Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali itahakikisha maeneo yote
yanayozunguza Ziwa Victoria yanapata maji safi na salama ili kuwaondolea adha
wananchi wa maeneo hayo ambayo
yanazungukwa na rasimali hiyo muhimu.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati
akizungumza na wananchi wa kata ya Lamadi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa mradi wa maji wa Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu, ambao
umegharimu shilingi bilioni 12.8 fedha ambazo ni mkopo kutoka Benki ya
Maendeleo ya Ufaransa na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya.
“Tumeamua Serikali ya Awamu ya Tano
kuanza mpango wa kuhakikisha miji yote iliyo kando kando ya Ziwa Victoria
inapata maji na ndiyo maana Lamadi mmepaa maji hongereni sana; mradi huu utatoa
lita milioni 3.3 kwa siku mahitaji ya maji ya hapa ni lita milioni 1.8 kwa hiyo
ni maji mengi yatakuwa yanatoka kwa siku kuliko mahitaji” alisema Rais
Magufuli.
Aidha, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Busega
kuutunza mradi huo na akawaonya kuwa endapo watahujumu miundombinu na kuuharibu
serikali haitapeleka mradi mwingine.
Naye Waziri wa maji na Umwagiliaji, Mhe.
Makame Mbarawa amesema mradi huo utakapo kamilika mwezi Mei 2018 utawahudumia
zaidi ya watu laki tatu watapa maji safi na salama.
Prof. Makame Mbalawa amesema ili
kuondokana na changamoto ya maji katika Mkoa wa Simiyu Serikali imekusudia
kutekeleza mradi mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria utakaowanufaisha wananchi
wa Wilaya ya Bariadi,Itilima na Mwanhuzi Meatu, ambao utagharimu shilingi bilioni
378.
Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi,
Mhe. Rais Magufuli pia amefungua Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Kufungua Mtandao wa barabara za lami Mjini Bariadi
zilizojengwa chini ya mradi wa ULGSP na kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa
Barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye refu wa KM
49.7.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi
mbalimbali mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Lamadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa (kulia)akimuongoza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli kwenda katika eneo ambalo aliweka Jiwe la Msingi la Mradi wa
Maji wa Lamadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua
Mtandao wa barabara za Lami za Mjini Bariadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa
kabla ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Lamadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Kutoka kushoto Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu
Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakiteta jambo, wakati wa ziara ya Mhe. Rais
Magufuli mkoani Simiyu, Septemba 08,
2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini , Bi. Bella Bird mara baada ya kufungua Mtandao
wa barabara za Lami za Mjini Bariadi ambazo zinajengwa kwa edha za mkopo kutoka
benki hiyo chini ya mradi wa ULGSP,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto,Mhe. Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya
Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ambaye alilifungua
jengo hilo Septemba 08, 2018 akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Baadhi ya viongozi na
wananchi wa mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa hadhara uliofanyika
Septemba 08, 2018 kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini , Bi. Bella Bird mara baada ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kufungua Mtandao
wa barabara za Lami za Mjini Bariadi ambazo zinajengwa kwa edha za mkopo kutoka
benki hiyo chini ya mradi wa ULGSP,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua
Mtandao wa barabara za Lami za Mjini Bariadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Septemba 08, 2018.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuweka
Jiwe la msingi, ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa KM 49.7 inayojengwa
kwa kiwango cha lami , Septemba O8, 2018 wakati akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment