Zaidi ya wananchi 2000 wa
Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wamenufaika na mradi wa
maji safi na salama na kuondokana na
adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji kwa kusogezewa huduma ya maji karibu
na makazi yao.
Hayo yamesemwa
na Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Goodluck
Masige wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, aliyefika katika mradi wa maji wa Lagangabilili
wenye thamani ya shilingi milioni 967, kwa ajili ya kufungua.
Masige amesema Mradi wa Maji
wa Lagangabilili ulianza kutekelezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2018 na
kuanza kutumika huku akibainisha uwezo
wake kuwa, una kisima chenye uwezo wa kutoa maji lita 15,000/= kwa saa, vituo
vya kuchotea maji 23 na mtandao wa maji wenye urefu wa mita 29,431.
“Kukamilika kwa mradi huu wakazi
2228 wanapata huduma ya maji safi na
salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengineyo,mradi umepunguza muda
waliokuwa wanaoutumia wananchi kutafuta maji kwa kuwasogezea huduma ya maji
karibu na makazi kwa saa 24,mpaka sasa kaya 25 na taasisi za Umma 20
zimeunganishiwa maji” alisema Masige .
Awali Mkuu wa Wilaya ya
Itilima Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa tangu
Uhuru eneo hilo lilikuwa halina maji kabisa, na baada ya kupatikana kwa huduma
hiyo kutapunguza adha ya uhaba wa maji, huku akibainisha kuwa Serikali inategemea
mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kuwa
suluhisho la kudumu la changamoto ya maji ka ajili ya matumizi ya binadamu na
wanyama pia.
Perusi Makeleja mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili amesema kukamilika kwa mradi huo kumewapunguzia adha wananchi hususani wanawake ya kusafiri umbali mrefu na kuamka alfajiri kufuata maji lakini umesaidia kupunguza magonjwa.
“Kabla ya
mradi huu tulikuwa tunaamka usiku usiku kwenda kutafuta maji mbali tunapishana
na fisi njiani, watoto wetu walikuwa wakiugua magonjwa ya tumbo na kuhara kutokana
na kunywa maji ambayo hayakuwa salama, , lakini kwa sasa hizo shida hamna tena,
tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu sisi Wanalagangabilili”
alisema
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho
ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamoto za wananchi wake,
ambapo katika ujenzi wa mradi huo Serikali ya Tanzania imechangia kiasi cha
shilingi milioni 907 huku serikali ya Misri ikichangia kiasi cha shilingi
milioni 60 ili kukamilisha ujenzi huo.
Mwenge wa Uhuru
ukiwa wilayani Itilima umefungua vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari ya Budalabujiga, vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi
Lagangabilili pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maboresho ya
kituo cha afya Ikindilo unaojumuisha jengo la wodi ya wazazi, jengo la
upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga na kukagua Shamba
darasa la Ufugaji wa Nyuki na Utunzaji wa Mazingira.
Aidha, kiongozi huyo ariridhishwa na ubora wa majengo
ya miradi hiyo, huku akiwapongeza viongozi wa wilaya na Halmasharui kwa
usimamizi makini ambapo aliwataka kuhakikisha majengo hayo yanakamilika ujenzi
wake na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine akiwa Wilayani Itilima Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Simiyu
kuendelea kuchangia chakula cha mchana shuleni ili watoto wapate
Muda wakujisomea zaidi hali itakayosaidia kupunguza utoro.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na Mbio zake Mkoani Simiyu
ambapo Agosti 15 Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Wilaya yaItilima umepita katika
miradi yenye thamani ya bilioni 1.6
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi(kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani katika kijiji cha Gamabasingu ili
Mwenge wa Uhuru uanze mbio zake wilayani Itilima, leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akitundika
mzinga wa Nyuki wa kisasa katika Shamba darasa la Ufugaji wa Nyuki na Utunzaji
wa Mazingira katikaKijiji cha Lagangabilili mara baada ya kukagua shamba darasa
hilo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua bomba
la maji kujiridhisha ikiwa linatoa maji kabla ya kuzindua mradi wa maji wa
Lagangabilili wilayani Itilima wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,
Agosti 15, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (wa
pili kulia) akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara ya Somo la Bailojia katika
Shule ya Sekondari Budalabujiga kabla ya kufungua vyumba vitatu vya maabara vya
shule hiyo wilayani Itilima, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,
Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (kushoto)
akizungumza na baadhi ya viongozi na wananchi wa Wilaya ya Itilima mara baada
ya kukagua Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Itilima, Dkt. Anold Musiba(kulia) akimuongoza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho kukagua Maboresho ya
Kituo cha Afya Ikindilo kabla hajaweka Jiwe la msingi, wakati wa mbio za Mwenge
wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi(kulia) akimuonesha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho tawimu za mradi wa Ujenzi
wa Vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari Budalabujiga,kabla ya kiongozi
huyo kufungua Vyumba hivyo, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,
Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua mradi
wa Maji wa Lagangabilili wilayani Itilima utakaowahudumia zaidi ya wananchi
2000, katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe
kabla ya kufungua mradi wa Maji wa
Lagangabilili wilayani Itilima utakaowahudumia zaidi ya wananchi 2000, katika
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (katikati)
akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara ya Somo la Bailojia katika Shule ya
Sekondari Budalabujiga kabla ya kufungua vyumba vitatu vya maabara vya shule
hiyo wilayani Itilima, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti
15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo
ya maji Bi. Mbuke Malogo mkazi wa Kijiji ch Lagangabilili wilayani Itilima mara
baada ya kufungua mradi wa maji utakaowahudumia zaidi ya wananchi 2000, katika
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akizungumza na
baadhi ya viongozi na wananchi wa Wilaya ya Itilima, kabla ya kufungua Vyumba
vitatu vya maabara katika Shule ya Sekondari ya Budalabujiga, wakati wa mbio za
Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho na Mkuu wa
wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na
Mwenge wa Uhuru, baada ya kuweka jiwe la msingi Maboresho ya Kituo cha Afya
Ikindilo, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Mkuu wa wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi(aliyenyoosha mkono wa kulia juu) akionesha maeneo
ya Kituo cha Afya Ikindilo, baada ya kuwekwa kwa jiwe la msingi Maboresho ya
Kituo cha Afya Ikindilo, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,
Agosti 15, 2018.
Mkuu wa wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho mara baada ya kumpokea
kutoka Wilya ya Meatu, wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Wilaya
ya meatu na Wilaya ya Itilima katika Kijiji cha Gambasingu, wilayani Itilima,
Agosti 15, 2018.
wa Skauti wa Wilaya ya
Itilima wakimvisha Skafu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2018, Ndg. Charles Francis Kabeho kabla ya makabidhano ya Mwenge wa Uhuru kati
ya Wilaya ya Meatu na Wilaya ya Itilima, katika Kijiji cha Gambasingu wilayani
Itilima Agosti 15, 2018.
Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Lagangabilili, Anna Mathew akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada
ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis
Kabeho kufungua Vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa kupitia mradi wa P4R
shuleni hapo, wakati wa mbio za Mwenge
wa Uhuru wilayani Itilima Agosti 15, 2018.
Diwani
wa Kata Kata ya Ikindilo akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, kuweka
jiwe la msingi Maboresho ya Kituo cha Afya Ikindilo, wakati wa mbio za Mwenge
wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akizungumza na
Mratibu wa Mwenge Mkoa wa Simiyu, Bw. Maganga Simon(katikati) na Mkuu wa Wilaya
ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi, kabla ya kufungua Vyumba vitatu vya maabara
katika Shule ya Sekondari ya Budalabujiga, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru
wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mabula akisalimiana na akisalimiana na
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis
Kabeho mara baada ya kumpokea kutoka Wilaya ya Meatu, wakati wa makabidhiano ya
Mwenge wa Uhuru kati ya Wilaya ya Meatu na Wilaya ya Itilima katika Kijiji cha
Gambasingu, wilayani Itilima, Agosti 15, 2018.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mabula ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis
Kabeho, kuweka jiwe la msingi Maboresho ya Kituo cha Afya Ikindilo, wakati wa
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
0 comments:
Post a Comment