Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally
amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya
kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na
uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza
na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini
Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali
wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna
wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za
maendeleo.
“Niwapongeze
kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005
kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa
hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi
sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya
kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema
Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye
manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni
wazalishaji wadogo hususani katika katika sekta ya kilimo na viwanda huku
akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo
viwanufaishe wengi.
Ameongeza kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga
mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ni vema kukawa na mpango wa
matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa watumiaji ambayo inakuwa
chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.
Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga
kuhakikisha kuwa itasimamia na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na
wataalam wenye taaluma na maadili ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na
kutatua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema
kuwa Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji
wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa
Simiyu zitasimamiwa vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.
Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti
kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)
ili kubaini fursa za kiuchumi zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji
vyote 470, ambapo utekelezaji wa Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP)
unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Februari.
Ameongeza kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo
wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000 kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha
vifungashio (Maswa) kiwanda cha bidhaa 18 za afya zitokanazo na pamba(Bariadi) vitajengwa mwaka huu 2019 Simiyu.
“Ndugu Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais
anapokea ndege ya Air Bus alicheza muziki na
ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha yake,
ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu” alisema Mtaka.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye
ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha
uhusiano mzuri, kusaidiana na kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi
viongozi kulinda na kuheshimu dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.
Akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa
Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew Chenge ametoa wito kwa viongozi na
wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha upendo, umoja na mshikamano hususani
katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko
Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo.
MWISHO
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na
Serikali mkoani Simiyu, katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James
na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt.
Bashiru Ally wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt.
Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019
wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
mhe. Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha
Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya
Itilima Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kuwasili wilayani humo kuweka jiwe la
msingi la Ofisi ya CCM ya Wilaya, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu
Januari 05, 2019 .
Baadhi
ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati
wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo
pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara
ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019.
Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Itilima, Mahamoud Mabula(kushoto) akitoa maelezo ya jengo la Ofisi ya
CCM wilaya kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(katikati) wakati
alipokuwa akikagua jengo hilo kabla ya kuliwekea jiwe la msingi, wakati akiwa
katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally(kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Enock Yakobo mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya
ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019.
Viongozi wa Wilaya ya
Itilima wakimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM Wilaya wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya
CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Enock Yakobo wakifurahia jambo
katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na
watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali
mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa
ziara yake mkoani hapa.
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tatu kulia) akifurahia jambo na baadhi ya viongozi
wa CCM wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya
CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.
Mbunge wa Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge akizungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima wakati wa ziara ya
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally
ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.
Mwenyekiti wa UVCCM na
Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kheri James akizungumza katika kikao cha
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi
na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika
Mjini Bariadi Januari 05, 2019
Baadhi
ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt.
Bashiru Ally(hayupo pichani) katika
kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
Januari 05, 2019
Baadhi ya watendaji,
viongozi wa dini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu
wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)
katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
Januari 05, 2019.
Baadhi ya watendaji,
viongozi wa dini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu
wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)
katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
Januari 05, 2019.
Vijana wa Chipukizi
Wilaya ya Busega wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally
mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na
Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika
Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mabula(kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu
wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally (wa tano kulia) kabla ya kumkabidhi zawadi
aliyoandaliwa na viongozi wa wilaya hiyo,
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM wilaya wakati akiwa
katika ziara yake mkoani Simiyu, Januari 05, 2019.
Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (kushoto) akizungumza mara baada ya kumpokea
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(mwenye skafu) kutoka mkoani Mara, kwa ajili ya kuanza ziara
mkoani Simiyu Januari 05,2019
Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Lydia Bupilipili
wakifurahia jambo katika Mji Mdogo wa Lamadi wakati wamapokezi ya Katibu Mkuu
wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)
ametokea mkoani Mara kwenda Simiyu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
Januari 05-06, 2019.
Baadhi ya viongozi wa
UWT mkoani Simiyu wakimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa
pili kulia) zawadi, wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu Januari 05,
2019.
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya watumishi na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya k kikao
chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
Januari 05, 2019.
Baadhi ya viongozi wa
CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa
Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa
Januari 05 na Januari 06 , 2019.
0 comments:
Post a Comment