Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Askofu
wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana,wametoa
salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela, wananchi wa Mwanza
pamoja na familia na ndugu wa waliopoteza maisha katika ajali ya kuzama kwa
Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 huko Ukerewe Mwanza.
Wakitoa salamu hizo kwa nyakati tofauti Septemba 22,
2018 wakati wa kufunga makambi ya
Waadiventista Wasabato katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani
Simiyu, Mhe. Mtaka na Askofu Malekana wamewaombea majeruhi wote wapone haraka
na kurejea katika majukumu yao.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Simiyu amasema msiba
huo mkubwa umewagusa watu wengi ikiwepo mkoa waSimiyu ambapo mwalimu mmoja
kutoka katika Kata ya Kalemela wilayani Busega amepoteza maisha katika ajali
hiyo.
“Mkoa wa Simiyu katika wilaya ya Busega mwalimu wetu
mmoja wa Shule ya msingi katika kata ya Kalemela, Mwalimu Mtaki amefariki kwenye ajali hii alikuwa naenda
kusalimia wazazi wake, huu ni msiba ambao umegusa maeneo mengi”
“ Kwa niaba ya wananchi wote wa mkoa wa Simiyu tunatoa
salamu za pole kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela, wananchi wa
Mwanza lakini zaidi pole kwa familia ambazo zimeguswa na jambo hili tunawaombea
kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote na wale ambao wamenusurika Mungu aendelee
kuwaimarisha wapone haraka” alisema Mtaka
Ameongeza kuwa Viongozi wa Mkoa wa Simiyu
siku ya Jumapili tarehe 23 Septemba, 2018 wataungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, viongozi wa Mkoa wa Mwanza, viongozi wengine
wa Serikali katika tukio la kuwahifadhi waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Naye Askofu wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana amesema “Kwa niaba ya Kanisa
la Waadventista Wasabato na washiriki wote napenda kutoa salamu za pole kwanza
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela, wananchi wa Mwanza kwa msiba huu
mzito ulioleta majonzi kwetu Watanzania”
“Kanisa pia linatoa pole kwa familia
zilizoguswa na ajali hii na ni ombi la kanisa kwamba wale ambao walijeruhiwa
Mungu awapatie uponyaji wa haraka na wale ambao wamelala ambao waliweka maisha
yao kwa Yesu ahadi ni kwamba Yesu atakapokuja mara ya pili atawaita kutoka
makaburini" alisema Askofu Malekana
Ameongeza kuwa Kanisa linaungana na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, viongozi
wengine na wananchi kuomba utulivu na mshikamano wakati huu wa majonzi.
MWISHO.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa
salamu za pole kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo, kufuatia vifo vilivyotokana na
ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere huko Ukerewe mkoani Mwanza, Septemba
20, 2018, salamu hizo zimetolewa wakati wa kufunga
makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la
Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana akitoa salamu za pole
kwa niaba ya Kanisa hilo, kufuatia vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa
Kivuko cha MV Nyerere huko Ukerewe mkoani Mwanza, Septemba 20, 2018, salamu hizo
zimetolewa wakati wa kufunga makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania,
Mark Malekana wakiteta jambo wakati wa kufunga makambi ya Waadiventista
Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la
Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana(kushoto) akimkaribisha Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka azungumze na Waumini wa Kanisa la Waadiventista Wasabato wakati wa kufunga makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
akizungumza na Waumini wa wa Kanisa la Waadiventista Wasabato
wakati wa kufunga makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22,
2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na Kiongozi wa ATAPE mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Paul Jidayi mara
baada ya kufunga makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22,
2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wachungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato
wakifuatilia Hotuba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka(hayupo
pichani) wakati wa kufunga makambi ya Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini
mwa Tanzania, Mark Malekana akifurahia jambo wakati Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipozungumza na Waumini wa Kanisa hilo katika kufunga makambi yao Septemba
22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kurasini
wakimtukuza Mungu kwa nyimbo wakati wa kufunga makambi ya kanisa hilo Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Waumini wa wa Kanisa la
Waadiventista Wasabato wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kufunga makambi ya
Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu.
Watoto wa Waumini wa Kanisa la Waadiventista Wasabato wakionesha
mambo mbalimbali waliyojifunza katika makambi Mjini Bariadi yliyofungwa
Septemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya AY Nyarugusu Kanisa la
Waadventista Wasabato Geita wakimtukuza Mungu kwa nyimbo wakati wa kufunga
makambi ya kanisa hilo Septemba 22, 2018
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Waumini wa wa Kanisa la
Waadiventista Wasabato wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kufunga makambi ya
Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Waumini wa wa Kanisa la
Waadiventista Wasabato wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kufunga makambi ya
Waadiventista Wasabato Septemba 22, 2018 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment