Wananchi wa Kijiji cha Mwasubuya wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu wamesema Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya wenye ekari 514
utawasaidia kubadili maisha yao kiuchumi kwa kuwa wanatarajia kuongeza mavuno
kutokana na kuanza kutumia zana za kilimo za kisasa katika uzalishaji kuanzia
hatua ya kuandaa mashamba hadi kuvuna.
Wananchi hao wameyasema hayo baada ya makabidhiano ya
zana za kilimo za kisasa zitakazotumika kuanzia hatua ya kuandaa mashamba mpaka
kuvuna, kutoka Kampuni ya Agricom kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambayo
imewadhamini wananchi walio katika mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya,
yaliyofanyika katika eneo la Mradi Kijiji cha Mwasubuya, Septemba 03, 2018.
Wamesema pamoja na kuongeza uzalishaji kutokana na
uwepo wa maji ya uhakika ya Bwawa la Mwasubuya na matumizi ya zana bora, mradi
huo ambao utajikita zaidi katika kilimo cha mpunga pia utawawezesha
wananchi na hasa vijana kujiajiri kupitia kilimo cha mboga mboga,
hatimaye kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla.
“Tumefurahi sana kupata mradi wa umwagiliaji, hii ni
ajira kwetu hasa sisi vijana wenye nguvu, nina imani tukiutumia mradi huu
vizuri utatubadilisha sisi kiuchumi kwa sababu mashine za kisasa tulizoletewa
tutazitumia kulima eneo kubwa kwa muda mfupi, tutatongeza mavuno na kupata hela
nyingi ” alisema Daniel Ntobi Mkulima wa Mwasubuya
“Nimeupokea mradi huu kwa furaha kabisa na nina
uhakika kupitia mradi huu tutalima na kupata mazao mengi hatutakuwa na njaa
lakini pia mazao mengine tutauza ili tujenge nyumba nzuri, tusomeshe watoto hata
kijiji chetu kitabadilika, cha msingi hapa tuutumie vizuri” alisema Monica
Severine Mkulima kutoka kijiji cha Mwasubuya
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi amesema zana za kilimo zilizokabidhiwa na
Kampuni ya Agricom zitawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa zao la
mpunga na hivyo kuongeza pato la kaya zao na kukuza uchumi wa
Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema dhamira ya Serikali ni kuufanya
Mradi wa Umwagiliaji Mwasubuya kuwa wa mfano ambao watu kutoka sehemu
mbalimbali za dunia watakuja kujifunza, ambapo amebainisha kuwa mpunga
utakaolimwa utakuwa wa aina moja,utalimwa mara mbili kwa mwaka na
hautatumia mbolea za viwandani.
Ameongeza kuwa pamoja na kilimo cha mpunga, Serikali
mkoani humo imekusudia kufunga kinu cha kukoboa mpunga na kupanga madaraja ya
mchele na kupitia mradi huo pia kutakuwa na ufugaji wa samaki katika Bwawa la
Mwasubuya ambapo vifaranga vitawekwa na ufugaji kupitia vizimba utafanyika
sambamba na kufuga samaki katika baadhi ya mashamba ya mpunga.
“Kwenye bwawa mle tutaweka vifaranga vya sangara,
kambare na sato pia katika ekari zitakazolimwa ekari 10 zitatengwa ambazo
mkulima atalima mpunga na kufuga samaki kwa wakati mmoja, wakati akivuna mpunga
anavuna na samaki; tunataka kufunga kinu cha kukoboa mpunga na kupanga
madaraja, nawaambia maisha yenu yatabadilika, hapa ni mahali tunataka kuiambia
dunia Simiyu ni nini” alisema Mtaka.
Akizungumzia namna wakulima watakavyolipa deni la
mkopo wa zana bora za kilimo kutoka Agricom, Mtaka amesema Halmashauri italima
shamba lote ekari 514, itatoa mbegu kwa wakulima, itapanda na kuvuna na baadaye
itachukua sehemu ya mavuno(gunia 10 kwa ekari) kutoka katika matarajio
ya mavuno ya kati ya gunia 30 hadi 42 kwa ekari, ili kufidia gharama
za uzalishaji na kurejesha deni.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Agricom, Bi Angelina
Ngalula amesema kampuni hiyo inafanya kazi na Halmashauri na wakulima walio
tayari na kubainisha kuwa imekopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mashine
za kulimia, kupandia na kuvunia zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200
ambazo kwa mujibu wa makubaliano zitalipwa baada ya mavuno.
Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya una eneo lenye
ukubwa wa ekari 700 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na umesajiliwa kwa
Jina la Umoja wa Umwagiliaji Mwasubuya (UMWASU) wenye wanachama 198.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Agricom Africa, Bi. Anjelina
Ngalula juu ya aina ya kilimo cha mpunga
iitwayo Shadidi kilicholimwa katika baadhi ya mashamba yaliyo katika Mradi wa
Uwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi, kabla ya makabidhiano ya zana bora za
kilimo kati ya Kampuni hiyo na Wakulima walio katika Mradi huo, Septemba 03,
2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Mwasubuya akiwa katika Moja ya
Zana ya kupandia mpunga ambayo ni miongoni mwa zana zilizokabidhiwa kwa ajili
ya kuwawezesha wakulima wa mradi wa
Umwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha
Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Mwasubuya akiwa katika
trekta ambalo ni miongoni mwa zana
zilizokabidhiwa kwa ajili ya kuwawezesha
wakulima wa mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi kulima
kilimo cha kisasa kupitia mradi huo, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha
Mwasubuya.
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert Siogopi akiwaonesha baadhi ya
viongozi na wananchi mfereji unaotoa maji kutoka bwawa la Mwasubuya kwenda
kwenye mashamba ya Mradi wa Umwagiliaji Mwasubuya , kabla
ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kati ya Kampuni hiyo na Wakulima walio
katika Mradi huo, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa hafla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka
Kampuni ya Agricom Africa kwa Wakulima wa Umwagiliaji Mwasubuya, katika Kijiji cha Mwasubuya
wilayani Bariadi, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Baadhi
ya Wananchi wa Kijiji cha Mwasubuya wakishangilia jambo wakati wa hafla ya
makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom Africa kwa
Wakulima wa Umwagiliaji Mwasubuya,
katika Kijiji cha Mwasubuya wilayani Bariadi, Septemba 03, 2018 katika Kijiji
cha Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi na wananchi wakielekea kuangalia Bwawa na baadhi ya
mashamba katika Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya, kabla ya makabidhiano ya
zana bora za kilimo kutoka Kampuni ya
Agricom Africa na Wakulima walio katika Mradi huo, Septemba 03, 2018 katika
Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock
Yakobo , katika hafla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom Africa na Wakulima walio
katika Mradi wa Umwagiliaji , Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, akizungumza na baadhi ya viongozi mara baada
makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka
Kampuni ya Agricom Africa na Wakulima walio katika Mradi wa Umwagiliaji Mwasubuya , Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert Siogopi akitoa taarifa ya Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya ,
kabla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kati ya Kampuni ya Agricom
Africa kwa Wakulima walio katika Mradi huo, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha
Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Mwasubuya wakati wa hafla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo
kutoka Kampuni ya Agricom Africa kwa Wakulima walio katika Mradi wa
Umwagiliaji Mwasubuya,, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya
Baadhi ya Wananchi wa
Kijiji cha Mwasubuya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,
katika hafla ya makabidhiano ya zana
bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom
Africa kwa Wakulima walio katika Mradi
wa Umwagiliaji Mwasubuya,, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Kutoka kulia Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na Mkurugenzi wa Agricom Africa, Bi. Angelina Ngalula wakifurahia jambo,
katika hafla ya makabidhiano ya zana
bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom
Africa kwa Wakulima walio katika Mradi
wa Umwagiliaji Mwasubuya, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, akizungumza na baadhi ya viongozi mara baada
makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka
Kampuni ya Agricom Africa na Wakulima walio katika Mradi wa Umwagiliaji
, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akicheza wimbo maalum pamoja na
wananchi wa Kijiji cha Mwasubuya na
baadhi ya viongozi wa mkoa huo katika
hafla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom Africa kwa Wakulima walio katika Mradi wa
Umwagiliaji Mwasubuya, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo akiwa katika trekta ambalo ni moja ya
zana zilizokabidhiwa na Kampuni ya Agricom Africa kwa Wakulima walio katika Mradi wa
Umwagiliaji Mwasubuya, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwasubuya,
wakati wa hafla ya makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka Kampuni ya Agricom Africa kwa Wakulima walio katika Mradi wa
Umwagiliaji Mwasubuya,, Septemba 03, 2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Agricom Africa, Bi. Angelina
Ngalula juu ya aina ya kilimo cha mpunga
iitwayo Shadidi kilicholimwa katika baadhi ya mashamba yaliyo katika Mradi wa
Uwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi, kabla ya makabidhiano ya zana bora za
kilimo kati ya Kampuni hiyo na Wakulima walio katika Mradi huo, Septemba 03,
2018 katika Kijiji cha Mwasubuya.
Baadhi ya Viongozi wa
Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, katika hafla ya
makabidhiano ya zana bora za kilimo kutoka
Kampuni ya Agricom Africa kwa
Wakulima walio katika Mradi wa Umwagiliaji Mwasubuya,, Septemba 03, 2018 katika
Kijiji cha Mwasubuya.
0 comments:
Post a Comment