Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka amezishauri taassi zinazosimamia masuala ya biashara kuwajengea
uwezo wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha umuhimu wa kusajili
kampuni zao hatua itakayowawezesha kuendesha shughuli zao kwa tija.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu bomba inayoendeshwa na kampuni ya simu ya
Haloteli mjini Bariadi,Mtaka amesema ili kuwawezesha wafanyabiashara kwenda
sambamba na mabadiliko ya teknolojia ni muhimu kuandaa mfumo utakaowatambua
kuanzia ngazi ya chini hatua itakayosaidia kufuatilia mienendo yao ya
kibiashara ikiwemo kuchangia pato la mkoa na taifa kwa ujumla.
“Nawapongeza sana
Halotel kwa hatua hii ya ubunifu mliyotuonyesha, ninaamini huu ni mwanzo mzuri kwenu wa kubuni huduma
nyingine muhimu zitakazowasaidia wafanyabiashara na makundi mengine muhimu
katika maeneo mbalimbali”.
“Kwa upande wetu Simiyu,
sisi ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mifugo mingi nchini halikadalika ni
mkoa unaoongoza kwa kilimo cha pamba, hivyo tungefurahi sana endapo Halotel
mngekuja na vifurushi vitakavyogusa maeneo hayo ,” alisisitiza Mtaka.
Aidha Mtaka ameishauri
kampuni ya simu ya Halotel kuweka utaratibu utakaowawezesha kujitathmini mara
kwa mara ili kujua nguvu ya soko lake na mahitaji ya ziada ya wateja wake hatua itakayoiwezesha
kuhimili ushindani na kuwa miongoni mwa kampuni zinazoendesha biashara zake kwa
kuzingatia mahitaji ya wateja wake.
Halikadhalika Mhe Mtaka
ameiagiza kampuni ya Godtech kuhakikisha inawaelimisha wajasiliamali wadogo
mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki na kusajili biashara zao kupitia mfumo rasmi
ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali.
“ Naendelea kusisitiza
Simiyu tumejiandaa kuendesha biashara zetu kimkakati, ili kutekeleza adhma hii
kwa vitendo, wafanyabiashara wetu
wataendelea kufanya biashara saa 24, lakini pia ninakuagiza mheshimiwa DC
fungeni taa sokoni kuruhusu biashara zifanyike mpaka saa nne usiku”, aliongeza
RC Mtaka.
Kwa upande wake balozi
wa kapeni ya Kitu bomba ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu nchini Jackob
Stephen maarufu kama JB ameahidi kuzitangaza kikamilifu fursa zinazopatikana
mkoani Simiyu kupitia kampeni hiyo huku akiwataka vijana wenye vipaji kuitumia nafasi
hiyo kukuza vipaji vyao.
Uzinduzi wa kampeni
hiyo ya Kitu Bomba inayolenga kuwajengea uwezo wananchi katika kupambana na umasikini
iliyozinduliwa mjini Bariadi
umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wadau wa
maendeleo.
Mwisho
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya
kitu bomba mhe Anthony Mtaka akizindua duka la kutoa huduma za kampuni ya
halotel mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Anthony Mtaka
akiwahutubia wageni waalikwa katika ukumbi wa MS mjini Bariadi katika
hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitu Bomba inayoendeshwa na kampuni ya Halotel.
Balozi wa kampeni ya Kitu Bamba Jackob Stephen
akifafanua jambo kuhusu matumizi ya bidhaa
za halotel katika ukumbi wa MS mjini Bariadi katika hafla ya uzinduzi wa
kampeni ya kitu bomba.
|
Watumishi na watoa huduma wa kampuni ya halotel
wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitu
bomba katika ukumbi wa MS mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment