Taasisi ya Uhifadhi na Utalii ya Friedkin Conservation
Fund, imetoa msaada ya shilingi millioni 110 ili kusaidia ujenzi wa shule ya
sekondari ya vipaji maalum katika Mkoa wa Simiyu.
Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na Wakurugenzi wa Taasisi hiyo wakiongozwa na
Abdukadir Mohamed katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane
Nyakabindi uliopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mohamed amesema Taasisi yao ambayo inamiliki
kampuni za Uwindaji na upigaji picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd
na Tanzania Game Trackers Safaris, ambazo zimewekeza mkoani humo, zimetoa
msaada huo kusaidia watoto kupata elimu, huku akibanisha kuwa huu ni mwendelezo
wa misaada ya kusaidia jamii inayotolewa ili kuchangia maendeleo ya mkoa
wa Simiyu.
"Tunachoomba ni kupewa ushirikiano tufanye kazi
zetu za utalii na uhifadhi ipasavyo
pasipo shida yoyote, tuko tayari kusaidia na kuchangia maendeleo katika
Mkoa wa Simiyu” alisema
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameshukuru wawekezaji hao kwa
msaada huo walioutoa ili kusaidia ujenzi wa shule maalum ya mkoa, ambapo
amesema pamoja na kujenga shule hiyo mkoa
huo una mpango wa kujenga shule nyingine tatu maalum.
Amesema awali mkoa ulipanga
kuifanya Shule ya Sekondari Simiyu kuwa shule ya ufundi kwa kuiongezea
miundombinu yote muhimu jambo ambalo lilishauriwa na Wizara ya Elimu litafutwe
eneo kubwa zaidi kwa kuwa lile llionekana kuwa dogo.
Ameongeza kuwa Mkoa umezingatia
ushauri wa Wizara na kutafuta eneo kubwa
lenye ukubwa wa ekari 50 lililopo
Sapiwi wilayani Bariadi na kubainisha
kuwa Wizara imeshatoa shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na
hivyo kuendelea kuifanya Simiyu Sekondari kubaki kuwa shule maalum ndani ya
mkoa.
Aidha, Mtaka amebainisha kuwa wadau
mbalimbali wamechangiai ujenzi wa shule hiyo maalum wakiwemo Shirika la Bima la
Taifa limetoa mifuo 400 ya saruji,
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mifuko 400, mifuko 400 kutoka Shirika la
Reli na mifuko 200 kutoka kwa Mtanzania mmoja aitwaye Reans na Mwiba Holdings
Limited ambaye amekabidhi hundi ya shilingi milioni 110.
“Watu mbalimbali wanaendelea
kuchangia ujenzi wa shule yetu saruji,
Shirika la Bima la Taifa limetoa mifuko 400, Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege mifuko 400, mifuko 400 kutoka Shirika la Reli na mifuko 200 kutoka kwa Mtanzania
mmoja aitwaye Reans, MWIBA Holdings
Limited nao sasa hivi wanatukabidhi pia hundi ya shilingi milioni 110”
“Kulikuwa na changamoto kwa
mwekezaji huyu lakini Kamati ya Ulinzi na Usalam ya Mkoa na kamati ya Siasa ya
Mkoa zilienda zikakutana na Viongozi wa Friedkin/ Mwiba Holdings Ltd na ufumbuzi
ukapatikana” alisisitiza.
Amesema wawekezaji hao wamekuwa na mchango mkubwa wa
maendeleo katika mkoa huo kwani hivi karibuni walitoa msaada wa mifuko
3000 ya saruji na bati 1000 kusaidia elimu.
Mchango mwingine ni kutoa ajira kwa wananchi na pia wamechangia
kuongeza mapato ya Mkoa kwa kuwa jalada la Malipo la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)
limehamishiwa Mkoani Simiyu kutoka mkoani Arusha lililokuwa awali.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt.
Joseph Chilongani amesema Serikali inatambua mchango wa Taasisi hiyo katika maendeleo ya jamii.
Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Esther Midimu amempongeza Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe Anthony
Mtaka pamoja na wasaidizi wake kwa jitihada wanazofanya kutafuta michango ya
wadau kufanikisha ujenzi wa shule hiyo na akaomba wasimamie vizuri michango
hiyo ili ifanye kazi iliyokusudiwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Itilima
Mhe. Benson Kilangi amesema yeye pamoja na wasaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka watafanya kila linalowezekana ili malengo
yalikusudiwa kufanyika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi yanafikiwa.
MWISHO
Mkurugenzi wa kampuni
za Uwindaji na upigaji picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania
Game Trackers Safaris Abdukadir Mohamed akikabidhi hundi ya shilingi milioni
110 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule maalum Simiyu, wengine ni viongozi
wa Mkoa wa Simiyu wakishuhudia makabidhiano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akitoa shukrani mara baada
ya makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 110 kati ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi wa kampuni za Uwindaji na upigaji
picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania Game Trackers
Safaris Abdukadir Mohamed kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule maalum Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,
Mhe. Benson Kilangi akizungumza mara
baada ya makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 110 kati ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi wa kampuni za Uwindaji na upigaji
picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania Game Trackers
Safaris Abdukadir Mohamed kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule maalum Simiyu.
Mkurugenzi wa kampuni
za Uwindaji na upigaji picha za Kitalii, Mwiba holdings Ltd na Tanzania
Game Trackers Safaris Abdukadir Mohamed akikabidhi hundi ya shilingi milioni
110 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule maalum Simiyu, wengine ni viongozi
wa Mkoa wa Simiyu wakishuhudia makabidhiano hayo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu(CCM) Esther Midimu akizungumza mara baada ya makabidhiano ya
hundi ya shilingi milioni 110 kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na Mkurugenzi wa kampuni za Uwindaji na upigaji picha za
Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Abdukadir
Mohamed kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule maalum Simiyu.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa, Mhe. Gungu Silanga akizungumza
mara baada ya makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 110 kati ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi wa kampuni za Uwindaji na
upigaji picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania Game
Trackers Safaris Abdukadir Mohamed kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule
maalum Simiyu.
0 comments:
Post a Comment