Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pole kwa waandishi wa habari watano wa
Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliopata ajali
katika wilayani Meatu, wakati akiwa ziarani wilayani humo, salamu ambazo
zimewasilishwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka, ambaye aliwatembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu walikokuwa
wakipatiwa matibabu.
Akiwasilisha salamu za Mhe.Rais, Mhe. Mtaka amesema magari matano ya Simiyu ya
Serikali na gari binafsi yaligongana na watu sita wakajeruhiwa wakiwemo
waandishi watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus
Kamani na kusisitiza kuwa Mhe. Rais
ameguswa na jambo hilo, hivyo ametoa shilingi laki tano kwa kila majeruhi ili iwasaidie
katika matibabu.
“...magari ya waandishi wa habari
lakini kulikuwa na gari binafsi, baada ya msafara wa Rais kwa sababu ya vumbi, dereva mmoja katika yale magari alisimama
kutaka kuona njia vizuri, magari yaliyokuwa yakifuatana matano yakagongana kwa nyuma, watu sita
wakapata majeraha miongoni mwao walikuwepo waandishi wetu watano na Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani”
“Mhe. Rais anatoa salamu zake za
pole kwa majeruhi wote, ameguswa sana na
jambo hili hasa pale aliposikia kuwa sehemu ya majeruhi ni waandishi ambao
tumekuwa nao pamoja katika ziara hii, wakafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha
Watanzania, akaomba mimi kama Mkuu wa
Mkoa nifikishe salamu zake za pole kwa niaba
yake kwa watu hawa sita” alisema.
Ameongeza kuwa Mkoa utaendelea
kuchukua tahadhari kupitia jeshi la polisi hasa katika misafara ya viongozi na
kuhakikisha kuwa wanajenga uelewa wa pamoja kwa madereva wakati wa maandalizi
ya safari juu ya namna ya kuchukua tahadhari.
.Rehema Evance ambaye ni
mwandishi wa Azam TV amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua na kuona
awape mkono wa pole ambao amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia katika
kugharamia matibabu.
“ Kwanza namshukuru Mungu kwa kutujalia tukapona, lakini kipekee napenda kumshukuru Mhe. Rais
kwa kuona kuna haja ya kutusaidia katika hili, kwa hiki alichotoa Mungu
ambariki sana kitatusaidia kwenye matibabu, tunaahidi kuendelea kuwahabarisha
Watanzania na kuhakikisha yale yote yanayotendeka ndani ya nchi yanawafikia”
alisema.
Ajali hii iliyotokea wilayani Meatu Septemba 09, 2018 imesababisha majeruhi
sita ambao ni waandishi watano Rehema Evance (AZAM TV), Belensi China(ITV),
Aidan Mhando(Channel Ten), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mpiga Picha Samson
Masunga pamoja na Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani na hakuna kifo
kilichotokea.
.
Majeruhi wote walipatiwa matibabu
katika Hospitaliya Wilaya ya Meatu ambapo waandishi wa habari Rehema Evance (AZAM TV), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo
ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliruhusiwa na Belensi China(ITV),
Aidan Mhando(Channel Ten), na Mpiga Picha Samson Masunga walipewa Rufaa kwenda
Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi salamu za pole kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa Mwandishi
wa habari wa AZAM TV, Bi Rehema Evance ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari
iliyotoea Septemba 09, 2018, wakati Mhe.Rais akiwa ziarani mkoani humo.
Kutoka Kushoto Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dk t.
Joseph Chilongani na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakimjulia hali,
Mwandishi wa habari wa AZAM TV, Bi Rehema Evance ambaye alijeruhiwa katika
ajali ya gari iliyotoea Septemba 09, 2018, wakati Mhe.Rais akiwa ziarani mkoani
humo
0 comments:
Post a Comment