Saturday, September 29, 2018

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAJIPANGA KUDHIBITI ONGEZEKO LA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO


Mkoa wa Simiyu utahakikisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua kwa kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imewekeza na kutumia gharama kubwa katika kuandaa wataalam(wakunga) wenye jukumu la kuhakikisha wanatoa huduma zitakazotoa majibu sahihi ya utatuzi wa changamoto hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakati akifunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa wakina mama na watoto wachanga chini ya mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka yaliyohusisha wakunga kutoka katika Halmashauri zote sita mkoani humo.

Kiswaga amesema pamoja na kuwepo dalili za kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito na  watoto wachanga mkoani huo bado ipo haja ya kujitathmini ili kubaini ukubwa wa tatizo kama njia ya kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

“ Ni kweli ukilinganisha takwimu za mwaka jana na mwaka huu zinaonyesha idadi ya vifo vinavyotokana na matatizo mbalimbali ya uzazi vimepungua, lakini naomba niwape angalizo,  tusizichukulie takwimu hizi kama kigezo cha ubora wa huduma zinazotolewa katika vituo vyetu, bali iwe chachu ya kufanya kazi kwa bidii  ili fikapo mwezi Desemba mwaka huu tuwe katika nafasi ya juu zaidi”.

Aidha Kiswaga amewaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuhakikisha wanaitumia kikamilifu elimu waliyoipata ili iwawezeshe kukabiliana na dharula wakati wa kuwahudumia wakina mama wajawazito na watoto wachanga na kuongeza kuwa serikali haitamvumilia mkunga yeyete atakayetumia kisingizio cha aina yoyote kwa kusababisha kifo cha mama au mtoto.

Halikadhalika Kiswaga ameishukuru serikali ya Canada kupitia chama cha wakunga cha nchi hiyo CAM na kusema kuwa imefanya uamuzi sahihi wa kuisaidia Tanzania katika eneo hili nyeti la kuwajengea uwezo wataalamu hao watakaotumika kuboresha huduma za  afya ya mama na mtoto na kuahidi kuwa serikali iko tayari kupokea ushauri utakaosaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Kwa upande wake rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA  Feddy Mwanga amesema tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mkunga mwenye mafunzo yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili akina mama wajawazito na watoto wachanga kwa 87%.

“ Hivyo kwa sisi wakunga tunaamini hatua hiyo ni nzuri na kwamba kinachofuata sasa ni kuwahimiza wakina mama wahudhurie kliniki mapema na kwa wakati na hapa ndipo tunaweza kupima mafanikio ya mpango huu kupitia kwa wahitimu hawa tunaowakabidhi vyeti hii leo” alisema Bi Mwanga.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyobebwa na kauli mbiu ya Mkunga Okoa Maisha -Jonas Julius ameiomba Serikali kuboresha mazingira yao ya kutolea huduma ikiwemo kuwapatia nyumba za kuishi jirani na vituo vya kazi sambamba na kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya wakunga 500 ambapo  kupitia mpango huo jumla ya wakunga 220 wamenufaika na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na CUSO International, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) pamoja na Chama cha wakunga Canada (CAM) .
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya Mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito  na watoto wachanga chini ya Mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018. 


Rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA  Feddy Mwanga akitoa taarifa ya mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa  akina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya Mradiwa Mkunga Okoa Maisha, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo mkoani Simiyu, Septemba 28, 2018.
Mkunga Jonas Julius akisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya Mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
 Mratibu wa Mradi wa Mkunga Okoa Maisha Martha Rimoy akitoa taarifa ya mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, katika hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.


Mwakilishi wa Chama cha Wakunga cha nchini Canada (CAM) Bi. Sylivia akitoa uzoefu wake wa namna wakunga wanavyofanya kazi nchin humo, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, iliyofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka akizungumza jambo katika hafla ya kufunga mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, iliyofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha wakunga nchini (TAMA), Mwakilishi wa Chama cha Wakunga cha nchini Canada (CAM) Bi. Sylivia, baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, baada ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.
Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Grace Mgombera akizungumza jambo katika hafla ya kufunga mafunzo ya yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito  na watoto wachanga, iliyofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
 Mkunga wa Zahanati ya Badugu, Bw. Ramdhani akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga,  kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018. 


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(wa pili kulia) pamoja na viongozi wa Chama cha wakunga nchini (TAMA), , baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo pamoja na wakunga(hawapo pichani) walioshiriki mafunzo ya ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, kabla ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(wa pili kulia) pamoja na viongozi wa Chama cha wakunga nchini (TAMA), baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo pamoja na wakunga(hawapo pichani) walioshiriki mafunzo ya ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, kabla ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.
Baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018. 
Baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!