Wakala
wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) unatarajia kusajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi 60,000 wa shule za Msingi za Sekondari wilayani Bariadi
mkoani Simiyu, kupitia Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto
wa miaka 06 hadi 18.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw. Charles Salyeem wakati wa
ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Salyeem
amesema mpango huo utahusisha usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi
wenye umri wa kuanzia miaka 06 hadi 18 kwa ushirikiano kati ya RITA na Ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia Idara za Elimu ambapo wanafunzi watasajiliwa
na kupata vyeti vya kuzaliwa katika shule zao.
Ameongeza
kuwa watoto wa umri wa miaka 06 hadi 18 ambao si wanafunzi watapata fursa ya
kusajiliwa katika Ofisi za Watendaji wa Kata, huku akibainisha kuwa watapaswa
kuwa na viambatisho vya msingi vinavyotakiwa kwa maelekezo watakayopewa na
Watendaji wa Kata kwenye maeneo yao.
Aidha,
Salyeem amesema wazazi na walezi wa watoto wenye umri huo watahitajika kuchangia
gharama kwa ajili ya usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao ili fedha zitakazopatikana ziwezeshe kupeleka mpango huu katika maeneo
mengine.
Awali
akifungua mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata kuhusu mpango huo kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
amewatakaWaratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuzingatia maelekezo
watakayopewa na kufanya kazi kwa uadilifu wakitanguliza uzalendo na siyo
maslahi binafsi.
Aidha,Kiswaga
amesema cheti cha kuzaliwa ni moja ya nyaraka muhimu kwa wanafunzi wanaotoka
hatua moja ya masomo kuingia nyingine hivyo akawataka viongozi na watendaji
kujipanga ili kuvuka lengo la RITA la kusajili wanafunzi 60,000 kwa kuhakikisha
kila fomu inayochukuliwa kwa ajili ya kuomba usajili inarudishwa na cheti cha
kuzaliwa kinachukuliwa.
“RITA
imejiwekea lengo la kusajili wanafunzi 60,000 kati ya zaidi ya 156,769 waliopo
wilayani Bariadi, wanafunzi wasio na vyeti ni wengi, hivyo basi tujipange
tuweze kuvuka lengo, tutumie viongozi kuhamasisha wazazi na kuhakikisha zoezi
hili linafanikiwa” alisema.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Ihusi, Kasimili Ngusa amesema mpango huu utawarahisishia wanafunzi
wengi wa umri wa miaka 06 hadi 18 kwa kupata vyeti vya kuzaliwa shuleni walipo,
tofauti na ilivyokuwa awali ambapo iliwalazimu wazazi na walezi kufuata huduma
ya usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Naye Mratibu
wa Elimu Kata ya Isanga, Sophia Kitobelo ametoa wito kwa wazazi na walezi kutumia
fursa hiyo ya kusajili na kuchukua vyeti vya kuzaliwa shuleni na katika Ofisi
za kata, kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata vyeti vya kuzaliwa ambavyo ni
miongoni mwa nyaraka muhimu kwa Watanzania.
Mkakati
huu wa Usajili wa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wenye umri wa miaka
06 hadi 18 umefunguliwa rasmi katika Wilaya ya Bariadi na baadaye utaendelea
katika wilaya nyingine za Mkoa wa Simiyu; hadi sasa umeanza kutekelezwa katika
wilaya kumi na moja za Mikoa miwili ya Dar es Salaam, Mara na Njombe.
MWISHO
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw. Charles Salyeem akitoa taarifa katika Ufunguzi wa
Mafunzo ya Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na
Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa
Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na
Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Donatus Weginah wakiteta jambo wakati ufunguzi wa mafunzo kwa
Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu
Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu
Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi
na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu
Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu
Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi
na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa
Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi waWilaya ya Bariadi wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu
Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu
Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi
na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa Watendaji Kata wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, baada ya ufunguzi
wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Meneja
Usajili RITA , Bi. Patricia Mpuya akiwasilisha mada katika mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa
Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili
na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari
wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi waWilaya ya Bariadi wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu
Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu
Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi
na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment