Tuesday, July 31, 2018

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA BURE MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KATIKA MAONESHO YA NANENANE SIMIYUMkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyaombukiza katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane  yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mhe. Mtaka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo Uwanja wa Nananenane kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema NHIF itatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza bure , hivyo hii ni fursa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa itawapunguzia gharama waitumie vizuri.

Wakati huo huoMtaka ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja na vikundi vikiwemo vyama vya ushirika zaidi ya 390 mkoani humo kujiunga nakuwa na kadi za Bima ya Afya,  ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma wakati wowote na kupunguza gharama za matibabu.

“Mini naamini ugonjwa hauna hodi hivyo nitoe wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa bima ya afya na sisi kwetu bima ya afya ni kipaumbele kwa kuwa tunahitaji mapinduzi ya kuchumi na kielimu tunayofanya ndani ya mkoa yaende sambamba na watu kupata kadi za bima ya afya, ili waone thamani ya Serikali kuwekeza katika sekta ya Afya” alisema.

“Katika sherehe za nanenane za mwaka 2018 niwaombe wananchi popote walipo watumie fursa hii ya kufikiwa na wenzetu wa Bima ya Afya,ili wawezeka kupata huduma za upimaji magonjwa yasiyoambukiza bure na kujiunga na bima ya afya “ alisisitiza.

Naye Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hilipoti Lello  amesema pamoja na kutoa huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure, huduma za usajili kwa ajili ya kupata kadi za bima ya afya  ya mtu mmoja , familia na vikundi zitatolewa ambazo zitalipiwa kulingana na aina ya kadi itakayotolewa .

“Tutatoa huduma za usajili na kutoa kadi za bima ya afya katika banda hili na mtu akishasajiliwa hapa kadi zitatolewa hapa hapa, tutakuwa na kadi za watoto toto afya kadi, tutakuwa na huduma za ktoa kadi kwa vikundi na kwa wakulima ni kwa wale walio kwenye vyama vya ushirika(AMCOS); mtu yeyote atakayepata kadi hii atapata matibabu Tanzania nzima kuanzia Zahanati hadi hospitali ya Rufaa” alifafanua.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, Bw. Shabani Kiduta ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza kujua afya zao na kupata tiba, ili Mapinduzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa mkoani humo yaweze kuwafikiwa wakiwa na afya njema.

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hilipoti Lello  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko huo, lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari jengo la maonesho la mkoa huo, lililojenhgwa katika Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo, ambalo lipo katika hatua za ukamilishaji.

Monday, July 30, 2018

KAMATI YA SIASA YA CCM SIMIYU YAELEZA KURIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Simiyu imeelezea kuridhishwa na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)  yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 Mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo, kutembelea Uwanja wa Nanenane Nyakabindi na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho ya Nanenane uwanjani hapo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, amesema kamati hiyo imeridhishwa na maandalizi hayo na kuwaomba wananchi kujitokeza ili kupata elimu kuhusiana na teknolojia ya kisasa ya kilimo na ufugaji.

“ Maandalizi yako vizuri, wananchi watakaofika hapa nina uhakika watafaidika na elimu ya ufugaji,  kilimo, matumizi ya zana bora za kilimo, wataona bidhaa mbalimbali za viwanda zinazolishwa  lakini pia watapata motisha wa kwenda kufanya vizuri kwenye maeneo yao” alisema Mhe. Enock

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT Meja Peter  Sebyiga amesema Jeshi hilo limejiaandaa vizuri katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi , hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujifunza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  maandalizi ya nane nane yamekamilika kwa asilimia 100, ambapo amebainisha kuwa Taasisi, Mashirika na makampuni yatakayoonesha teknolojia za kilimo, mifugo na uvuvi, wasindikaji na waongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi wameshafika kwa wingi.

Aidha, amewakaribisha wananchi wote hususani wa Mkoa wa Simiyu kufika katika maonesho hayo huku akibainisha kuwa kufika kwa wananchi katika maonesho hayo kutakidhi malengo ya mkoa  ya kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kupitia mafunzo watakayoyapata katika maonesho hayo.

Ameongeza kuwa kupitia Nanenane hii wananchi watapata fursa ya kuona kwa macho teknolojia mbalimbali zitakazowahamisha kutoka kwenye kile walichonacho katika maisha yao ya kila siku kuja kwenye teknolojia za kisasa.

“Matarajio yangu ni kwamba Nanenane hii itakuwa ni mahali sahihi kwa wananchi wa Simiyu kama wenyeji kubadilisha masha yao kutoka katika kufanya shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi kwa mazoea kwenda kuzifanya shughuli hizo kisasa zaidi” alisema Mtaka.

Kauli mbiu ya Nanenane mwaka 2018 ni “WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

MWISHO

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akiwaongoza  Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kutembelea mashamba darasa la JKT katika uwanja wa Nanenane Nyakabindi  wakati wa ziara yao ya kujionea maandalizi ya maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Luteni Joseph Lyakurya Meneja wa Mradi Sumaponics (kulia) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu  juu ya teknolojia ya ufugaji wa samaki kupitia matanki ambayo itaoneshwa kwa wananchi wakati wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu ya eneo la jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nayakabindi wakati wa ziara yao katika Uwanja huo kujione maandalizi ya Maonesho ya nanenane, yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa ya CCM Mkoani Simiyu walipotembelea Uwanja wa Nanenane kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia baadhi ya zana bora za Kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo itakayooneshwa na SUMA JKT katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia baadhi za viwanda  zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ( wtatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akisaini Kitabu cha wageni  katika Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu katika uwanja wa Nanenane Nyakabindi  kujionea maandalizi ya maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa ya CCM Mkoani Simiyu walipotembelea Uwanja wa Nanenane kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia)  akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto)  akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea jengo la maonesho ya nanenane la Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018  katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akiangalia maji ya kunywa ya UHURU PEAK yanayotengenezwa na JKT wakati wa wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Simiyu, katika Uwanja Nanenane Nyakabindi Bariadi kujionea maandalizi yaMaonesho ya nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu. 

Sunday, July 29, 2018

JKT YAJIPANGA KUFUNDISHA WANANCHI TEKNOLOJIA ZA UFUGAJI SAMAKI MAONESHO YA NANENANE SIMIYU


Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMA JKT),  Luteni Kanali Peter Lushika  amesema  JKT  limedhamiria kuwafundisha wananchi watakaofika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Bariadi  Mkoani Simiyu, teknolojia mbalimbali za ufugaji wa samaki ikiwa ni pamoja na ufugaji kwa kutumia mabwawa, matenki  na vizimba(ndani ya ziwa), ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa samaki na kuzuia uvuvi haramu.

Luteni Kanali Lushika ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya maandalizi ya Jeshi hilo katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018  na namna walivyojipanga kutoa elimu wa wananchi katika maeneo mbalimbali hususani katika kilimo, ufugaji na uvuvi.

“Tunajua wengi wanafahamu ufugaji wa samaki kwenye mabwawa, mwaka huu tunawaletea teknolojia ya ufugaji wa samaki kwenye matenki, walioko ziwani tutaonesha ufugaji wa samaki kwenye vizimba, teknojia hizi zitamsaidia mvuvi kuvua kuwa na uhakika wa upatiakanaji wasamaki, uhifadhi wa mazingira na kuondokana na uvuvi haramu” alisema Luteni Kanali Lushika.

Amesema JKT itawaeleza wananchi kuwa ufugaji wa samaki ni njia pekee ya kumwezesha mvuvi kupata samaki wakati wowote atakaohitaji hasa ufugaji  kwa kutumia  matenki.

Ameongeza kuwa pamoja na kuona teknolojia hizo  JKT itaandaa madarasa katika uwanja wa nanenane kwa ajili ya kufundisha wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali ili waweze kuona mbinu za kilimo, ufugaji na uvuvi bora na matumizi bora ya pembejeo.

Katika hatua nyingine Luteni Kanali Lushika amesema ili kufikia Tanzania ya Viwanda lina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata pamba ambacho kitachakata pamba kutoka ikiwa ghafi mpaka kufikia kwenye zao la mwisho ambalo ni nguo, hivyo kitaliongezea zaidi thamani zao la pamba.

Naye Luteni Joseph Lyakurya Meneja wa Mradi Sumaponics amesema teknojia ya kufuga samaki kwa kutumia matenki ni nzuri kwa kuwa inatumia eneo dogo la ardhi , maji kidogo lakini inakuwa na uwezo wa kuchukua samaki wengi ikilinganishwa na teknolojia ya mabwawa, hivyo akatoa wito watu wafike Uwanja wa Nanenane wajifunze.

Kwa upande wao Vijana wa JKT wamesema mafunzo waliyoyapata katika teknolojia mbalimbali yamewawezesha kupata maarifa ambayo yanaweza kuwasaidia kujiajiri wenyewe,  hivyo wakatoa wito kwa wananchi kwenda kuona teknolojia hizo.

“Kama mtaalam  wa masuala ya uvuvi niliyehitimu chuo cha uvuvi Kigoma, nikiwa JKT nimepata elimu ya vitendo zaidi ya kile nilichokipata chuoni, tukiwa hapa Nanenane Bariadi  tutatoa elimu kuhusiana na masuala ya uvuvi kwa kutumia vizimba, nawaomba wananchi waje wajifunze, maana ufugaji wa samaki nao una tija katika Tanzania ya Viwanda” alisema Almasi Idd Yusuph kikosi cha 822 Lwamkoma JKT.

“Miimi nikiwa JKT nimejifunza namna ya kuandaa bustani kutokana na mafunzo niliyopata naweza kutambua  udongo mzuri na ambao  si rafiki kwa kilimo cha bustani kama huu, kupitia maonesho haya wananchi wataelewa ni namna gani wanaweza wakaufanya udongo huu ukafaa na wakalima bustani” alisema Nasri Mataka Kijana wa JKT 822 KK Lwamkoma Mara.

Naye Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa SUMA JKT Meja Peter Sebyiga amesema JKT inatoa huduma na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kuzingatia ubora , muda unaokubalika na jamii kwa bei rafiki kwa wateja, hivyo akatoa wito kwa wananchi kufika kwenye maonesho ya Nanenane ili kuona bidhaa hizo kutoka kwenye viwanda, kilimo, mifugo na uvuvi.

Meja Sebyiga ametoa wito kwa Taasisi, Makampuni na watu binafsi kutumia samani zinazotengenezwa na Kiwanda cha Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi na nyumbani na kusisitiza kuona umuhimu wa Watanzania kupenda vya kwao.

MWISHO
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwaMkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)  Meja Jenerali Martin Busungu na  Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu ufugaji wa samaki kupitia teknolojia ya matanki yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya maandalizi maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.

Viongozi wa JKT na  mkoa wa Simiyu wakiangalia moja ya mabwawa ya samaki yaliyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Luteni Joseph Lyakurya Meneja wa Mradi Sumaponics  akiwaeleza  waandishi wa habari juu ya teknolojia ya ufugaji wa samaki kupitia matanki ambayo itaoneshwa kwa wananchi wakati wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Nasri Mataka Kijana wa JKT 822 KK Lwamkoma Mara akiwaeleza  waandishi wa habari juu ya bustani zilizolimwa kisasa ambazo zitaoneshwa kwa wananchi wakati wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa SUMA JKT Meja Peter Sebyiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya maandalizi maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.


Saturday, July 28, 2018

SIMIYU YAJIPANGA KUONGEZA UFAULU MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo umedhamiria kuongeza ufaulu na kufikia nafasi ya kwanza hadi ya tisa (single digit) katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018.


Mtaka ameyasema hayo katika kikao kati yake na Wakuu wa Shule za Sekondari mkoani Simiyu chenye lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

“Ni lazima twende kwenye ‘single digit’ matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, haiwezekani tufanye vizuri kidato cha sita tushindwe kufanya vizuri kidato cha nne, uthubutu tuliuonesha kuwa tunataka kuwa mkoa unaofanya vizuri kielimu tumaanishe, mwaka jana watu walikuwa wanahamisha watoto wao lakini mwaka huu wanaomba kuhamia” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewashauri wazazi kuwapunguzia kazi wanafunzi wa madarasa yote ya mitihani kwa shule za msingi na sekondari mkoani humo, ili kuwapa nafasi ya kupata muda mwingi wa kujisomea na kujiandaa na mitihani.

Wakati huo huo amewaagiza Wakuu wa Shule zote za Serikali za bweni mkoani Simiyu Sekondari kuongeza muda wa kuzima taa usiku kutoka saa nne usiku hadi saa sita kwa wanafunzi wa Kidato cha nne na sita, ili kutoa nafasi kwa  wanafunzi kupata muda mwingi wa kujisomea.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kulipokea  agizo lake la kuzitaka  Shule zote za Serikali za Sekondari kuongeza muda wa kuzima taa usiku kutoka saa nne usiku hadi saa sita kwa wanafunzi wa Kidato cha nne na sita ili waweze kupata muda mwingi wa kujisomea.

“Tunamshukuru Mkuu wa mkoa kwa kuagiza wanafunzi wasizimiwe taa hadi saa sita usiku, hapa shuleni kwetu ratiba ya kujisomea inaanza 11:00 hadi saa 12:00 asubuhi, baadae tunaanza vipindi, usiku tunaanza kusoma kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 6:00 usiku, hii inatupa muda zaidi wa kujisomea” alisema Erick Kamala mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi.

Katika hatua nyingine wanafunzi wameomba kambi za Kitaaluma kwa madarasa ya mtihani ziwe ajenda ya kudumu ya  Mkoa kwa kuwa wamekiri kambi zilizopita zimechangia mkoa huo kuwa na matokeo mazuri.

“ Tunaomba kambi ziendelee kuwepo kwa madarasa ya mitihani, mwezi wa sita tulipokuwa kambi mimi nilijifunza vitu vingi kwa walimu na wanafunzi wa shule za jirani tuliokuwa nao kambini, naomba tuwekewe tena kambi mwezi wa tisa kabla ya mtihani wa Taifa” alisema Faudhia Haruni mwanafunzi wa kidato cha nne  shule ya sekondari Bariadi.

“Kambi za kitaaluma zitatusaidia kubadilishana uzoefu na mbinu za kujibu mitihani na kukabiliana na (topic) mada zenye changamoto, tumeona wenzetu zimewasaidia sana nanina uhakika na sisi tutafanya vizuri zaidi ya mwaka huu” alisema William Charles  mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Bariadi.

Aidha, katika kikao cha wakuu wa shule na mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wakuu wa shule walieleza mikakati yao katika kuhakikisha mkoa huo unafanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne kama ilivyokuwa kwa Kidato cha Sita mwaka 2018, ikiwa ni pamoja na kuendeleza kambi hizo za kitaaluma.

“ Kambi za Kitaaluma zinawasaidia sana wanafunzi na ni suala ambalo wazazi wanalikubali, mwaka jana niliwatoa wanafunzi wangu kuwapeleka shule ya Itinje wengine Mwamalole lakini wazazi ndiyo waliochangia” alisema Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwamalole, Mwl.Marco Mwendamkono.

“ Sisi tumelipokea wazo lako Mkuu na hatuna muda wa kupoteza, kila siku saa 12:00 asubuhi, wanafunzi wanaanza kujisomea saa 12:30 asubuhi mwalimu anatoa swali la siku baaada ya hapo ni usafi, saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:50 wanakuwa darasani, baada ya kula saa 10:00 jioni tena wanaingia darasani hadi saa 12:00 jioni; baada ya chakula ni ibada na kuanzia saa 2:00 hadi saa 6:00 usiku kujisomea lakini wanaohitaji kuendelea baada ya hapo hawazuiwi” Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Konga Jackson.

Mkoa wa Simiyu katika matokeo ya mtihani waTaifa kidato cha sita mwaka 2018 umefanya vizuri na kushika nafasi ya 10 kifaifa kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017, huku kambi za kitaaluma zikitajwa na wadau mbalimbali kuwa miongoni mwa mikakati iliyoifikisha katika nafasi hiyo.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa wa Kidato cha nne na sita Shule ya Sekondari Bariadi mara baada ya kufunga kikao chake na wakuu wa shule kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati)  akizungumza na Wakuu wa Shule kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Erick Kamala mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkula akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Deus Toga akizungumza na katika kikao kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika shuleni hapo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya Itilima, akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.

Mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Faudhia Haruni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bariadi, akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Afisa Taaluma wa Mkoa, Mwl.Onesmo Simime akizungumza na wanafunzi katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo na wanafunzi wa Kidato cha Nne na Sita wa Shule ya Sekondari Bariadi, kilichofanyika shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne na Sita wakishangilia baada ya kupokea agizo la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali(za bweni) kuwataka wasiwazimie taa wanafunzi hadi saa sita usiku ii kuwaongezea muda wa kujisomea, katika kikao kilichfanyika shuleni hapo.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa wa Kidato cha nne na sita Shule ya Sekondari Bariadi mara baada ya kufunga kikao chake na wakuu wa shule kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwamalole, Mwl.Marco Mwendamkono. akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.

Friday, July 27, 2018

WAZIRI MKUCHIKA AAGIZA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA KUANZISHA VITUO VYA URASIMISHAJI NA UENDELEZAJI BIASHARA

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika ameziagiza  halmashauri zote nchini  kutenga maeneo ya uanzishwaji vituo vya urasimishaji biashara kwa wananchi ili waweze kuondokana na umasikini.


Agizo hilo limetolewa na kwa naiba yake na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga  katika uzinduzi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema MKURABITA ndio nyenzo muhimu ya kuwawezesha, kuibua na kuendeleza uwezo wa wananchi kuwa wawekezaji wa ndani wanaowajibika kutengeneza mtaji, soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi, hivyo ipo haja kwa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya vituo vya urasimishaji biashara  ili kuwasaidia wananchi.

“ Ni matumaini yangu kuwa vituo vya kurasimisha biashara vitatumika pia kutambua na kuzitumia fursa za uwekezaji ambazo zinatengenezwa na kuimarishwa, nitumie fursa hii kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa vituo hivi katika kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda vinavyomilikiwa na wananchi” alisema Kiswaga akisoma hotuba ya Waziri Mkuchika 
.
Aidha, amewahamasisha wafanyabiashara na wananchi wote mkoani Simiyu kutumia huduma zipatikanazo katika vituo vya kusajili na kuendeleza biashara zao, huku akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo kama mamalishe, wamachinga na waendesha bodaboda kutumia Kituo cha Bariadi, ili waweze kujiondoa katika mfumo usio rasmi na kuingia katika mfumo rasmi wa uchumi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Daniel Ole Njoolay ameiomba Serikali kutoa nyenzo za kutosha za kusukuma urasimishaji na uendelezaji wa biashara kukuza mitaji ya wafanyabiashara kwa kuwa hadi sasa utafiti unaonesha kuwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya biashara si rasmi.

Mwenyekiti Mstaafu wa mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) John Chiligati ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu hususani Bariadi kutumia hati miliki za kimila kama dhamana ya kupata mikopo ya kuendeleza kilimo, kuanzisha viwanda na biashara.

Mtendaji mkuu wa MKURABITA Seraphia Mgembe amewashukuru wote waliopata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara na kuahidi kuwafuatilia na kuhakikisha kuwa miaka ijayo waweze kufanikiwa kiuchumi.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara wameishukuru Serikali kwa mpango huo kuanzisha mradi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara, kupitia MKURABITA na kuomba waendelee kupewa mafunzo ili wawze kunufaika na biashara zao.

“Tunaomba tuendelee kupigwa msasa zaidi na zaidi ili tuweze kutunza mahesabu ya biashara zetu vizuri, tuweze kulipa kodi na kuendeleza biashara zetu katika mfumo ulio rasmi” alisema Mashaka Than mfanyabiashara kutoka Bariadi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichofunguliwa Julai 26, 2018 kitatoa huduma za leseni za biashara, usajili wa biashara, huduma za kibenki, TRA, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, wakala wa vipimo na huduma za kampuni binafsi ya GODTEC.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akikata utepe kuashiria ufunguzi  wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifungua kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Kapt.George Mkuchika Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na wafanyabiasha  katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  akisoma hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Kapt.George Mkuchika, katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018. 
Mwakilishi wa kampuni sita ya Mjini Bariadi ambazo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA , Bw. Elimringi Lyimo  akisoma risala katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi iliyofanyika Julai 26, 2018.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akiteta jambo na Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi iliyofanyika Julai 26, 2018.
Baadhi ya Maafisa Biashara wa Halmashauri 21 zinazounda Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga), wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka wa Makampuni sita ya Mjini Bariadi ambayo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA  wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye suti ya rangi ya bluu bahari mbele) akiwaongoza Viongozi na wajumbe wa Bodi ya MKURABITA kwenda kwenye ufunguzi wa  ufunguzi  wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, uliofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara kutoka wa Makampuni sita ya Mjini Bariadi ambayo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA , baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.


Baadhi ya Vijana waliopewa mafunzo na walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA  wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.

Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya MKURABITA  akizungumza na viongozi, katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.

 Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi na wafanyabiashara katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck  Humbe akiwa siliha taarifa ya Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara kilichofunguliwa rasmi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) akimpongeza Mwakilishi wa kampuni sita za Mjini Bariadi ambazo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA, Bw. Elimringi Lyimo  baada ya kusoma risala na kumkabidhi, katika hafla ya ufunguzi  wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe akizungumza na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Mhe. Angelina Kwinga akizungumza na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mtaalam kutoka Kampuni ya GOD TEC akitoa malezo juu ya manufaa ya Kituo cha Urasimishaji na uendelezaji biashara kwa viongozi mbalimbali waliofika katika hafla ya  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na wafanyabiasha  katika hafla ya  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na wafanyabiasha  katika hafla  ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na viogozi wengine wakifurahia ufunguzi wa kituo Kimoja cha Urasimishaji  na Uendelezaji  Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika  Julai 26, 2018.Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!