Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka ameongoza
Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo
Wilayani Meatu ambapo jumla shilingi milioni 84,876,950/= zimepatikana, fedha
taslimu ikiwa shilingi 18,776,000/= ahadi 66,100,000/= pamoja na mifuko 253 ya
saruji, mbuzi 12 na ng’ombe 3.
Akizungumza na wananchi na viongozi wa Chama na
Serikali Mtaka amewapongeza viongozi wa kata ya Mwanjolo kwa jitihada
walizofanya kwa kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha wanafunzi wa kike
wanapata bweni, huku akiwasisitiza wananchi kuona umuhimu wa kuwekeza katika
elimu ili kuuweka mkoa huo kwenye ushindani na mikoa mingine.
Aidha, ametoa wito kwa Madiwani wa kata zote mkoani
humo kuiga mfano wa Kata ya Mwanjolo ambapo amesema viongozi na wananchi
wanapaswa kuona uchungu na kuona haja ya kuwa na mabweni kwa watoto wa kike ili
waondakane na vishawishi na changamoto nyingine zinazowakabili ili waweze
kufikia malengo yao.
“Madiwani wetu hili jambo waige, haiwezekani hawa
wasichana wadogo wanaenda kupanga kwenye vijiji pateni uchungu watoto wa kike
wajengewe hosteli, Mungu ametupa ardhi, mifugo, nguvu za kufanya kazi,
tukishikamana kama watu wa Mwanjolo, watoto wetu wa kike wote watapata mabweni”
“Mwanjolo wametuamasha, niwaombe waheshimiwa
madiwani na viongozi wenzangu kwenye wilaya zote za Mkoa wa Simiyu moto huu
uliowashwa hapa Mwanjolo uende kwenye kata zote, tuanze kujenga mabweni ya
watoto wa kike wanapofaulu kwenda kidato cha kwanza wakae shule wasitembee
njiani wakaanza kupewa lift za baiskeli na bodaboda” alisema Mtaka
Ameongeza kuwa kwa sababu elimu ni kipaumbe cha
kwanza cha mkoa ni vema viongozi wote mkoani humo wakaweka dhamira kuwa kufikia
mwaka 2020 wanafunzi wa kike wote wanaosoma shule za sekondari mkoani Simiyu
wakae bweni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mhe. Luhaga Mpina ametoa wito kwa Wananchi
hususani jamii ya wafugaji kuchangia na kuunga mkono jitihada mbalimbali za
maendeleo ya elimu ili watoto wa jamii za kifugaji waweze kusoma katika
mazingira mazuri.
Wakati huo huo amewahimiza vijana wanaotoka katika
jamii za kifugaji kusoma kwa bidii ili waweze kuzisaidia jamii zao kufuga
ufugaji wenye tija utakaowaletea manufaa.
Nao wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Mwanjolo
wamewashukuru viongozi na wananchi ambao wamechangia ujenzi wa bweni, ambapo
wamesema endapo bweni hilo litakamilika litawasaidia kuondokana na vishawishi
mbalimbali vilivyokuwa vikisababisha baadhi yao kupata ujauzito na kushindwa
kumaliza masomo yao.
“Kukamilika kwa bweni kutatusaidia kutatua
changamoto tunazokutana nazo sisi wasichana hasa suala la mimba, kuna wenzangu
nilioanza nao kidato cha kwanza mwaka 2016 hawapo shuleni sasa hivi sababu ya
mimba, naamini tukikaa bweni tutakuwa salama
na tutapata muda mwingi wa kujisomea kwa kuwa hatutatembea mwendo mrefu
tena” Eunice Kapombe mwanafunzi Kidato
cha Tatu.
Kwa upande wao wazazi na walezi wa baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwanjolo wamesema ujenzi wa bweni la wasichana
katika Shule ya Sekondari Mwanjolo utakuwa msaada mkubwa kwa watoto wa kike
katika kuwawezesha kufikia kwenye malengo yao,kwa kuwa baadhi yao wamekuwa
wakikatisha masomo kutokana na mimba zinazosababishwa na vishwawishi
wanavyopata kwa kutembea mwendo mrefu kwenda shule na baadhi yao kupanga
vijijini.
Harambee ya ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya
Sekondari Mwanjolo iliyofanyika Shuleni hapo Agosti 31, 2018, imehusisha viongozi wa Chama na Serikali ngazi
ya Mkoa na Wilaya ya Meatu, Wadau mbalimbali wa Maendeleo na wananchi, ambapo
mpaka kukamilika kwa Bweni hilo jumla ya shilingi 125,024,504.35 zitahitajika.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akichangia katika Harambee ya Ujenzi wa
Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo
ilifanyika Agosti 31, 2018 shuleni hapo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu, Mhe.
Luhaga Mpina akichangia katika Harambee ya
Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu
, ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018 shuleni hapo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa akipokea michango kutoka
kwa Madiwani na baadhi ya watendaji wa Halmashauri hiyo katika Harambee ya
Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu
, ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018 shuleni hapo.
Baadhi
ya Wananchi wa Kata ya Mwanjolo wakichangia fedha katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule
ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018
shuleni hapo.
Baadhi
ya Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Mwanjolo wakiwa katika picha ya pamoja
na viongozi walioshiriki katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule
ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018
shuleni hapo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wakiwa katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule
ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018
shuleni hapo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani wakati wakiwa katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule
ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018
shuleni hapo.
Mkuu
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaelezea
viongozi wa kata ya Mwanjolo mbele ya wananchi na namna walivyofanikisha Harambee
ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani
Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018 shuleni hapo, (kushoto) Afisa Mtendaji
wa Kata ya Mwanjolo, Bw.Abel Mpina,(wa pili kulia) Diwani wa Viti Maalum Kata
ya Mwanjolo, Mhe. Consolata Lushu na kulia ni Diwani wa Kata ya Mwanjolo, Mhe.
Jeremiah Jilya.
Baadhi
ya Wananchi wa Kata ya Mwanjolo wakichangia fedha katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule
ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika Agosti 31, 2018
shuleni hapo.
Diwani
wa Viti Maalum Kata ya Mwanjolo, Mhe. Consolata Lushu (kulia) akimshukuru Mkuu
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuchangia shilingi milioni
tano kwenye Harambee ya Ujenzi wa Bweni
la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika
Agosti 31, 2018 shuleni hapo
Mkuu
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimshukuru Mzee maarufu kutoka Katika
Kijiji cha Jinamo kwa kutoa mchango wake wa ng’ombe mmoja na fedha taslimu shilingi
100,000/= katika Harambee ya Ujenzi wa Bweni
la Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwanjolo wilayani Meatu , ambayo ilifanyika
Agosti 31, 2018 shuleni hapo.
0 comments:
Post a Comment