Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara mkoani hapa kuwa Serikali itatatua
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji na umeme kupitia mradi wa maji wa
ziwa Victoria, uimarishwaji wa mamlaka za maji na kujengwa kwa vituo vya
kupozea umeme.
Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa
hoteli ya Sweet Dreams iliyoko Mjini Bariadi na kumpongeza mfanyabiashara John
Sabu kwa uwekezaji huo.
Amesema
Mkoa unaendelea kuimarisha vyanzo vya maji na mamlaka za maji na kufikia mwaka
2020 maji kutoka Ziwa Victoria yatakuwa yameshafika katika makao makuu ya mkoa,
huku akibainisha kuwa tatizo la umeme litatatuliwa na ujenzi wa vituo vya
kupozea umeme.
“Sisi
tuna mradi mkubwa wa maji wa Ziwa
Victoria ambao (kwa maelezo ya Waziri wa Maji) mpaka mwezi Februari 2019
watakuwa wametangaza zabuni ya ujenzi wa mradi huo ili maji yafike hapa, kwa
kuanza mpaka kufikia mwaka 2020 maji yatakuwa yamefika makao makuu ya mkoa”
“Kwenye
umeme tumezungumza na watu wa Wizara ya Nishati, tutajengewa (sub-stations)
vituo viwili vya kupozea umeme, kwa kuanzia kimoja kitajengwa mwaka huu kwa
hiyo tutakuwa na umeme wa uhakika” alisisitiza Mtaka.
Katika
hatua nyingine Mtaka amewataka Wakuu wa Wilaya kuwalinda wafanyabiashara
wakubwa na wadogo na kuwasaidia kutafsiri sheria, miongozo na taratibu
zinazopaswa kuwasaidia kufanya biashara zao katika mazingira mazuri, huku
akisisitiza biashara ziendelee kufanyika saa 24.
Kwa
upande wao Wafanyabiashara wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka kwa kuwaruhusu kufanya biashara saa 24 na wakamuahidi kuwa wataendelea
kuwekeza katika ujenzi wa vitega uchumi mbalimbali ikiwemo hoteli za kisasa na
kuendelea kuwa walipa kodi waaminifu.
“Tunamshukuru
Mhe. Mkuu wa mkoa kwa kuruhusu wafanyabishara tufanye biashara zetu saa 24
tunamuahidi kuwa tutaendelea kufungua biashara mbalimbali kama hoteli ili kuondoa adha ya malazi kwa wageni
wanaofika hapa mkoani, pia tutaendelea kuwa walipa kodi halali wa nchi yetu”
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mhe. Njalu Silanga.
Awali
akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Hoteli ya Sweet Dreams mtoto wa Mmiliki wa
hoteli hiyo, Mary John Sabu amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka kwa ubunifu na ushawishi wake uliopelekea matukio mengi ya Kitaifa kufanyika
mkoani Simiyu, ambayo yamechangia kuongeza mzunguko wa biashara mkoani hapa.
MWISHO
Kutoka
kushoto Mfanyabiashara wa Bariadi Bw. John Sabu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara mkoa wa Simiyu, Mhe. Njalu
Silanga wakiteta jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu
Silanga akizungumza na wafanyabiashara na viongozi wa mkoa huo, wakati wa hafla
ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kushoto) akisalimiana na Bibi.
Elizabeth Mlanda mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda mara
baada ya kutoa pongezi kwa Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli
ya Sweet Dreams, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara
kutoka Mjini Bariadi Bw. Yuma akimpongeza Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli
ya Sweet Dreams (aliyeshika kinasa sauti)wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli
hiyo Mjini Bariadi.
Sehemu
ya Jengo la Hoteli ya Sweet Dreams(ghorofa) iliyopo Mjini Bariadi iliyofunguliwa
hivi karibuni.
Katibu
Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Tano Mwera wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams
Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wafanyabiashara na wadau wa maendeleo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya
Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara
John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams na mkewe wakiingia katika hafla ya
ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Watoto
wa Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams wakiwasilisha
risala ya ujenzi wa hoteli hiyo katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara
John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams (kushoto) akizungumza na baadhi ya
wafanyabiashara wenzake katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo katika hafla ya ufunguzi
wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye
pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw.
Jumanne Sagini wakiteta jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet
Dreams Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya JB wakitoa burudani wakati wa wa hafla ya ufunguzi
wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara
Bw. James Nchubi akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) mara baada ya kutoa pongezi kwa Mfanyabiashara
John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams, wakati wa hafla ya ufunguzi wa
Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, wafanyabiashara na wadau wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla
ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Sehemu
ya Jengo la Hoteli ya Sweet Dreams(ghorofa) iliyopo Mjini Bariadi iliyofunguliwa
hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment