Wednesday, August 29, 2018

RITA KUSAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA ZAIDI YA WANAFUNZI 60,000 WILAYANI BARIADI


Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) unatarajia kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi 60,000 wa shule za Msingi za Sekondari wilayani Bariadi mkoani Simiyu, kupitia Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa miaka 06 hadi 18.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw. Charles Salyeem wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.

Salyeem amesema mpango huo utahusisha usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka 06 hadi 18 kwa ushirikiano kati ya RITA na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia Idara za Elimu ambapo wanafunzi watasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa katika shule zao.

Ameongeza kuwa watoto wa umri wa miaka 06 hadi 18 ambao si wanafunzi watapata fursa ya kusajiliwa katika Ofisi za Watendaji wa Kata, huku akibainisha kuwa watapaswa kuwa na viambatisho vya msingi vinavyotakiwa kwa maelekezo watakayopewa na Watendaji wa Kata kwenye maeneo yao.

Aidha, Salyeem amesema wazazi na walezi wa watoto wenye umri huo watahitajika kuchangia gharama kwa ajili ya usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao  ili fedha zitakazopatikana  ziwezeshe kupeleka mpango huu katika maeneo mengine.

Awali akifungua mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata kuhusu mpango huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewatakaWaratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuzingatia maelekezo watakayopewa na kufanya kazi kwa uadilifu wakitanguliza uzalendo na siyo maslahi binafsi.

Aidha,Kiswaga amesema cheti cha kuzaliwa ni moja ya nyaraka muhimu kwa wanafunzi wanaotoka hatua moja ya masomo kuingia nyingine hivyo akawataka viongozi na watendaji kujipanga ili kuvuka lengo la RITA la kusajili wanafunzi 60,000 kwa kuhakikisha kila fomu inayochukuliwa kwa ajili ya kuomba usajili inarudishwa na cheti cha kuzaliwa kinachukuliwa.

“RITA imejiwekea lengo la kusajili wanafunzi 60,000 kati ya zaidi ya 156,769 waliopo wilayani Bariadi, wanafunzi wasio na vyeti ni wengi, hivyo basi tujipange tuweze kuvuka lengo, tutumie viongozi kuhamasisha wazazi na kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa” alisema.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Ihusi, Kasimili Ngusa amesema mpango huu utawarahisishia wanafunzi wengi wa umri wa miaka 06 hadi 18 kwa kupata vyeti vya kuzaliwa shuleni walipo, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo iliwalazimu wazazi na walezi kufuata huduma ya usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.

Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Isanga, Sophia Kitobelo ametoa wito kwa wazazi na walezi kutumia fursa hiyo ya kusajili na kuchukua vyeti vya kuzaliwa shuleni na katika Ofisi za kata, kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata vyeti vya kuzaliwa ambavyo ni miongoni mwa nyaraka muhimu kwa Watanzania.

Mkakati huu wa Usajili wa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wenye umri wa miaka 06 hadi 18 umefunguliwa rasmi katika Wilaya ya Bariadi na baadaye utaendelea katika wilaya nyingine za Mkoa wa Simiyu; hadi sasa umeanza kutekelezwa katika wilaya kumi na moja za Mikoa miwili ya Dar es Salaam, Mara na Njombe.
MWISHO

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw. Charles Salyeem akitoa taarifa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  akifungua mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah wakiteta jambo wakati ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi waWilaya ya Bariadi wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji Kata wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Meneja Usajili RITA , Bi. Patricia Mpuya akiwasilisha mada katika  mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi waWilaya ya Bariadi wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata  kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018  mjini Bariadi.

Monday, August 27, 2018

DARASA LA SABA SIMIYU WAOMBA WASIMAMIZI WENYE TABIA YA KUWATISHA WATAHINIWA WAACHE


Wanafunzi wa darasa la saba shule za msingi za Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wamemuomba Mkuu wa Mkoa, Mhe Anthony Mtaka, kuwataka  wasimamizi wa Mtihani wa Taifa wenye tabia ya kuwatisha wanafunzi wakiwa katika chumba cha mtihani waache tabia hiyo ili wanafunzi wafanye Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, mwaka 2018 kwa uhuru pasipo uoga.

Wanafunzi hao wametoa ombi hilo Agosti 27, 2018, wakati Mkuu Mkuu huyo wa Mkoa alipokutana na wanafunzi wa darasa la saba takribani 782 wa shule tano za msingi za Mjini BARIADI, katika Shule ya Msingi Sima B, lengo likiwa ni kuwahimiza kusoma kwa bidii katika siku chache zilizobakia na kuwatakiwa kila la heri katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.

Wamesema kuwa wamepata taarifa kutoka kwa wenzao waliowatangulia kuwa siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba ambao walikuwa wakiwatisha na kuwanyanyasa watahiniwa, hivyo kuwafanya wanafunzi kufanya mtihani wakiwa na hofu jambo lililofanya baadhi yao kushindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

“ Miaka ya nyuma tunasikia kuna wasimamizi walikuwa wanawatishia sana wanafunzi, tunaomba  Mkuu wa mkoa utusaidie na sisi wasije wakatutishia tukashindwa kufanya mtihani wetu wa Taifa vizuri” alisema John Isack Mwanafunzi wa darasa la Saba Shule ya Msingi Sima A, Bariadi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wanafunzi hao kuwa hakutakuwa na vitisho wala manyanyaso yoyote kutoka kwa wasimamizi wa mitihani na akawaeleza kuwa atakutana na wasimamizi wa mitihani ambao wapo katika semina elekezi na  kuwapa angalizo hilo.

“Nikitoka hapa sasa hivi naenda kuongea na wasimamizi wa mitihani, niwahakikishie tu kwamba hamtatishwa msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni kujisomea mjiandae vizuri na mtihani na mkiwa kwenye chumba cha mtihani mkawe watulivu na kumwomba Mungu awakumbushe yote mliyokuwa mnajisomea” alisema Mtaka.

Akizungumza na wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba, Mtaka amewataka wasimamizi hao ambao ni walimu kuwasimamia wanafunzi hao huku wakitambua kuwa wao ni walezi, hivyo wanapaswa kusimamia kwa kufuata taratibu zilizowekwa pasipo kuwatisha wala kuwanyanyasa watahiniwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa mwanafunzi wa kiume, milioni moja na laki tano kwa mwanafunzi wa kike atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka 2018 na shilingi milioni tatu kwa Shule ya Msingi ya Mkoa huo itakayokuwa miongoni mwa shule kumi bora Kitaifa.

Nao wanafunzi wa Darasa la Saba Mjini Bariadi wamemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watafanya vizuri katika Mtihani wa Taifa kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao katika shule zao na katika kambi za Kitaaluma walizokaa kwa siku 21 mwezi Juni kujiandaa na mtihani huo.

“Tunakushukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kutuwezesha kuwa na kambi za kitaaluma, zimetusaidia kutuandaa na mtihani wa Taifa maana tulijifunza vitu vingi, tukapata maarifa mapya, sasa pia hivi walimu wetu wametuandaa vizuri tuko tayari kwa Mtihani wa Taifa, tunakuahidi tutafanya vizuri” alisema Hilda Mgalula Mwanafunzi wa darasa la saba Sima B.

Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime amesema jumla ya watahiniwa elfu 35 Mkoani Simiyu wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la saba Septemba tano na sita, mwaka 2018.

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi kwa lengo la kuwatakia kila la heri katika mitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Kumaliza Elimu ya Msingi utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi wakinyosha mikono ili kujibu maswali waliyokuwa wakiulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwa lengo la kuwatakia kila la heri wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Kumaliza Elimu ya Msingi utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018
John Isack mwanafunzi wa darasa la saba kutoka Shule ya Msingi SIMA A Mjini Bariadi akiwasilisha ombi lake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza na waannfunzi wa darasa la saba wa Shule tano mjini Bariadi kwa lengo la kuwatakia kila la heri wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Mwalimu Aloyce Masejo kutoka Shule ya Msingi SIMA mjini Bariadi akizungumza na wanafunzi na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi ambao walikusanyika kuzzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kwa lengo la kuwatakia kila la heri katikamitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Kumaliza Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi kwa lengo la kuwatakia kila la heri katika mitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Kumaliza Elimu ya Msingi utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi kwa lengo la kuwatakia kila la heri katika mitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.

Baadhi ya walimu ambao wasimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba Mkoani Simiyu  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka  wakati alipozungumza nao wakiwa katika semina elekezi  Mjini Bariadi, kwa ajili ya maandalizi kuelekea katika usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba utakaofanyika   Septemba 05 na 06, 2018.
Baadhi ya walimu ambao wasimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba Mkoani Simiyu  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka  wakati alipozungumza nao wakiwa katika semina elekezi  Mjini Bariadi, kwa ajili ya maandalizi kuelekea katika usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba utakaofanyika   Septemba 05 na 06, 2018.
Hanifa Makoti  mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Bariadi, akizungumza jambo wakati wanafunzi wa shule tano za msingi mjini Bariadi walipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kuzungumza nao kwa lengo la kuwatakia kila la heri katika mitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Isack Sayi mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Sima A,  akizungumza jambo wakati wanafunzi wa shule tano za msingi mjini Bariadi walipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na kuzungumza nao kwa lengo la kuwatakia kila la heri katika mitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.
Mwalimu Janeth Kato kutoka Shule ya Msingi Bariadi mjini Bariadi akizungumza na wanafunzi na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba Mjini Bariadi ambao walikusanyika kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kwa lengo la kuwatakia kila la heri katikamitihani yao wanapojiandaa kuelekea kwenye Mtihani wa Taifa  wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.

Tuesday, August 21, 2018

HALMASHAURI ZAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE VIWANJA VINAVYOPIMWA MKOANI SIMIYU


Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu zinawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza kwenye jumla ya viwanja 3758 vilivyopimwa na vinavyotarajiwa kupimwa kwa nyakati tofauti.

Hayo yamebainishwa na Viongozi wa Halmashauri hizo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi,watumishi na wadau mbalimbali waliofanikisha, kilichofanyika Agosti 20, Mjini Bariadi.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo amesema Halmashauri yake inatarajia kupima viwanja 758 katika eneo la Maperani, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akibainisha kuwa Halmashauri hiyo kuanzia Septemba Mosi, 2018 itaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko amesema Halmashauri hiyo imeanza kupima viwanja 2000 Agosti 20, 2018  katika eneo ambalo liko umbali wa chini ya kilomita moja kutoka Ziwa Victoria, pia imetenga ekari zaidi ya 2000 kwa ajili ya uwekezaji na akasisitiza kuwa ardhi itatolewa bure kwa wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda.

Viongozi hao  wametoa wito kwa wafanyabiashara, wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa wa Simiyu,Taasisi, mashirika, makampuni na wananchi kujitokeza kununua viwanja hivyo kwa ajili ya kuviendeleza kwa uwekezaji na kubainisha kuwa maeneo yote yanayotarajiwa kupimwa Bariadi, Maswa na Busega ni ya kimkakati katika uwekezaji.

"Kuanzia tarehe 01 Septemba, tutaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka Maswa, ni eneo la kimkakati katika uwekezaji kwa sababu patapitiwa na Standard Gauge(Reli ya Kisasa) na patajengwa dry port (bandari kavu), nitoe wito kwa wafanyabiashara kuja kununua viwanja Malampaka kwa ajili ya kufanya uwekezaji mbalimbali; kwa wale wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda sisi Maswa tutatoa ardhi bure" alisema Dkt. Sagamiko.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Mkoa huo kuwekeza katika Ujenzi wa Hoteli, Nyumba za kulala wageni na kumbi za mikutano hususani katika Eneo la Uwanja wa Nanenane Nyabindi na maeneo mengine, ili kukabiliana na changamoto ya malazi kwa kuwa Simiyu imepewa heshima ya kuwa Mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane kwa miaka mitatu mfululizo.

Amesema pamoja na kuwa mwenyeji wa Maonesho Nanenane Kitaifa yapo matukio mengine yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ikiwa ni pamoja na Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 2018, Maadhimisho ya  Kimataifa ya siku ya watu wenye Ulemavu Desemba 2018, Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hapa nchini mwaka 2019 na mengine mengi yatafuata baada ya hapo hivyo maandalizi ni muhimu..

Amesema Serikali mkoani humo kupitia Halmashauri zake  imedhamiria kuwekeza katika ujenzi wa sehemu za malazi lakini inaendelea kuweka msukumo kwa wafanyabishara kuwekeza si tu katika ujenzi wa nyumba za kulala wageni na hoteli, bali katika ujenzi wa vituo vya mafuta, maeneo ya utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za chakula na huduma za kibenki.

Mmoja wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu Bw. Malongo Midimu amesema wako tayari kuwekeza  mkoani hapa na akaomba Serikali pamoja Taasisi za Kifedha zikiwemo Benki kuondoa vikwazo na urasimu pale wanapohitaji masuala hayo

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito kwa Wafanyabiashara kujipanga katika uwekezaji kwa kuwa Simiyu inabadilika na inaendelea kufunguka ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa Ujenzi wa miundombinu kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Igegu wilaya ya Bariadi, barabara ya Maswa-Bariadi kutachangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa.

Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018, Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kiliwahusisha Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Watumishi na Wadau mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu kikiwa na lengo la kushukuru na kutambua mchango wa wadau wote muhimu waliofanikisha maonesho hayo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara na Mjumbe wa NEC  Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu Bw. Gungu Silanga akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara wa Mjini Bariadi, Bw. Clement Mlanda akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo  akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.

Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya akizungumza katika kikao cha  Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi..

SIMIYU YAJIPANGA KUUFANYA MRADI WA UMWAGILIAJI MWASUBUYA KUWA WA MFANO, KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuutumia Mradi wa Uwagiliaji wa Mwasubuya kubadilisha maisha ya wananchi wilayani Bariadi, kupitia kilimo cha kisasa kinachotumia zana za kisasa na kuufanya kuwa mradi wa mfano ambao watu wateanda kujifunza.


