Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli atafanya ziara ya siku tatu (03) Mkoani Simiyu,
kuanzia kesho tarehe 08/09/2018 hadi tarehe 10/09/2018, Mkoani Simiyu.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake
Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amesema Mhe. Rais akiwa mkoani Simiyu atapata
nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi,
kufungua pamoja na kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Mtaka
amesema siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2018, Mhe. Rais atakagua na kuweka jiwe
la msingi Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Lamadi uliopo wilayani Busega na baadaye,
ataelekea wilayani Bariadi.
Aidha,
amesema Mhe. Rais akiwa katika Wilaya ya Bariadi, atafungua Jengo la Wagonjwa
wa Nje(OPD) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, atakagua na kufungua barabara
za lami (kilomita 6.9) zilizojengwa chini ya mradi wa kuboresha Miundombinu ya
Miji (ULGSP).
“Siku
hiyo pia atakagua maendeleo ya Ujenzi wa
barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka
jiwe la msingi. Mhe.Rais atapokea salamu za Chama Cha Mapinduzi, salamu za
Wilaya, Mkoa, taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara na baadaye kuzungumza na
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania wote kwa ujumla, katika Mtaa wa
Salunda kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda.”
“Tarehe
09/09/2018 Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima eneo la Makao
Makuu ya Wilaya (Lagangabilili) na kuelekea wilayani Meatu. Akiwa njiani
kuelekea Meatu Mhe. Rais atapata fursa ya kusalimia wananchi wa Kijiji cha
Mwandoya na baadaye atafungua Miundombinu ya Uboreshaji wa Huduma za Afya
Hospitali ya Wilaya ya Meatu na kuzungumza na wananchi katika Viwanja vya
Stendi ya Mwanhuzi” Alisema Mtaka.
Ameongeza
kuwa Siku ya Jumatatu tarehe 10/09/2018 Mhe. Rais Magufuli atahitimisha ziara
yake Mkoani Simiyu kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Sibiti na
kuwasalimia wananchi. Daraja la Mto Sibiti ndilo linalounganisha Mkoa wa Simiyu
na Singida.
Katika
hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Simiyu hususani
katika Miji ya Lamadi, Bariadi, Lagangabilili, Mwanhuzi na vitongoji vyake
kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli atapita na
kufanya mikutano ya hadhara.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, kuhusu
ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08
hadi Septemba 10, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari Ofisini
kwake leo, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03)
kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10, 2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM
Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Waandishi
wa Habari, kuhusu ziara ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye
anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10,
2018 mkoani Simiyu.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ofisini
kwake alipozungumza nao leo, kuhusu
ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08
hadi Septemba 10, 2018
0 comments:
Post a Comment