuwa na uhakika watarejea na ushindi”.

“ Binafsi ninawaahidi nitawapa msaada wowote mnaohitaji, sote tunafahamu kanda ya ziwa kuna wachezaji wazuri sana, kinachohitajika ni kuweka mfumo mzuri wa kuwatambua na ndio maana tumeamua safari hii tutakuwa na makocha watano kwenye kambi zetu za taifa ambazo tunatarajia kuziweka katika mikoa ya Arusha na Pwani, mimi ninaamini tukidhamiria kuleta mabadiliko katika mchezo huu tunaweza ”, alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho akiwemo mwanariadha  mkongwe ambaye ni mchezaji wa kwanza kushiriki katika michezo ya Olympic mwaka 1964, Mzee Thomas Daniel walimweleza rais wa chama hicho kuwa ukosefu wa viwanja vyenye ubora, kutokuwepo kozi ya makocha wa ngazi ya juu, uhaba wa vifaa pamoja na kozi maalumu kwa ajili ya makocha ni miongoni mwa changamoto zinazohitaji kupatiwa majawabu ili kuongeza hamasa katika mchezo huo.

Kikao hicho cha siku moja kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya riadha kanda ya ziwa kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Mara na Geita.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na rais wa chama cha riadha nchini Anthony Mtaka akiwakaribisha wajumbe wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha riadha ofisini kwake mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni rais wa chama cha riadha nchini Anthony Mtaka akiwa kwenye kikao na viongozi wa vyama vya riadha kanda ya ziwa mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa riadha kutoka mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza na Geita wakiwa katika kikao na rais wa chama hicho mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na rais wa chama cha riadha nchini Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa riadha kutoka mikoa ya Simiyu, Mara,  Geita na Mwanza mara baada ya kikao chao mjini Bariadi.


Friday, January 18, 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aiagiza Mikoa Minane Inayolima Pamba Kuongeza Kasi ya Usimamizi kwa Kutoa Elimu kwa Wakulima, Simiyu Yaahidi Kuongeza Uzalishaji Hadi Tani 240,000, Yajiandaa Kumkwamua Mkulima Kuondokana na Utegemezi wa Mikopo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja   na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa wakifuatilia mkutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference) ulioongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujadili mwendendo wa kilimo cha Pamba.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mkutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference)  kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na wakuu wa mikoa minane inayolima pamba katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu mjini Bariadi.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka  akiwa pamoja na makatibu tawala wasaidi wakifuatilia mkutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference) kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Wakuu wa mikoa minane katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja   na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa wakifuatilia mkutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference) ulioongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akichangia hoja kuhusu mikakati ya kuboresha kilimo cha zao la pamba katika mkutano kwa njia ya mawasiliano ya video (Video Conference) kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Wakuu wa mikoa minane.

Monday, January 14, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka Awapa Somo Wachezaji wa Timu ya Coasta Unioni ya Tanga.

RC Mtaka Awashauri Wachezaji na Viongozi wa Coastal Union kutumia Falsafa ya Michezo ni Ajira na Biashara Kama Njia ya Kuleta Mapinduzi ya Soka Nchini

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewashauri wachezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga kutambua kuwa michezo ni biashara na pia ni ajira hivyo wanapaswa kujiwekea malengo ya muda mrefu na mfupi ili waweze kunufaika na matunda ya jitihada zao.

RC Mtaka ametoa kauli hiyo ofisini kwake mjini Bariadi alipotembelewa na kikosi cha timu hiyo na viongozi wake kilichokuwa kikitokea mkoani Mara kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ambako ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 3 -2 na biashara United.

Katika salamu zake kwa timu hiyo Mtaka amesema njia pekee ya mafanikio kwa timu hiyo na wachezaji wake inaanzia kwenye nidhamu ya wachezaji ndani na nje ya uwanja na pia uwepo wa viongozi makini wanaojitambua na wenye nia ya kuleta mapinduzi ya soka nchini.

