Monday, January 7, 2019

DKT. BASHIRU AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUJIFUNZA KUFANYA MAAMUZI KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewataka Watumishi wa Serikali  kujifunza kufanya maamuzi  kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo mjini Bariadi katika kikao na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kujenga kiwanda cha (vifaa tiba) bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, ambacho kililenga kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Dkt. Bashiru  amesema watumishi wa serikali waache tabia ya kuzungumza bila kutenda badala yake wawe na moyo wa uzalendo na wafanye maamuzi sahihi kwa muda muafaka huku akisisitiza kuwa hawapaswi kuwa sehemu ya vikwazo katika  maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.

“Watumishi wa Serikali jifunzeni kutoka  kwenye tabia ya Rais wetu, fanyeni maamuzi kwa maslahi mapana ya Taifa, muwe na moyo wa uzalendo na ujasiri katika kuchukua maamuzi; maamuzi hayo yafanyike kwa usahihi kwa muda muafaka” alisema Dkt.. Bashiru.

Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zinazotokana na zao la pamba mkoani Simiyu, Dkt. Bashiru alioneshwa kutoridhishwa na kasi ya maandalizi ya ujenzi huo  na   kumwagiza Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji (TIC), Bw. Godfrey Mwambe  kuratibu mazungumzo ya kuwakutanisha wahusika wote ili utekelezaji wa mradi uanze mara moja.

“Tulikubaliana kazi itaanza Desemba 2018 na Desemba imeshapita, tumedhamiria na tumeshatamka kuwa tutajenga viwanda, hatuwezi tukakwamisha mipango ya kujenga viwanda na wakati tumeamua kujenga uchumi wa viwanda hapana; Tarehe 09 Januari saa 3:00 asubuhi wale wote wanaohusika na ujenzi wa kiwanda hiki tukutane Lumumba tuzungumze” alisema Dkt. Bashiru.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema viongozi wa Serikali wanaohusika katika kutoa maamuzi yatakayopelekea ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba  wachukue hatua,  ili wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba waanze kujua mahitaji ya pamba itakayotumika na kiwanda hicho katika msimu wa mwaka 2018/2019.

“Yapo mambo tulikubaliana kufikia Desemba 2018 yawe yamekamilika, tunaomba kama kuna mambo bado yako mezani yaondoke jambo hili liweze kusogea, taratibu za manunuzi zianze ili hatua za kutengeneza mashine zifanyike na kupitia pamba itakayoanza kununuliwa mwezi Mei, wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba waanze kujua mahitaji ya kiwanda katika msimu wa mwaka 2018/2019, ili kiwanda kisije kikakamilika pamba ikakakosekana” alisema Mtaka.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Bw. Marco Mtunga amesema upatikanaji wa malighafi ya kiwanda cha vifaa tiba (bidhaa za afya zitokanazo na zao la pamba)  kinachotarajiwa kujengwa Bariadi ni wa uhakika na kubainisha kuwa Bodi hiyo imejiwekea malengo ya kuzalisha tani milioni moja ifikapo mwaka 2022.

Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Bernad Konga amesema tayari bodi ya mfuko huo imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kuwekeza katika  ujenzi wa kiwanda cha (vifaa tiba) bidhaa za afya zitokanazo na pamba mkoani Simiyu, lengo likiwa ni kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi na kuongeza thamani ya zao la pamba nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD), Bw. Laurian Rugambwa amesema bidhaa za afya zitokanazo zao la pamba zitakazozalishwa na kiwanda hicho zitapata soko la uhakika katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara(SADC) na hapa nchini kupitia Bohari hiyo, kwa kuwa sasa bidhaa hizo zinaagizwa nje ya nchi.

Baadhi ya wawekezaji wa viwanda vya kuchambua pamba mkoani Simiyu wamesema pamoja na kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba njia kuu ya kuongeza thamani ya zao la pamba ni kujenga viwanda vya nyuzi na nguo, huku wadau wa wakitoa maoni yao
.
“Tunapaswa kuongeza thamani ya zao la pamba ili wakulima waweze kunufaika na uzalishaji wanaofanya, moja ya njia kuu ya kuongeza thamani ni uwekezaji katika viwanda vya nyuzi na nguo, huu ni uwekezaji mkubwa unaotoa ajira nyingi, Serikali ingalie upya sera, sheria na kodi zinazogusa uwekezaji katika eneo hili” alisema Salum Khamis mwekezaji Shinyanga.

“Ipo haja ya kwenda kwenye uwekezaji katika viwanda vya nyuzi na nguo hapa nchini  na kwa sababu sisi ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa pamba Afrika, tukitegemea sana soko la nje kwa siku zijazo tunaweza kukwama hasa katika suala bei ya pamba” alisema Boaz Ogola Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery.

Kiwanda cha Bidhaa za afya zitokanazo na zao la pamba kinatarajiwa kujengwa mwaka huu 2019 katika Kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ambapo ujenzi huo umeshirikisha Taasisi nyingine za Umma ambazo ni wadau muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa ufanisi.

Taasisi hizo ni Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB Corporate) na Bohari ya Dawa  ya Taifa (MSD).
MWISHO


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa nne kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tatu kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa huo, wakuu wa taasisi zaumma ofisini kwake mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenziwa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.



 Mwekezaji na Mbunge wa Meatu, Mhe. Salum Khamis akichangia hoja  katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Mwekezaji katika zao la pamba , Bw. Gungu Silinga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mtaalam wa masuala ya Viwanda kutoka TIRDO, Bw. Ndaki Mnyeti akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji cha Taifa(TIC), Bw. Godfrey Mwambe (wa tatu kushoto walioketi) akizungumza jambo na na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, wakuu wa taasisi za umma mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge(wa pili kulia) akizungumza jambo na na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(kulia),  baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, wakuu wa taasisi za umma mara baada ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
 Baadhi ya viongozi wakiwa katika katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.



 Naibu Waziri wa madini na Mbunge wa Maswa Mashariki, Mhe. Stanslaus Nyongo akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.


Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa SIMIYU, Ndg. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kujenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama na Serikali na  wawekezaji katika zao la pamba mkoani Simiyu, kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili ujenzi wa kiwanda hicho na mnyororo wa thamani wa zao la pamba.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!