Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuutumia Mradi wa Uwagiliaji wa Mwasubuya
kubadilisha maisha ya wananchi wilayani Bariadi, kupitia kilimo cha kisasa kinachotumia
zana za kisasa na kuufanya kuwa mradi wa mfano ambao watu wateanda kujifunza.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao cha tathmini
ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu na
kuwashukuru viongozi wa Chama na Serikali, Watendaji, Watumishi, wafanyabiashara
na wadau wengine waliofanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Amesema mradi huo wenye ekari 514 zitakazolimwa
kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya Bwawa la Mwasubuya lililoigharimu
Serikali shilingi bilioni 1.24, utahusisha kilimo cha kisasa chenye kutumia
zana za kisasa katika hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, palizi na
kuvuna badala ya kuhusisha zana za kilimo za mikono.
“ Nimewaambia watu wa Bariadi tunahitaji
Kijiji kimoja ambacho tutabadilisha maisha ya wananchi na watu wataenda
kujifunza na kuangalia transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lakini pia
tunahitaji lile shamba lote la ekari 514 lilimwe pasipo kutumia mikono ya
wanadamu kuanzia hatua za kuandaa shamba, kupanda, palizi hadi kuvuna” alisema
Ameongeza kuwa dhamira ya Mkoa ni kuona
wananchi wanalima kisasa kwa kutumia zana bora za kilimo ambazo baada ya mazungumzo
na Kampuni ya Agricom Africa imekubali
kuikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi zana zote muhimu ili kuwawezesha
wakulima katika mradi wa Mwasubuya kuongeza tija katika uzalishaji.
Aidha, Mtaka amesema Bwawa la Mwasubuya
lililopo katika Mradi huu wa Umwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi litawekewa
vifaranga vya samaki vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.
"Huu ni mradi ambao tungehitaji
watu wote ndani ya mkoa waende wakaangalie transformation(mabadiliko) ya kile
kijiji, lile bwawa tutaliwekea vifaranga vya samaki vya zaidi ya shilingi
milioni kumi na tutalifunga mpaka mwezi Agosti 2019, uongozi utakaokuja mwakani
kwenye Nanenane moja ya eneo watakalotembelea ni bwawa la Mwasubuya na
tutafanya shughuli ya uvuaji wa hao samaki" alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa Watumishi na wananchi wa
Bariadi watahamasishwa kwenda kutengeneza vizimba katika Bwawa hilo, lengo
likiwa ni kutafsiri namna maji yanavyoweza kuinufaisha jamii kwa namna nyingine
zaidi ya kilimo cha Umwagiliaji.
Kwa upande wake Mratibu wa Matawi ya
Agricom Africa hapa nchini Bw. Zuberi Lujina amesema kampuni hiyo iko tayari
kufanya kazi na mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wakulima wanaondokana na
kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo chenye tija na kilimo biashara wakitumia
zana bora za kilimo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi amesema wameshazungumza na
Viongozi wa Kampuni ya Agricom Africa ambapo wameahidi kufikisha vifaa na zana
hizo katika Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi katika juma la tarehe 20 hadi 27
mwezi huu.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu akizungumza katika Kikao cha Tathmini
Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi
na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine
walioshiriki katika kufanikisha maonesho
hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mratibu wa Matawi ya
Kampuni ya Agricom Africa inayohusika na uuzaji wa zana bora za kisasa za
kilimo, Bw. Zuberi Lujina akiztoa maelezo ya namna kampuni yake inavyofanya
kazi, katika Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya
ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara
na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika
Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali,
Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika
Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment