Wananchi
wa Vijiji vya Igegu na Ng’arita Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi wameridhia
kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani
Simiyu ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Igegu wilayani Bariadi.
Wananchi
hao wameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uthamini
na upimaji wa maeneo hayo, ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya mwezi mmoja
na wiki mbili kuanzia sasa.
Wamesema
kuwa wamefurahishwa na hatua ya Serikali kujenga Kiwanja cha Ndege wilayani
Bariadi na kwa kuwa ujenzi huo ni suala la maendeleo hawawezi kupinga, huku
wakiiomba Serikali kuhakikisha wanalipa fedha za fidia kwa wakati mara tu baada
ya kukamilisha zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo hayo.
“Kwa
kuwa ujenzi wa kiwanja cha ndege ni maendeleo hatuwezi kukataa kutoa maeneo
yetu, tumekubali kutoa maeneo ila ombi letu kwa Serikali tunaomba tulipwe fidia
ya maeneo yetu kwa wakati na tulipwe kwa haki” alisema Ndaturu Malemi mkazi wa
Kijiji cha Igegu.
“Tumekubali
kutoa maeneo yetu Uwanja wa Ndege ujengwe, ushauri wangu tu ni kwamba kwa kuwa
tunaelekea msimu wa kuandaa mashamba baada ya tathmini tunaomba tuliokuwa na
maeneo hapa tuambiwe mapema kama ujenzi utaanza au tunaweza kuendelea na shughuli za
kilimo”alisema Mahembe Mayumba mkazi wa Kijiji cha Igegu
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewataka Wataalam wa
Ardhi watakaohusika na zoezi la uthamini na upimaji wa eneo litakojengwa Kiwanja hicho
cha Ndege kufanya zoezi hilo kwa kufuata haki na sheria za nchi.
“Nimewaagiza
wataalam watakaohusika kufanya zoezi la tathmini na kulipa fidia kwa kumuogopa
Mungu, watende haki, kila ambacho mwananchi anapaswa kufidiwa wahakikishe
kinafidiwa kwa mujibu wa sheria; tumekubaliana wataalam watavaa vitambulisho
ili watambuliwe na ikitokea mtu akihujumu zoezi hili iwe rahisi kumfahamu na
kuchukua hatua” alisema Kiswaga.
Akizungumzia
suala la taarifa ya uthamini kutolewa
mapema kwa wananchi, Kiswaga amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa
mwezi mmoja na wiki mbili na baada ya hapo wenye maeneo watapewa taarifa.
Meneja
wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Easter Dotto
Madale amesema Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa utawasaidia
wananchi kupata usafiri wa anga ambao ni wa haraka, uhakika na salama, huku
akisisitiza kuwa kiwanja hicho kitakapoanza kujengwa wananchi hususani vijana
watapata ajira kwenye kazi za ujenzi na wanawake watajiajiri katika kazi za
kupika na kuuza vyakula
Naye
Afisa Ardhi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Bi. Cecilia Mwing’uri amesema Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini
(TAA) imeshatoa fedha kwa ajili ya tathmini, uthamini na upimaji wa maeneo
Kiwanja kitakapojengwa na mara baada ya zoezi hilo kukamilika wananchi
wanaohusika watalipwa fidia.
Bi.Cecilia amewahakikishia
wananchi wa Vijiji vya Igegu na Ng’arita kuwa watalipwa fedha zao zote mara
baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki , kwa kuwa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini (TAA)
imetenga fedha hizo kwa ajili ya fidia ya Kiwanja cha Ndege cha Simiyu.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanja
cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto
Madale Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu kitakapokamilika
kitakuwa ni miongoni mwa Viwanja vikubwa hapa nchini ambavyo vina uwezo wa kupokea ndege kubwa.
MWISHO
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ng’arita katika Kata ya Sapiwi Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa huo, wakati wa Mkutano wa kufungua Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ng’arita Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani humo, katika Uzinduzi wa zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Simiyu kitakapojengwa.
Baadhi ya wananchi wa
Kijiji cha Igegu katika Kata ya Sapiwi
Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo
Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa
Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa
huo, wakati wa Mkutano wa kuzindua
Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018.
Afisa Ardhi Mkuu kutoka
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Cecilia
Mwing’uri akifafanua jambo katika
Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo laUjenzi wa Kiwanja
cha Ndege cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita
wilayani Bariadi Septemba 14, 2018.
Meneja wa Kiwanja cha
Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale
akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa
eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu,
uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14,
2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Igegu Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani
humo, kuhusu uzinduzi wa Zoezi la uthamini
na upimaji wa maeneo ambayo Uwanja wa
Ndege wa mkoa wa Simiyu utakapojengwa.
Kutoka kushoto Afisa
Ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Bi. Cecilia Mwing’uri , Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster
Dotto Madale na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga, wakiteta jambo, katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini
na upimaji wa eneo laUjenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Simiyu,
uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14,
2018.
Baadhi ya wananchi wa
Kijiji cha Ng’arita wakimsiiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo laUjenzi wa
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji
vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018.
Diwani
wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, Mhe. Jamsi Gamaliel Kibunga akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Igegu, katika Uzinduzi wa zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Simiyu kitakapojengwa
0 comments:
Post a Comment