Tuesday, August 7, 2018

RAIS MSTAAFU MKAPA MGENI RASMI KILELE CHA NANENANE KITAIFA 2018 SIMIYU


RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha  Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amesema  Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo  viongozi mbalimbali wa Chama na  Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.

“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na  Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”

“Wageni wengine ni Wakurugenzi wa Benki ya NBC na NMB pamoja Viongozi waandamizi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, hivyo napenda kuwakaribisha wananchi wote wa Mikoa ya Mara, Shinyanga na kwa msisitizo wananchi wa Simiyu ambao ndiyo mkoa mwenyeji kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho ya maonesho haya ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani kwetu” alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka amewahakikishia wananchi kuwa usafiri wa kufika katika Uwanja wa Nanenane utakuwa wa uhakika kwa kuwa mabasi ya kwenda huko yapo ya kutosha na nauli zimepunguzwa  kutoka Lamadi mpaka Nyakabindi na kutoka Mjini Bariadi kwenda Nyakabindi.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu , Bw. Jumanne Sagini(kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(kushoto) akisalimiana na Wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelezo ya awali kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (kulia) wakiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!