Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) limewahakikishia viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa litaanza
kujenga majengo ya kudumu katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Bariadi mkoani
humo, mwishoni mwa mwaka 2018.
Haya
yamesemwa na Mwakilishi wa Mkuu wa JKT,
Meja Jenerali Martin Busungu, Luteni Kanali
Respicious Kaiza wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na
viongozi wa Wilaya ya Bariadi wakiagana na baadhi ya viongozi na Maafisa
wa JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi mara baada ya kukamilisha siku tatu
za nyongeza za maonesho ya nanenane zilizotolewa na Waziri wa Kilimo,
Dkt. Charles Tizeba, wakati akifungua maonesho hayo Kitaifa mwaka 2018, mkoani
Simiyu.
Luteni Kanali
Kaiza amesema viongozi wa JKT wameondoka Nyakabindi Uwanja wa Nanenane kwa
lengo la kwenda kujipanga ili waondokane na majengo ya kuhamisha na kuanza
ujenzi wa majengo ya kudumu katika uwanjauwanja huo katika maonesho
yajayo.
"Tutaka
kwenda kujipanga baada ya muda kidogo tutarudi kuanza rasmi ujenzi wa majengo
ya kudumu ili tusiwe na majengo haya ambayo ni ya kuhamisha, Mungu akijalia
mwishoni mwa mwaka huu tunataka tuwe tumeshaanza kujenga"'alisema.
Aidha, Luteni
Kanali Kaiza amesema pamoja na viongozi na Maafisa wa JKT kuondoka Uwanjani
hapo, vijana wa JKT pamoja na viongozi wa JKT waliokuwepo katika Kambi ya
Nyakabindi wakati wa Maonesho ya Nanenane watabaki katika Eneo hilo la
Nyakabindi kuendeleza shughuli walizozianzisha katika Uwanja huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya Mkoa huo ni kuwa
na Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa hivyo amewaomba viongozi wa JKT
kuona uwezekano wa kujenga majengo makubwa zaidi ya yaliyotumika mwaka huu kwa
kuwa mwaka 2019 watu zaidi ya 100,000 wanatarajiwa kushiriki maonesho ya
nanenane na akawaomba pia waone uwezekano wa kuanza kujenga majengo hayo mapema
kuanzia mwezi Oktoba, 2018.
Mtaka ametoa
wito kwa JKT pia kujenga hoteli, hosteli, kumbi za mikutano na miundombinu
mingine muhimu katika eneo la Nykabindi kwa kuwa eneo hilo litatumika kwa
maonesho ya nanenane, maonesho ya kilimo biashara kila baada ya miezi mitatu na
Vyuo vingi vya Elimu ya Juu vitajengwa karibu na eneo hilo, hivyo majengo hayo
yakijengwa yatasaidia na kurahisisha kutoa huduma katika eneo hilo.
Aidha,
amesema Serikali imeandaa utaratibu wa kuliendeleza eneo la Uwanja wa
Nyakabindi ambapo itatoa nafasi kwa vijana, watumishi wa Umma walio tayari
kufanya shughuli zao katika kilimo na mifugo kwa usimamizi wa Wataalam wa Kilimo
na mifugo ili liweze kutumika kwa manufaa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ameshauri kwa kuwa JKT liwekeze
katika ujenzi wa hoteli na hosteli
katika eneo la Nyakabindi kwa kuwa ina
nguvu kazi ili watu wanapokuja kwenye
maonesho wapate huduma ya malazi kwa urahisi ndani ya mkoa badala ya kutoka nje,
lakini pia JKT waweze kufanya biashara kupitia uwekezaji huo.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melckizedeck Humbe
amesema uwepo wa JKT utachangia mji huo kukua kwa kasi, huku akibanisha kuwa
Halmashauri inatarajia kupima viwanja katika eneo la Nyakabindi lengo ni
kufanya JKT na wawekezaji mbalimbali kujenga miundombinu yote muhimu karibu na
Uwanja wa Nanenane ikiwemo vituo vya mafuta, hoteli, kumbi na hosteli.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkuu wa
Jesho la Kujenga Taifa( JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, Luteni Kanali
P.M.Kaiza katika kikao kifupi kabla ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Simiyu,Viongozi wa Wilaya ya Bariadi na baadhi ya Viongozi na Maafisa wa JKT
waliokuwepo Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuagana hapo
jana, baada ya kukamilisha siku tatu za nyongeza ya maonesho ya nanenane
zilizomalizika Agosti 11.
Katibu Tawala wa
mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga katika kikao
kifupi kabla ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa
Wilaya ya Bariadi na baadhi ya viongozi na Maafisa wa JKT waliokuwepo Uwanja wa
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuagana hapo jana, baada ya
kukamilisha siku tatu za nyongeza ya maonesho ya nanenane zilizomalizika Agosti
11.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melckizedeck Humbe akizungumza na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa Wilaya ya Bariadi, baadhi ya
viongozi na Maafisa wa JKT waliokuwepo Uwanja wa NnaneNyakabindi Halmashauri ya
Mji wa Bariadi kuagana hapo jana, baada
ya kukamilisha siku tatu za nyongeza ya maonesho ya nanenane zilizomalizika
Agosti 11.
Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi Wilbert Siogopi akizungumza na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa Wilaya ya Bariadi,
baadhi ya viongozi na Maafisa wa JKT waliokuwepo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuagana
hapo jana, baada ya kukamilisha siku tatu za nyongeza ya maonesho ya
nanenane zilizomalizika Agosti 11.
Mwakilishi wa
Mkuu wa Jesho la Kujenga Taifa( JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, Luteni Kanali
P.M.Kaiza( wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Simiyu,Viongozi wa Wilaya ya Bariadi katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi baada ya kikao kifupi na kuagana hapo jana, baada ya kukamilisha siku
tatu za nyongeza ya maonesho ya nanenane zilizomalizika Agosti 11.
Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Mwanamizi wa Polisi Deusdedit Nsimeki akizungumza katika kikao kifupi kati ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu,
Viongozi wa Wilaya ya Bariadi, baadhi ya viongozi na Maafisa wa JKT waliokuwepo
Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi kabla ya kuagana hapo jana, baada ya kukamilisha siku tatu za
nyongeza ya maonesho ya nanenane zilizomalizika Agosti 11.
0 comments:
Post a Comment