Mtaka ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu na kuwashukuru viongozi wa Chama na Serikali, Watendaji, Watumishi, wafanyabiashara na wadau wengine waliofanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema mradi huo wenye ekari 514 zitakazolimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya Bwawa la Mwasubuya lililoigharimu Serikali shilingi bilioni 1.24, utahusisha kilimo cha kisasa chenye kutumia zana za kisasa katika hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, palizi na kuvuna badala ya kuhusisha zana za kilimo za mikono.

“ Nimewaambia watu wa Bariadi tunahitaji Kijiji kimoja ambacho tutabadilisha maisha ya wananchi na watu wataenda kujifunza na kuangalia transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lakini pia tunahitaji lile shamba lote la ekari 514 lilimwe pasipo kutumia mikono ya wanadamu kuanzia hatua za kuandaa shamba, kupanda, palizi hadi kuvuna” alisema

Ameongeza kuwa dhamira ya Mkoa ni kuona wananchi wanalima kisasa kwa kutumia zana bora za kilimo ambazo baada ya mazungumzo na Kampuni ya Agricom Africa  imekubali kuikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi zana zote muhimu ili kuwawezesha wakulima katika mradi wa Mwasubuya kuongeza tija katika uzalishaji.

Aidha, Mtaka amesema Bwawa la Mwasubuya lililopo katika Mradi huu wa Umwagiliaji wa  Mwasubuya wilayani Bariadi litawekewa vifaranga vya samaki vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.

"Huu ni mradi ambao tungehitaji watu wote ndani ya mkoa waende wakaangalie transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lile bwawa tutaliwekea vifaranga vya samaki vya zaidi ya shilingi milioni kumi na tutalifunga mpaka mwezi Agosti 2019, uongozi utakaokuja mwakani kwenye Nanenane moja ya eneo watakalotembelea ni bwawa la Mwasubuya na tutafanya shughuli ya uvuaji wa hao samaki" alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Watumishi na wananchi wa Bariadi watahamasishwa kwenda kutengeneza vizimba katika Bwawa hilo, lengo likiwa ni kutafsiri namna maji yanavyoweza kuinufaisha jamii kwa namna nyingine zaidi ya kilimo cha Umwagiliaji.

Kwa upande wake Mratibu wa Matawi ya Agricom Africa hapa nchini Bw. Zuberi Lujina amesema kampuni hiyo iko tayari kufanya kazi na mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wakulima wanaondokana na kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo chenye tija na kilimo biashara wakitumia zana bora za kilimo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi amesema wameshazungumza na Viongozi wa Kampuni ya Agricom Africa ambapo wameahidi kufikisha vifaa na zana hizo katika Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi katika juma la tarehe 20 hadi 27 mwezi huu.

MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.


Mratibu wa Matawi ya Kampuni ya Agricom Africa inayohusika na uuzaji wa zana bora za kisasa za kilimo, Bw. Zuberi Lujina akiztoa maelezo ya namna kampuni yake inavyofanya kazi,  katika Kikao cha Tathmini  ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.



Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.

RC MTAKA AKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOANI SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Taleck  na kumhakikishia Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Ndg. Charles Kabeho  kuwa atachukua hatua dhidi ya mapungufu yaliyobainika wakati Mwenge wa Uhuru ukipitia baadhi ya miradi ya maendeleo mkoani Simiyu.

Mtaka amesema ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Ndg. Charles Kabeho  yatafanyiwa kazi,ikiwa kuna mahali pa kuchukua hatua,  hatua stahiki zitachukuliwa na ikiwa kuna mahali pa kufanya maboresho ili miradi hiyo itekelezwe katika viwango vinavyokidhi haja ya kutoa huduma kwa wananchi, Serikali ya mkoa itahakikisha inasimamia.

“Ndugu Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 na wakimbiza Mwenge wenzako, tunawashukuru kwa kuwa sehemu ya jicho la tatu kwenye miradi inayotekelezwa ndani ya mkoa, niwahakikishie kwamba tutachukua stahiki pale ambapo palionesha ukakasi kwenye taarifa zetu na pale ambapo mliona kunahitajika hatua ili miradi iweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi tutachukua hatua” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Kabeho amewashukuru viongozi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano waliompa yeye na wakimbiza Mwenge wenzake walipokuwa Simiyu.

Aidha, Kabeho alitoa rai kwa watumishi wa Umma kuachana na kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake wafanye kazi kwa weledi na bidii, hususani katika usimamizi wa miradi ili iweze kutekelezwa kwa wakati katika viwango vya ubora unaotakiwa na wananchi wapate huduma kwa wakati.

Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa katika kijiji cha Wishiteleja katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo ukiwa mkoani Simiyu ulipitia miradi 36 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.4.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Taleck katika Kijiji cha Wishiteleja wilayani Kishapu mkoani Simiyu Agosti 20, 2018. 



Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!