Wednesday, August 8, 2018

BENKI YA NBC YAAHIDI KUFUNGUA TAWI MJINI BARIADI SIMIYU


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Taifa ya Biashara(NBC) ,Theobald Sabi amewahakikishia wakazi wa Bariadi Mkoani Simiyu kuwa Benki hiyo itafungua tawi Mjini Bariadi ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Sabi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Wakala Mkubwa (Super Agent) Mjini Bariadi, Agosti 07, 2018.

Amasema Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu ina wateja wengi wa NBC lakini huduma zilikuwa mbali hivyo, kufunguliwa kwa wakala mkubwa (SUPER AGENT) ni sehemu ya mpango wa kupeleka karibu huduma kwa wateja wao.

“Hapa Bariadi tuna wateja wengi lakini huduma zilikuwa zinapatikana mbali, hivyo kufunguliwa kwa wakala huu ni kutawasaidia wateja wetu kupata huduma karibu na tutaendelea kuongea na wananchi ili tuweze kupata tawi la NBC,  ni nia yetu hivi karibuni kuongeza tawi hapa Bariadi” alisema .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kufunguliwa kwa Wakala Mkubwa wa NBC  Bariadi kumekuja katika wakati muafaka ambapo utaweza kupima mzunguko wa fedha mjini Bariadi na kuwa njia ya kwenda kwenye kufungua Tawi kamili la NBC. 

Amesema Mkoa wa Simiyu ni mkoa mpya unaojengwa kiuchumi hivyo ikiwa benki hiyo ikijipanga vizuri Wakala huo uliofunguliwa utafanya biashara kwa kuwa wakazi wa mkoa wa Simiyu ni wafayabiashara wazuri wa mazao mbalimbali pamoja na mifugo.

“Mkoa wa Simiyu ni mkoa wenye Uchumi mzuri tunao uwezo wa kuzungusha zaidi ya Bilioni 100 wakati wa mavuno ya pamba, benki ikijipanga vizuri na ikapata msimamizi mzuri wa wakala anayefahamu biashara ya benki mtafanya biashara, Wanyantuzu ni wafanyabiashara hakuna Mnyantuzu mcheza pulu” alisema

Naye Mfanyabiashara wa Mjini Bariadi, Bw. John Sabo ameshukuru uanzishwaji wa  Wakala huo  ambao utawapunguzia adha ya kufuata huduma mikoa ya Mwanza na Shinyanga  na kuabainisha kuwa  Wakala tu hautoshi, hivyo wafanyabiashara wengi wenye akaunti NBC wanaomba Benki ya NBC kufungua Tawi kamili Mkoani Simiyu.
MWISHO.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony  Mtaka  (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) Bariadi  Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony  Mtaka  (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Benki ya Taifa ya Baishara (NBC) pamoja na viongozi wa Chama na Serikali wakishangilia mara baada ya Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) kufunguliwa  Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza na wananchi kabla  ya Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) kufunguliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Siiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi.
 Mfanyabiashara wa Bariadi Mjini Bw.  John Sabo (wa pili kulia) akizungumza jambo juu ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka(kulia) wakati wa Ufunguzi wa Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) kufunguliwa  Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi wakiteta jambo mara baada ya kufungua Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) kufunguliwa  Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa  pili kushoto) na viongozi wengine wakipokea maelezo juu ya namna Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) uliofunguliwa  Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi, utakavyofanya kazi.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Esther Midimu akizungumza na wananchi  kabla  ya Wakala Mkubwa (Super Agent) wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) kufunguliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Siiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 07, 2018 Mjini Bariadi. 0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!