Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa
mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho amewahimiza wananchi wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu
kuwekeza katika miundombinu ya elimu ili kukabiliana na msongamano wa
wanafunzi unaotokana na utekelezaji wa Sera ya Elimu bila malipo.
Kabeho ametoa wito huo katika
kijiji cha Jija wakati akizindua mradi wa Maji na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari
Jija, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 19, 2018 .
Amesema kutokana na utekelezaji
wa sera ya Elimu bila malipo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa
darasa la awali, darasa la kwanza wanaojiunga na kidato cha kwanza, hivyo wananchi
wawekeze katika ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine ya elimu ili wanafunzi waweze
kusoma katika mazingira mazuri.
Katika hatua nyingine Kabeho amewataka Watumishi wa Umma
kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa kwa weledi na
ufanisi mkubwa wakiizingatia sheria, kanuni na taratibu.
“Mhe. Rais anaposema HAPA KAZI TU anamaanisha fanya kazi
kwa bidii, zingatia sheria, taratibu na
kanuni, wapo watumishi wanafanya kazi pale tu palipo na maslahi mahali ambapo
hapana maslahi hamwajibiki, achaneni na kufanya kazi kwa mazoea fanyeni kazi
kwa kujituma na kwa ufanisi” alisema
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki
akizungumza kwa niaba wa wananchi ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea
kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo
ameshukuru kwa kupelekea miradi hiyo ya maji na elimu katika Kijiji cha Jija
,huku akisisitiza wazazi kutowakatisha masomo watoto wao hususani wa kike
.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Maswa umepitia miradi yenye thamani ya milioni 516,
kutoka sekta ya Elimu, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii (Vikundi vya vijana na
wanawake)
Mbio za mwenge mkoani SIMIYU zimehitimishwa Agosti
19 baada ya kuanza kukimbizwa Agosti 14 ukitokea mkoani Singida na unatarajiwa
kukabidhiwa mkoani Shinyanga Agosti 2018.
MWISHO
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho akifungua vyumba
viwili vya madasa katika Shule ya Sekondari Jija wilayani Maswa, Agosti 19,
2018, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho akishuhudia jiwe la
Ufunguzi wa Madarasa mawili aliyofungua katika Shule ya Sekondari Jija wilayani
Maswa, Agosti 19, 2018 likisomwa, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake
wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho mara baada ya
kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(hayupo pichani),
Agosti 19, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho akimtwisha ndoo
mkazi wa Jija mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Jija wilayani Maswa
Agosti 19, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkimbiza
Mwenge Kitaifa Dominik Rweyemamu Njunwa, mara baada ya makabidhiano kati ya
Wilaya ya Busega na Maswa yaliyofanyika Kijiji cha Jija kukamilika, Agosti 19,
2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.
Tano Mwera wakitakiana heri mara baada ya kukamilika kwa makabidhiano ya mwenge
wa Uhuru baina yao, yaliyofanyika katik a Kijiji cha Jija Wilayani Maswa Agosti
19,2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kushoto) na Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho wakiteta jambo mara
baada ya madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Jija kufunguliwa na kiongozi
huyo Agosti 19, 2018, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani
humo
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko(kushoto) akisalimiana na Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho mara baada ya
kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(hayupo pichani)
kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, Agosti 19, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho akifuatilia nyaraka
mbalimbali zinazoonesha uthibitisho wa fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
zilizotolewa kama mkopo kwa vikundi vya Vijana na Wanawake, kabla ya kukagua
kazi za Vikundi hivyo, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani
humo Agosti 19, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho akizungumza na
viongozi wa Wilaya ya Maswa, kabla ya kuzindua Mradi wa Maji wa Kijiji cha Jija
wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo Agosti 19, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.
Tano Mwera wakitakiana heri mara baada ya kukamilika kwa makabidhiano ya mwenge
wa Uhuru baina yao, yaliyofanyika katik a Kijiji cha Jija Wilayani Maswa Agosti
19,2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho akizungumza na
viongozi wa Wilaya ya Maswa, wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita katika Mradi wa
Jengo la Bweni ukiwa katika mbio zake wilayani humo Agosti 19, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho akisalimiana na
Wajasiriamali kutoka katika Vikundi vya wakina mama na vijana, wakati alipopita
na kuona kazi zao, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo Agosti
19, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kulia), akikiri kupokea Mwenge wa
Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera katika makabidhaiano
yaliyofanyika katika Kijiji cha Jija wilayani Maswa, wakati
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo Agosti 19, 2018.
Vijana wa
Wilaya ya Maswa wakimvisha skafu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Kabeho mara baada ya
kuwasili wilayani humo akitokea wilayani Busega, tayari kwa kuanza mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 19, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif
Shekalaghe(kulia), Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuanza kuukimbiza katika Wilaya ya
Maswa, Agosti 19, 2018.
0 comments:
Post a Comment