“ Binafsi sikubaliani na zile kauli  mbiu za michezo ni afya au michezo ni burudani, naendelea kusisitiza michezo ni biashara halikadhalika michezo ni ajira hivyo kipaji chako ndio mtaji wako”.

“Mkitambua hilo mtafika mbali, tunayo mifano hai, hebu mtazameni mchezaji kama Mbwana Samatta, huyu alijitambua mapema, akajiwekea malengo na ndio maana ameweza kufikia hapo alipo,analipwa mshahara ambao watanzania wachache sana wanaupata”, aliongeza Mtaka.

“Kumbukeni nidhamu ndio muhimili mkubwa utakaowapeleka mbali,achaneni na ulimbukeni wa Usimba na Uyanga, na pia msikubali kuingia katika vishawishi vya kutumia dawa za kulevya, mkifanya hivyo kwa umri wenu huu nawahikikishia mtafika mbali kuliko mnavyotegemea”, alisisitiza RC Mtaka.

Aidha Mtaka pia aliwatolea mfano wachezaji wa zamani kama George Weah ambaye kwa sasa ni rais wa Liberia na golikipa wa zamani wa TP Mazembe Robert Kidiaba Muteba ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa mbunge huko Congo DRC  kuwa ni kielelezo cha nidhamu bora michezoni akisema kuwa kama wangekuwa na sifa mbaya jamii isingeweza kukubali kuwapa nyadhifa kubwa za kisiasa.

Kuhusu uongozi wa vyama vya soka nchini, Mheshimiwa Mtaka amesema ipo haja ya kuvitazama kwa makini zaidi kwani kwa sehemu kubwa ya viongozi wake wanaendesha mambo kijanja kijanja hali inayodhoofisha jitihada za serikali za kuleta mapinduzi ya soka nchini.

“ Mara nyingi huwa najiuliza, hivi kuna haja gani ya kusajili mchezaji wa kigeni kwa mamilioni wakati kiwango chake ni cha chini kuliko wachezaji wetu wa ndani, hawa viongozi wana ajenda gani na soka letu mpaka kufikia maamuzi hayo”, alihoji Mtaka.

 RC Mtaka ameongeza kuwa njia pekee itakayosaidia kuleta mabadiliko ya soka nchini ni mabadiliko ya mitazamo ya viongozi wake ambapo amesema wanapaswa kuweka uzalendo mbele na kuiona michezo kama fursa inayoweza kutangaza utalii wetu kupitia wachezaji waliowahi kutamba au wale wanaogonga vichwa vya habari hivi sasa akitolea mfano wa nchi kama Uganda ambayo baadhi ya mitaa yake imepewa majina ya wachezaji maarufu.

Aidha mheshimiwa Mtaka ambaye pia ni rais wa chama cha riadha nchini amesema kumekuwa na tofauti kubwa ya kimaisha kati ya wanariadha waliopata mafanikio kimichezo miaka ya nyuma na wachezaji wa soka waliowahi kutamba miaka hiyo kutokana na mfumo wa uongozi wa michezo uliopo.

RC Mtaka amesema kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa soka wamejikuta wakiwa taabani kimaisha mara baada ya kustaafu kucheza soka hali ambayo amesema tiba yake itapatikana endapo viongozi na wadau wa soka wataamua kubadili mitazamo yao na kuingia katika medani za soka la kibiashara kama ilivyo kwa nchi nyingi zilizoendelea.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amekiri kuwepo kwa dosari za kiuongozi katika usimamizi wa mipango ya soka nchini na kuahidi kuufanyia kazi ushauri wake pale ambapo umeigusa timu yake.

“ Mheshimiwa mkuu wa mkoa timu yetu ni timu kongwe na imepitia vipindi vingi vya mpito, lakini kama ulivyojionea kwa sasa hali ni tofauti, tuna vijana chipukizi wenye uwezo mkubwa wa kuleta matokeo yatakayo washangaza wengi, binafsi ninaamini tutafika mbali”, aliongeza Mgunda.

Aidha kuhusu ushiriki wa mchezaji wa timu hiyo ambaye pia ni mwanamuziki maarufu wa kizazi kipya Ali Kiba, Mgunda amesema mchezaji huyo ni hazina kubwa ya timu hiyo na kwamba hawawezi kumtumia kwenye mechi za ugenini ambazo mapato yanachukuliwa na timu mwenyeji.

“Ali Kiba ni brand ya Coastal Union, anapoingia uwanjani ni lazima watu wajae kutazama mechi, na sisi kwa kutambua umuhimu wake tutamtumia kwa mechi za nyumbani tu ili pato lote liingie mfukoni kwetu”. Alisisitiza Mgunda.

Timu ya Coastal Union tayari imeondoka mjini Bariadi kuelekea Dar es Salaam kuendelea na michezo yake ya ligi kuu. 


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiwakaribisha viongozi na wachezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga mara baada ya kuwasili mjini Bariadi wakitokea mkoani Mara, kulia ni kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mgunda.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony akiongea na kocha mkuu wa timu ya Coastal Union ya Tanga Juma Mgunda mara baada ya kuwapokea ofisini kwake mjini bariadi.


Wachezaji wa timu ya Coastal Union wakisikiliza maelekezo ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka walipomtembelea ofisini kwake mjini Bariadi wakiwa safarini kutoka mkoani Mara kuelekea Dar es Salaam.

Wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Coastal Union wakiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mjini bariadi wakitokea mkoani Mara.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony akisisitiza jambo wakati akiongea na wachezaji na viongozi wa timu ya Coastal Union ya Tanga ofisini kwake mjini Bariadi.Kocha mkuu wa Timu ya Coastal Union Juma Mgunda pamoja na wachezaji wa timu hiyo wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka walipomtembelea ofisini kwake mjini Bariadi


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akisikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa timu ya Coastal Union ya Tanga walipomtembelea ofisini kwake mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika picha ya pamoja na viongozi wa timu ya Coastal Union ya Tanga  walipomtembelea ofisini kwake mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony akiwasindikiza viongozi na wachezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga kuelekea katika basi lao tayari kwa safari kuelekea Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony akiagana na wachezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga mara baada ya kukamilisha ziara yao ya kimichezo katika mikoa ya kanda ya ziwa .Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony akiagana na kocha mkuu  wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda katika eneo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Bariadi.

Wachezaji na viongozi wa timu ya Coastal Union wakiwa ndani ya basi lao tayari kwa safari kuelekea jijini Dar es Salaam kuendalea na ratiba ya michezo ya ligi kuu.


  Timu ya Coastal Union ikiondoka mjini Bariadi Kuelekea Dar es Salaam kuendelea na michezo ya ligi kuu.

Wednesday, January 9, 2019

RC Mtaka Asema Simiyu imejipanga Kuendesha Biashara Kimkakati

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amezishauri taassi zinazosimamia masuala ya biashara kuwajengea uwezo wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha umuhimu wa kusajili kampuni zao hatua itakayowawezesha kuendesha shughuli zao kwa tija.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu bomba inayoendeshwa na kampuni ya simu ya Haloteli mjini Bariadi,Mtaka amesema ili kuwawezesha wafanyabiashara kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ni muhimu kuandaa mfumo utakaowatambua kuanzia ngazi ya chini hatua itakayosaidia kufuatilia mienendo yao ya kibiashara ikiwemo kuchangia pato la mkoa na taifa kwa ujumla.

“Nawapongeza sana Halotel kwa hatua hii ya ubunifu mliyotuonyesha, ninaamini  huu ni mwanzo mzuri kwenu wa kubuni huduma nyingine muhimu zitakazowasaidia wafanyabiashara na makundi mengine muhimu katika maeneo mbalimbali”.

“Kwa upande wetu Simiyu, sisi ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mifugo mingi nchini halikadalika ni mkoa unaoongoza kwa kilimo cha pamba, hivyo tungefurahi sana endapo Halotel mngekuja na vifurushi vitakavyogusa maeneo hayo ,” alisisitiza Mtaka.

Aidha Mtaka ameishauri kampuni ya simu ya Halotel kuweka utaratibu utakaowawezesha kujitathmini mara kwa mara ili kujua nguvu ya soko lake na mahitaji  ya ziada ya wateja wake hatua itakayoiwezesha kuhimili ushindani na kuwa miongoni mwa kampuni zinazoendesha biashara zake kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wake.

Halikadhalika Mhe Mtaka ameiagiza kampuni ya Godtech kuhakikisha inawaelimisha wajasiliamali wadogo mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki na kusajili biashara zao kupitia mfumo rasmi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali.

“ Naendelea kusisitiza Simiyu tumejiandaa kuendesha biashara zetu kimkakati, ili kutekeleza adhma hii kwa vitendo, wafanyabiashara  wetu wataendelea kufanya biashara saa 24, lakini pia ninakuagiza mheshimiwa DC fungeni taa sokoni kuruhusu biashara zifanyike mpaka saa nne usiku”, aliongeza RC Mtaka.

Kwa upande wake balozi wa kapeni ya Kitu bomba ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu nchini Jackob Stephen maarufu kama JB ameahidi kuzitangaza kikamilifu fursa zinazopatikana mkoani Simiyu kupitia kampeni hiyo huku akiwataka vijana wenye vipaji kuitumia nafasi hiyo kukuza vipaji vyao.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ya Kitu Bomba inayolenga kuwajengea uwezo wananchi katika kupambana na umasikini iliyozinduliwa  mjini Bariadi umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wadau wa maendeleo.

MwishoMgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu bomba mhe Anthony Mtaka akizindua duka la kutoa huduma za kampuni ya halotel mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu Anthony Mtaka  akiwahutubia wageni waalikwa   katika ukumbi wa MS mjini Bariadi katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitu Bomba inayoendeshwa na kampuni ya Halotel. 
Balozi wa kampeni ya Kitu Bamba Jackob Stephen akifafanua jambo kuhusu matumizi ya  bidhaa za halotel katika ukumbi wa MS mjini Bariadi katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu bomba.
Watumishi na watoa huduma wa kampuni ya halotel wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu bomba katika ukumbi wa MS mjini Bariadi.

Monday, January 7, 2019

DKT. BASHIRU AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUJIFUNZA KUFANYA MAAMUZI KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewataka Watumishi wa Serikali  kujifunza kufanya maamuzi  kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo mjini Bariadi katika kikao na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kujenga kiwanda cha (vifaa tiba) bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, ambacho kililenga kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Dkt. Bashiru  amesema watumishi wa serikali waache tabia ya kuzungumza bila kutenda badala yake wawe na moyo wa uzalendo na wafanye maamuzi sahihi kwa muda muafaka huku akisisitiza kuwa hawapaswi kuwa sehemu ya vikwazo katika  maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.

“Watumishi wa Serikali jifunzeni kutoka  kwenye tabia ya Rais wetu, fanyeni maamuzi kwa maslahi mapana ya Taifa, muwe na moyo wa uzalendo na ujasiri katika kuchukua maamuzi; maamuzi hayo yafanyike kwa usahihi kwa muda muafaka” alisema Dkt.. Bashiru.

Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zinazotokana na zao la pamba mkoani Simiyu, Dkt. Bashiru alioneshwa kutoridhishwa na kasi ya maandalizi ya ujenzi huo  na   kumwagiza Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji (TIC), Bw. Godfrey Mwambe  kuratibu mazungumzo ya kuwakutanisha wahusika wote ili utekelezaji wa mradi uanze mara moja.

“Tulikubaliana kazi itaanza Desemba 2018 na Desemba imeshapita, tumedhamiria na tumeshatamka kuwa tutajenga viwanda, hatuwezi tukakwamisha mipango ya kujenga viwanda na wakati tumeamua kujenga uchumi wa viwanda hapana; Tarehe 09 Januari saa 3:00 asubuhi wale wote wanaohusika na ujenzi wa kiwanda hiki tukutane Lumumba tuzungumze” alisema Dkt. Bashiru.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema viongozi wa Serikali wanaohusika katika kutoa maamuzi yatakayopelekea ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba  wachukue hatua,  ili wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba waanze kujua mahitaji ya pamba itakayotumika na kiwanda hicho katika msimu wa mwaka 2018/2019.

