Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema atatoa kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali
ya Mkoa wa Simiyu na kuutaka Wakala wa Majengo hapa nchini (TBA) kujenga
majengo hayo usiku na mchana, ili kuhakikisha yanakamilika katika kipindi cha
meizi sita kama ilivyoahidiwa na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 08, 2018 katika Uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la
Hospiali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika mtaa wa Nyaumata mjini Bariadi,
wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Dkt Magufuli amesema kuwa atatoa shilingi bilioni nne
ambazo zitasaidia kujenga majengo mengine ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu na
maeneo jirani waweze kupata huduma za rufaa huku akieleza kuwa kutokana na umuhimu wa sekta ya afya
shirika la Global fund wametoa shilingi bilioni 1.5.
“Leo ninafungua jengo hili na nakugiza Mhe. Waziri wasaidizi
wako na TBA anzeni kupima majengo mengine yote yaliyobaki muanze leo fedha zitatatolewa,
zipo za global fund bilioni1.5 zipo za Serikali bilioni 1.5 na mimi nawaongezea
nyingine bilioni nne ziwe bilioni saba, ninachowaomba TBA mjenge usiku na
mchana” alisema.
Awali akitoa taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa
Nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Waziri wa
Afya,jinsia ,wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa jengo hilo lianza
kujengwa Novemba 2015 na kukamilika Mei 2018, limegharimu kiasi cha bilioni 2.1
ikiwemo na fidia ya eneo.
Ameongeza kuwa Wizra ya Afya itahakikisha miundombinu
yote muhimu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inakamilika, ili Hospitali hiyo iweze
kutoa huduma bora kwa wananchi, ambapo amebainisha kuwa hospitali hiyo
itapunguza mlundikano wa wagonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa ambayo ina
hadhi ya Hospitali ya Wilaya.
Aidha, Mhe. Waziri Ummy amemuahidi Mhe. Rais kuwa yeye kwa
kushirikiana na wasaidizi wake watahakikisha majengo ambayo yatajengwa kwa
kutumia fedha aliyoahidi kuitoa yanakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita,
ambapo alisema kwa sasa huduma za wagonjwa wa nje, huduma za dharura, usatwi wa
jamii na huduma za maabara vipimo vya kawaida zinatolewa
Ummy pia alibainisha kuwa katika bajeti ya mwaka
2018/2019, Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi
wa hospitali ya Mkoa ambayo kukamilika kwake kutawapunguzia wananchi wa Simiyu kufuata
huduma za rufaa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
amesema katika mwaka wa fedha 2017.2018 mkoa wa Simiyu umepokea shilingi
bilioni 11 kwenye sekta ya Afya ambapo Vituo vya Afya 39 vimejengwa na
kukarabatiwa pamoja na bilioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa dawa.
Pamoja na kufungua Jengo la
Wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Mhe. Rais
Magufuli amefungua Mtandao wa barabara za lami Mjini Bariadi zilizojengwa chini
ya mradi wa ULGSP, kuweka jiwe la msingi mradi wa maji Lamadi na kuweka jiwe la
Msingi Ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami
yenye urefu wa KM 49.7.
Sepemba 09, 2018 Mhe. Rais
Magufuli anaendelea na ziara mkoani Simiyu ambapo atapita na kufanya mkutano wa
hadhara Lagangabilili Itilima na kuelekea Meatu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara
baada ya kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Simiyu, Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Sehemu
ya mbele ya Jengo la Wagonjwa wa Nje la
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Jiwe la
msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa KM 49.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami , Septemba O8, 2018 wakati
akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia na baadhi ya
Mawaziri na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu, baada ya kuweka Jiwe la msingi,
ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa KM 49.7 inayojengwa kwa
kiwango cha lami , Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Baadhi
ya Wananchi wa Mkoa waSimiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo
pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya
Msingi Salunda Mjini Bariadi, Septemba O8, 2018 wakati
akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa
Kata ya Lamadi katika Kijiji cha Kalago mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Lamadi, Septemba 08, 2018
katika ziara ya Rais mkoani Simiyu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara
baada ya kuweka Jiwe la msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu
wa KM 49.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami , Septemba
O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku
tatu mkoani humo.
Viongozi
mbali mbalimbali wakifurahia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli, kuweka Jiwe la msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa
yenye urefu wa KM 49.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami , Septemba O8, 2018 wakati
akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(anayeshangilia kulia) akifurahia
baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kuahidi kutoa bilioni nne kwa ajili kuendeleza
Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Septemba
O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku
tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada kuweka
Jiwe la msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa KM 49.7
inayojengwa kwa kiwango cha lami , Septemba
O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku
tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka Septemba 08, 2018 ,
wakati wa ziara yake ya Siku tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda Mjini
Bariadi, Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika
ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Mkoa wa Simiyu baada ya
Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda Mjini
Bariadi, Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika
ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada kuweka Jiwe la
msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa KM 49.7 inayojengwa
kwa kiwango cha lami , Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo
0 comments:
Post a Comment