Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John
Pombe amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi.
Isack Kamwelwe na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kusimamia Ujenzi wa Daraja la
Mto Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida na kuhakikisha
linakamilika ifikapo Machi, 2019.
Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 10, wakati
akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu na Singida katika Kijiji cha Nyahaa
wilayani Mkalama Mkoani Singida muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi
ujenzi wa daraja hilo.
Amesema daraja hilo limeanza kujengwa muda mrefu na
akazikataa sababu zilizotolewa na Mkandarasi kuwa zimepelekea kuchelewesha
ukamilishaji ikiwemo mkandarasi kufanya kazi miezi minne tu kwa mwaka kutokana
na eneo hilo kuwa na maji mengi hususani kipindi cha mvua.
"Wananchi wa hapa wanahitaji daraja limalizike
hawahitaji sababu, mkandarasi alipokuwa akiomba kazi hakujua kuwa hapa maji
huwa yanapita, ma-engineer hawakujua? Hapa hakuna sababu,msitafute
kisingizio"
"Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote,
Mtendaji Mkuu TANROADS nataka daraja hili sasa likamilike, mimekuja kwa
makusudi kuweka jiwe la msingi nataka siku nikirudi nipite juu" alisema
Rais Magufuli
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi. Isack Kamwelwe amesema Daraja la Mto Sibiti likikamilika
litakuwa mkombozi katika kuunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na mkoa wa Singida
na kuahidi ujenzi wa kilomita 25 za lami kwenye tuta la daraja hilo.
"Daraja hili limejengwa katika viwango vya juu
sana, tuta lake pia limejengwa kwa kiwango cha juu sana na tayari tumeshaongea
na TANROADS kwamba kupitia kwenye fedha za matengenezo, tuta hili kwa karibu
kilomita 25 tutaziweka lami Mhe. Rais, tutaposhindwa tutakupa taarifa"
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi. Patrick
Mfugale amesema kazi ya Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti inayofanywa na Mkandarasi
Hainan
International Limited kutoka nchini China na mpaka sasa umefikia asilimia 70 na hadi
kukamilika kwake litagharimu jumla ya shilingi bilioni 16.3.
Rais amehitimisha Ziara yake ya siku tatu mkoani
Simiyu Septemba 10, ambapo akiwa Simiyu alipata nafasi ya kuweka mawe ya
msingi, kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi
katika maeneo mbalimbali kupitia mikutano ya hadhara.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe
kuashiria Uwekajiwa Jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba
10, 2018, wengine ni viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, viongozi wa dini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na akiwa
pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, viongozi wa dini, akivuta utepe kuashiria Uwekaji wa Jiwe la
Msingi la Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida,
Septemba 10, 2018.
Viongozi mbalimbali wa,
Chama, Serikali na Viongozi wa madhehebu ya Dini wakishangilia mara baada
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mto
Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Sehemu
ya Daraja la Mto Sibiti ambalo Ujenzi wake umewekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Septemba 10, 2018.
Baadhi ya wananchi wa
Mikoa ya Simiyu na Singida wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipozungumza nao katika Kijiji cha
Nyahaa wilayani Mkalama kabla ya kuweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti
ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea eneo maalum
lililoandaliwa kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi Daraja la Mto
Sibiti Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10,
2018.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi. Isack Kamwelwe akiwasalimia
wananchi wa Wilaya ya Mkalama(Singida) na Wilaya ya Meatu (Simiyu) Kijiji cha
Nyahaa wilayani Mkalama, kabla ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuweka Jiwe
la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida,
Septemba 10, 2018
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara (TANROADS) Mhandisi. Patrick Mfugale, mara baada ya kumalizika
zoezi la Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha
mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa
Wilaya ya Mkalama(Singida) na Wilaya ya Meatu (Simiyu) katika Kijiji cha Nyahaa
wilayani Mkalama mara baada ya kuweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti
ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi. Patrick Mfugale akitoa taarifa
ya Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo,
Septemba 10, 2018.
Kutoka kulia Mkuu wa
Wilaya ya Maswa, mhe. Dkt. Seif Shekalaghe, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na (kushoto) Mkuu wa
Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara (TANROADS) Mhandisi. Patrick Mfugale, mara baada ya kumalizika zoezi
la Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa
ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Simiyu na Singida wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipozungumza nao katika Kijiji cha Nyahaa wilayani Mkalama kabla ya kuweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Baadhi ya Viongozi wa
Mikoa ya Simiyu na Singida wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla ya
uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya
Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo akiwasalimia
wananchi wa Wilaya ya Mkalama(Singida) na Wilaya ya Meatu (Simiyu) katika Kijiji
cha Nyahaa wilayani Mkalama kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo
litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
Waziri wa Maji na
Umwagiliaji , Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya
Mkalama(Singida) na Wilaya ya Meatu (Simiyu) katika Kijiji cha Nyahaa wilayani
Mkalama, kabla ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuweka Jiwe la msingi
Ujenzi wa Mto Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba
10, 2018.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya
Mkalama(Singida) na Wilaya ya Meatu (Simiyu) katika Kijiji cha Nyahaa wilayani
Mkalama, kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mto
Sibiti ambalo litaunganisha mikoa ya Simiyu na Singida, Septemba 10, 2018.
0 comments:
Post a Comment