“Yapo mambo tulikubaliana kufikia Desemba 2018 yawe yamekamilika, tunaomba kama kuna mambo bado yako mezani yaondoke jambo hili liweze kusogea, taratibu za manunuzi zianze ili hatua za kutengeneza mashine zifanyike na kupitia pamba itakayoanza kununuliwa mwezi Mei, wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba waanze kujua mahitaji ya kiwanda katika msimu wa mwaka 2018/2019, ili kiwanda kisije kikakamilika pamba ikakakosekana” alisema Mtaka.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Bw. Marco Mtunga amesema upatikanaji wa malighafi ya kiwanda cha vifaa tiba (bidhaa za afya zitokanazo na zao la pamba)  kinachotarajiwa kujengwa Bariadi ni wa uhakika na kubainisha kuwa Bodi hiyo imejiwekea malengo ya kuzalisha tani milioni moja ifikapo mwaka 2022.

Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Bernad Konga amesema tayari bodi ya mfuko huo imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kuwekeza katika  ujenzi wa kiwanda cha (vifaa tiba) bidhaa za afya zitokanazo na pamba mkoani Simiyu, lengo likiwa ni kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi na kuongeza thamani ya zao la pamba nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD), Bw. Laurian Rugambwa amesema bidhaa za afya zitokanazo zao la pamba zitakazozalishwa na kiwanda hicho zitapata soko la uhakika katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara(SADC) na hapa nchini kupitia Bohari hiyo, kwa kuwa sasa bidhaa hizo zinaagizwa nje ya nchi.

Baadhi ya wawekezaji wa viwanda vya kuchambua pamba mkoani Simiyu wamesema pamoja na kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba njia kuu ya kuongeza thamani ya zao la pamba ni kujenga viwanda vya nyuzi na nguo, huku wadau wa wakitoa maoni yao
.
“Tunapaswa kuongeza thamani ya zao la pamba ili wakulima waweze kunufaika na uzalishaji wanaofanya, moja ya njia kuu ya kuongeza thamani ni uwekezaji katika viwanda vya nyuzi na nguo, huu ni uwekezaji mkubwa unaotoa ajira nyingi, Serikali ingalie upya sera, sheria na kodi zinazogusa uwekezaji katika eneo hili” alisema Salum Khamis mwekezaji Shinyanga.

“Ipo haja ya kwenda kwenye uwekezaji katika viwanda vya nyuzi na nguo hapa nchini  na kwa sababu sisi ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa pamba Afrika, tukitegemea sana soko la nje kwa siku zijazo tunaweza kukwama hasa katika suala bei ya pamba” alisema Boaz Ogola Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery.

Kiwanda cha Bidhaa za afya zitokanazo na zao la pamba kinatarajiwa kujengwa mwaka huu 2019 katika Kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ambapo ujenzi huo umeshirikisha Taasisi nyingine za Umma ambazo ni wadau muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa ufanisi.

Taasisi hizo ni Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB Corporate) na Bohari ya Dawa  ya Taifa (MSD).
MWISHO


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa nne kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tatu kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa huo, wakuu wa taasisi zaumma ofisini kwake mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenziwa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba. Mwekezaji na Mbunge wa Meatu, Mhe. Salum Khamis akichangia hoja  katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Mwekezaji katika zao la pamba , Bw. Gungu Silinga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mtaalam wa masuala ya Viwanda kutoka TIRDO, Bw. Ndaki Mnyeti akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji cha Taifa(TIC), Bw. Godfrey Mwambe (wa tatu kushoto walioketi) akizungumza jambo na na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, wakuu wa taasisi za umma mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge(wa pili kulia) akizungumza jambo na na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, wakuu wa taasisi za umma mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
 Baadhi ya viongozi wakiwa katika katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba. Naibu Waziri wa madini na Mbunge wa Maswa Mashariki, Mhe. Stanslaus Nyongo akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.


Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa SIMIYU, Ndg. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!