Serikali imetenga kiasi cha
shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali tatu za Halmashauri
za Wilaya ya Busega ,Bariadi na Itilima Mkoani Simiyu katika bajeti
2018/2019, ili kuendelea kuboresha
utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala
wa Mkoa wa SIMIYU Bw. JUMANNE SAGINI
katika kikao cha wadau wa Afya kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa
kujadili mipango na shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau hao mkoani
Simiyu.
Sagini amewaomba Wakuu wa wilaya
Bariadi, Busega na Itilima kuwa fedha
hizo zitakapoletwa wazisimamie kwa ukaribu na kuhakikisha ujenzi wa hospitali
hizo unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma.
Aidha, Sagini ametoa wito kwa
wadau wa afya mkoani humo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuboresha huduma za afya kwa kuwekeza
zaidi katika vipaumbele vya Mkoa huo hususani ujenzi wa Miundombinu ya afya
ikiwemo Vituo vya Afya na zahanati ambavyo mahitaji yake ni makubwa kwa
wananchi.
“Tuna vituo vya Afya 17 kati
ya130 vinavyotakiwa na kuna juhudi zinafanywa na wadau vituo vya Afya vingine
sita vinajengwa, zahanati ziko 192 mahitaji ni zahanati 279 na zinazoendelea
kujengwa 107; kuna uhitaji wa vituo vya kutolea huduma na ndiyo maana
tunalipigia kelele kweli suala hili” alisema Sagini.
Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba
akitoa taarifa ya maazimio ya kikao kilichopita, ameainisha mafanikio ya wadau
wa afya mkoani humo kuwa wamesaidia katika ujenzi na ukarabati wa vituo vya
afya, kutoa magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) katika baadhi ya vituo vya
kutolea huduma, kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuwepo kwa ongezeko la
matumizi ya huduma za uzazi wa mpango.
Naye Hererico
Ernest Afisa Mradi Amref Mkoa wa Simiyu, amesema Shirika hilo linatarajia
kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya 24 kupitia Mradi wa Uzazi Uzima,
ili viweze kutoa huduma stahiki kwa mama na mtoto
“ Katika wilaya ya Meatu
tutakarabati vituo vitatu, Maswa vituo vitano, Itilima vituo vinne, Bariadi
mjini vituo vitatu, Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi vituo viko vinne, Busega vituo vitano, tutavikarabati lengo
ni kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa wananchi, tutahakikisha huduma ya maji inapatikana
na katika baadhi ya vituo tutajenga majengo wodi za wazazi” alisema
Kwa upange wake Mratibu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu
duniani (UNFPA) Mkoa Wa Simiyu, Dkt Amir
Batenga amesema mfumo wa Serikali kutumia ‘Force Account’ katika ujenzi wa
vituo 38 vilivyojengwa na kukarabatiwa na shirika hilo umesaidia majengo hayo
kujengwa kwa gharama nafuu na ubora unaotakiwa chini ya usimamizi wa Watalaam
wa Halmashauri.
Kikao cha Wadau wa Afya Mkoa wa Simiyu kiliwahusisha
Viongozi na Watendaji wa Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Viongozi wa
madhehebu ya Dini na Wadau hao wakiwemo AMREF, AGPAHI, CUAMM, UNFPA, Mkapa Foundation, AMERICARE,
PSI, Red Cross, ICAP, INTRAHELTH, BORESHA AFYA na MARIESTOPES
Baadhi ya Viongozi,
watendaji na wadau wa afya wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa
Mkoa, Bw. Jumanne Sagini katika kikao kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini
Bariadi, kwa lengo la kujadili mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
Baadhi ya Viongozi,
watendaji na wadau wa afya wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa
Mkoa, Bw. Jumanne Sagini katika kikao kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini
Bariadi, kwa lengo la kujadili mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
Mratibu wa Mapambano
dhidi ya UKIMWI mkoa wa Simiyu , Dkt. Khamis Kulemba akitoa taarifa katika
kikao cha wadau wa afya wa Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Septemba 17,
2018 Mjini Bariadi, kwa lengo la kujadili mipango na shughuli za wadau hao
mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,
Mhe. Benson Kilangi, akichangia hoja katika kikao cha viongozi, watendaji na
wadau wa afya wa Mkoa huo, kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi, kwa
lengo la kujadili mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
Mratibu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa
Linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Mkoa Wa Simiyu, Dkt Amir Batenga
akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya wa Mkoa
huo kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi, kwa lengo la kujadili
mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Kikristo(CCT) Mkoa wa Simiyu, Mch. Martine
Nketo(kushoto) akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola katika kikao
cha wadau wa afya wa mkoa huo kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika
lisilo la Kiserikali la ICAP akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya
wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi.
Mmoja wa wadau wa Afya
Mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao cha viongozi, watendaji na wadau wa
afya wa Mkoa huo, kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi, kwa lengo la
kujadili mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiongoza kikao cha viongozi, watendaji
na wadau wa afya wa Mkoa huo, kilichofanyika Septemba 17, 2018 Mjini Bariadi,
kwa lengo la kujadili mipango na shughuli za wadau hao mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment