Mkoa
wa Simiyu umezindua Mpango wa kupima maeneo ya wafugaji na wakulima kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya ndege nyuki (drones) lengo likiwa ni kuwawezesha
kuyatambua maeneo yao na kupewa hati miliki na baadaye kuyawekea miundombinu
muhimu ya ufugaji na kilimo na kuondokana na migogoro kati ya wakulima na
wafugaji.
Zoezi
hilo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka katika kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu na linatekelezwa
Chini ya Serikali kwa Kushirikiana na Taasisi Ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi
na Kijamii (ESRF).
Amesema
Mkoa huo ndiyo unaoongoza kwa kilimocha pamba nchini na ni miongoni mwa mikoa
yenye ng’ombe wengi nchini, kwa kuwa wakulima na wafugaji wanamiliki ardhi ni
vema maeneo yao yakapimwa wakapewa hati miliki na baadaye watalaam wa ardhi
wawasaidie kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Ameongeza
kuwa wafugaji wa mkoa wa Simiyu wamekuwa wakitozwa faini katika maeneo
mbalimbali hivyo ili kuondokana na kadhia hiyo maeneo yao yakipimwa na wakaweka
miundombinu muhimu kama vile mabwawa, visima, majosho na maeneo ya malisho
wataondokana na uchungaji wa mifugo na kwenda kwenye ufugaji wenye tija
“Tungehitaji
mpime mashamba yenu yakishapimwa mtapewa hati, watalaam wa halmashauri watawatengenezea
mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuwashauri namna sahihi ya uwekeaji wa
miundombinu kama majosho, mabwawa, visima ili muwe wafugaji wenye tija ambao
hamtapigwa faini wala kuibiwa ng’ombe” alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mfumo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na
Kijamii(ESRF) Bw. John Kajiba amesema upimaji kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki
utafanyika kwa urahisi na haraka zaidi na ikilinganishwa na upimaji
wa watu moja kwa kwa moja.
“Uzuri
wa kutumia ndege nyuki ni kwamba tutatumia muda mfupi sana kupima eneo kubwa
kwa wakati mmoja mfano, eneo ambalo
lngeweza kupimwa na watu wane kwa muda wa siku nne drone(ndege nyuki) inafanya
kwa muda wa siku moja” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa amesema upimaji wa maeneo ya wakulima na
wafugaji utawasaidia kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kupata
hati ziatazowasaidia kuchukua mikopo kwenye taasisi za kifedha na kufanya
shughuli za maendeleo kupitia maeneo yao
Nao wananchi wa Meatu wanasema
wameupokea mpango huo kwa mikono miwili kwa sababu watakuwa na uhakika wa umiliki wa
maeneo yao baaada ya kupewa hati ambazo pia wamesema zitawasaidia kukopa mitaji
ya kufuga na kulima kisasa na kwa tija.
“ Tumeupokea mradi huu kwa mikono
miwili maana tutakapopimiwa maeneo yetu tutakuwa tunakopesheka kwenye taasisi
za fedha, vile vile tutakuwa tumeondokana na migogoro kati ya wakulima na
wafugaji kwa sababu maeneo yetu yatakuwa na mipaka iliyo wazi na kila mmoja
atakuwa na hati ya kumili eneo lake” alisema John Mchagula mfugaji kutoka
Kijiji cha Ng’hoboko
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akijiandaa kurusha angani ndege nyuki (drone) inayotumika kupima ardhi, katika
uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo,
ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad
Kalemani(katikati mbele) na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu na Mkoa wa
Simiyu wakifurahia jambo wakati wa ziara ya Waziri huyo Septemba 20, 2018
wilayani Meatu.
Mtaalam
wa kutumia Ndege nyuki(drone) akiwaonesha viongozi na wananchi namna kifaa hcho
cha kisasa kinavyorushwa angani na kwenda kukusanya taarifa zinazotakiwa,
katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani
humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka/(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya
ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani, katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya
wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko
wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Baadhi
ya wananchi wa Wilaya ya Meatu wakiiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa
ambacho kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji
wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata
ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba
19, 2018.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu wakifauatilia burudani kutoka
katika Kikundi cha BASEKI (hawapopichani), katika uzinduzi wa zoezi la upimaji
wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata
ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba
19, 2018.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akiwasilisha taarifa ya zoezi la upimaji wa
maeneo ya wakulima na wafugaji wilayani humo, katika uzinduzi wa zoezi hilo
mkoani Simiyu, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Ng’hoboko, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya
wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani
Meatu, Septemba 19, 2018.
Baadhi
ya wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, wakimsikiliza mkuu wa
Mkoa huo wakati wa uzinduzi wa zoezi la
upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika
katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,
Septemba 19, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani
akizungumza na wananchi wa Kata ya
Ng’hoboko wakati wa uzinduzi wa
zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika
Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,
Septemba 19, 2018.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo akielezea utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa
uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani
humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Lumen Mathias
akielezea utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati
wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa
maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya
Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19,
2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe
akiwasalimia wananchi wa Kata ya
Ng’hoboko, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima
na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Kutoka
kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu, Mhe.
Pius Machungwa,(anaonekana nyuma) wakifurahia jambo, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa
maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko
wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Mtaalam wa Ndege nyuki akiwaeleza wakulima na
wafugaji na wananchi wengine juu ya namna kifaa hicho cha kisasa kinachotumika
katika zoezi la upimaji wa maeneo ya
wakulima na wafugaji, ambalo limezinduliwa katika Kata ya Ng’hoboko wilayani
Meatu, Septemba 19, 2018.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wa
Wilaya ya Meatu wakiiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa ambacho
kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo
ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya
Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19,
2018.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wa
Wilaya ya Meatu wakiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa ambacho
kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo
ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya
Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19,
2018.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Enock Yakobo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian
Manoza, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu, Mhe.
Pius Machungwa,(anaonekana nyuma) wakifurahia jambo, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa
maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani
Meatu, Septemba 19, 2018
Baadhi
ya viongozi wa Vijiji na kata za Wilaya ya Meatu, wakitambulishwa wakati wa
uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo
limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani humo Septemba 19, 2018.
Mtaalamu
wa Ndege nyuki akitoa maelezo ya namna kifaa hicho kinavyofanya kazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,
wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji,
ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Mtaalam
wa kutumia Ndege nyuki(drone) akiwaonesha viongozi na wananchi namna kifaa hcho
cha kisasa kinavyorushwa angani na kwenda kukusanya taarifa, katika uzinduzi wa
zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo
limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19, 2018.
Kikundi
cha Burudani kiitwacho BASEKI kutoka
Bariadi Mjini kikitoa burudani ya ngomba katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa
maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya
Ng’hoboko wilayani Meatu, Septemba 19,
2018.
0 comments:
Post a Comment