Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasilianona Uchukuzi
kutafuta Mkandarasi wa Ujenzi wa barabara za lami (kilomita tatu ) katika Mji
wa Mwanhuzi wilayani Meatu Mkoani Simiyu.
Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 09, 2018
wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika
Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakati akiwa
katika ziara yake mkoani humo.
Amesema wakati akiwa Waziri wa ujenzi aliahidi
ujenzi wa barabara hiyo Waziri wa ujenzi Mawasiliano na uchukuzi ahakikishe
anamtafuta Mkandarasi ili aanze kufanya kazi hiyo mwezi huu Septemba 2018, ili
ahadi hiyo aliyoitoa kwa wananchi wa Meatu itimie.
“Wakati nilipokuja hapa nikiwa Waziri wa Ujenzi niliahidi
ujenzi wa kilomita tatu za lami, nimeshaangaa sana kuona hizo kilomita
hazijajengwa, nakuagiaza Waziri wa Ujenzi kabla mwezi huu haujaisha nimuone
mkandarasi anaanza kufanya kazi hapa” alisema
Aidha, Mhe. Rais amewataka wananchi kushirikiana na
viongozi wao katika kujiletea maendeleo huku akiwasisitiza kuacha kujichukulia
sheria mkononi na badala yake wazingatie sheria za nchi.
Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli amewaagiza
Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kuweka mipango itakayowezesha wakulima na wafugaji wanafanya shughuli zao kwa
amani.
Awali akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo una mpango wa kutambua na kuyapima maeneo
ya Wafugaji na kuyawekea miundombinu ili wafugaji waachane na ufugaji waachane
na kuhama hama na wafuge kwa tija.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi amesema Serikali inajiandaakufanya usanifu wa awali wa Ujenzi wa
barabara ya Bariadi-Itilima-Kisesa-Mwandoya-Ng’oboko-Sibiti ili kwa baadaye ijengwe katika kiwango cha
lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Simiyu, ambapo
Septemba 10 amesalimia wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Lagangabilili
Itilima, Kisesa, Mwandoya, mkutano wa hadhara Mwanhuzi na kufungua majengo ya
uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa niaba ya
vituo vingine 39.
MWISHO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu mkoani Simiyu,
Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika
ziara yake mkoani humo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoka
kukagua majengo ya majengo ya uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya
Wilaya ya Meatu, kabla ya kufuungua kwa niaba ya vituo vingine 39, Septemba 09,
2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Wananchi
wa Tarafa ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipowasilimia, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Baadhi
ya viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi
wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Baadhi
ya viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi
wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi wa wilaya ya Meatu na
Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya mara baada ya kufungua majengo ya
uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa niaba ya
vituo vingine 39, Septemba 09, 2018 wakati
akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Wananchi
wa Tarafa ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipowasilimia, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
akizungumza na viongozi wa wilaya ya Meatu na Baadhi ya watumishi wa sekta ya
afya, mara baada ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kufungua majengo ya
uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa niaba ya
vituo vingine 39, Septemba 09, 2018 wakati
akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Baadhi
ya viongozi wa wilaya ya Meatu na watumishi wa sekta ya afya,
wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
mara baada ya kufungua yamajengo ya
uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa
niaba ya vituo vingine 39, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo mara baada
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kufungua majengo ya uboreshaji wa
huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa niaba ya vituo vingine
39, Septemba 09, 2018 wakati akiwa
katika ziara yake mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo
akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja
vya Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo.
Wananchi
wa Mji wa Mwanhuzi wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa hadhara , Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli(kulia) akifuatilia jambo katika mkutano wake na
viongozi wa wilaya ya Meatu na Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya, mara baada
ya kufungua majengo ya uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya
ya Meatu, kwa niaba ya vituo vingine 39, Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu, (kushoto ) Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe. Anthony Mtaka ( katikati) Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA hapa nchini Bi.
Jacqueline Mahon.
Wananchi
wa Mji wa Mwanhuzi wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa hadhara , Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Wananchi
wa Mji wa Mwanhuzi wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa hadhara , Septemba 09, 2018 wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment