Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde ametoa wito kwa
Wazazi nchini kuwalea watoto wao katika maadili mema ili
kuwaepusha na matumizi ya dawa za kulevya na Maambukizi
ya Virusi Vya Ukimwi.
Ushauri huo ameutoa wakati
akifungua makambi ya siku saba ya Kanisa la Waadventisa Wasabato mkoani SIMIYU,
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mavunde amesema malezi ya watoto ni jambo muhimu sana
hasa katika kizazi cha hivyo watoto wakikosa malezi bora katika umri walio nao
ni rahisi kutumbukia katika makundi yasiyofaa yakiwemo ya matumizi ya dawa za
kulevya na hivyo kukosa nguvu kazi ya Taifa.
“Kwa mujibu wa takwimu Tanzani kila siku watu 200 wanapat
maambukizi mapya ya VVU katika watu 200 watu 80 ni vijana katika hao vijana 80
asilimia 80 ni watoto wa kike, hivyo tuendelee kuelemisha na kuliandaa hili kundi kubwa la Vijana
katika malezi bora ili wawe nguvu kazi ya kuleta tija katika Taifa letu”
alisema.
Ameongeza kuwa ili watu waweze kuondokana na umaskini ni
lazima wafanye kazi hivyo akatoa wito kwa Viongozi, waumini wa Kanisa la
Waadventisa Wasabato na wananchi wote kufanya kazi kwa staha, uadilifu na
malengo ili waweze kufanikiwa kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema
makambi hayo ni sehemu ya Maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma
na Wajasiriamali Waadventista Wasabato (ATAPE) unatarajiwa kufanyika mwaka 2019
mkoani humo.
Aidha, Mtaka alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa
mwaka 2019 kutakuwa na matukio makubwa matatu ambayo yataitambulisha Simiyu
ambayo ni mkutano huo wa ATAPE, Mkutano wa Madaktari wa Nchi nzima na Maonesho
ya Nanenane ya Kimataifa.
Katika hatua nyingine amewahimiza wananchi kujifunza
masuala ya Ujasiriamali na kuwakaribisha katika Maonesho ya Viwanda Vidogo SIDO
yatakayofanyika Kitaifa mwaka huu 2018 kuanzia tarehe 24 hadi 28 Oktoba, 2018
katika Viwanja vya Nyakabindi.
Awali akitoa somo kuhusu masuala ya Ujasiriamali,
Mchungaji Joshua Njuguna aliwasisitiza waumini wote kuwa siyo mpango wa Mungu
mtu yeyote awe maskini , akawaasa kufanya kazi ili kuutafuta utajiri hivyo akawataka wazitafute fursa za kupata
utajiri na kufanya kazi kwa bidii.
Pia Naibu Waziri MAVUNDE ameahidi kuchangia
jumla ya mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuwaunga mkono WAUMINI HAO
katika ujenzi wa Hospitali ya Kanisa katika eneo la Pasiasi
jijini Mwanza.
Ufunguzi wa makambi umehudhuriwa na waumini mbalimbali
kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, lengo likiwa ni kujifunza neno la Mungu,
kutoa elimu ya ujasiriamali, mafunzo ya ndoa na malezi ya watoto na kuliombea Taifa.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge
Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu Mhe.
Anthony Mavunde(mwenye miwani), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
wakikagua gwaride la Vijana Kanisa la Waadventista Wasabato katika ufunguzi wa
makambi Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akivisha
skafu na Vijana Kanisa la Waadventista
Wasabato kabla ya ufunguzi wa makambi Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018 ambao
alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye skafu kulia) akiimba pamoja na Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista
Wasabato(SDA) Kurasini, katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo yanayofanyika
Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018 .
Baadhi ya
waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) wakifuatilia hotuba ya Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na
Walemavu Mhe. Anthony Mavunde katika
ufunguzi wa makambi yanayofanyika Mjini
Bariadi, Septemba 18, 2018
Waimbaji
wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) wakiimba katika ufunguzi wa
makambi ya Kanisa hilo yanayofanyika
Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde(wa tatu kilia) na
viongozi wengine wa Serikali na Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA),
wakifuatilia mafundisho katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18,
2018 ambayo yanafanyika Mjini Bariadi
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), wakati akifungua makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), wakati akifungua makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na waumini wa Kanisa
la Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo
Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika
Mjini Bariadi.
Mchungaji
wa Kanisa la Waadiventista Wasabato kutoka Nchini Kenya Joshua Njuguna Kenya
akitoa mafundisho, katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018
ambayo yanafanyika Mjini Bariadi.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na
Walemavu Mhe. Anthony Mavunde (mwenye
miwani) akipokea zawadi kutoka kwa wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la
Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba
18, 2018 ambayo yanafanyika Mjini
Bariadi.
Mkuu wa
Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akipokea zawadi kutoka kwa
wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika
ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akipokea zawadi kutoka kwa
wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika
ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika Mjini Bariadi
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na
Walemavu Mhe. Anthony Mavunde( wa pili
kushoto ) akisalimiana na mmoja wa Viongozi wa ATAPE mkoa wa Simiyu, Eng. Paul
Jidayi mara tu alipowasili Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi kufungua
makambi ya Kanisa la Waadiventista Wasabato(SDA) , Septemba 18, 2018.
0 comments:
Post a Comment