Mkurugenzi
wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu
ya vipando vilivyoandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika
Kitaifa Mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi
wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka walipotembelea
eneo hilo lililopo Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.
.................................................
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini
(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu
ameahidi kuwa Jeshi hilo litajenga Majengo
ya kudumu katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya
Ziwa Mashariki wa Nyakabindi Bariadi
Mkoani Simiyu, ili kuendelea kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na
wavuvi.
Meja Jenerali Busungu ameyasema hayo
wakati alipotembelea eneo la JKT lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi kwa lengo la kujionea maandalizi
hayo yanayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.
Busungu amesema baada ya Nanenane wataanza
ujenzi wa majengo ya kudumu ili wakulima, wafugaji na wavuvi wanufaike na teknolojia ya kilimo kwa muda
wote.
“Mkuu wa mkoa ametupa mkakati wao kuwa
kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na maonesho katika uwanja huu, tunaahidi
kujenga majengo ya kudumu hapa na maonesho yajayo miezi mitatu inayofuata
wananchi watarajie kupata vitu vizuri kutoka JKT, maana JKT ni kisima cha kila
kitu” alisema Meja Jenerali Busungu.
“ Katika maonesho haya watarajie kuona
teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi pia watarajie kuona bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na JKT zikiwemo bidhaa za kilimo, viwanda na kwa ndugu zangu
Wanyantuzu wataona mbuzi na kondoo wa maziwa na wataona kuwa si ng’ombe tu
wanaotoa maziwa” alisisitiza Meja Jenerali Busungu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka ameishukuru JKT kwa kazi kubwa ya
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane waliyoifanya, huku akibainisha kuwa uwepo wa
JKT utasaidia kuwabaadilisha vijana wa
Simiyu kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali.
“ Tunawashukuru sana JKT kwa kutuamini na
tunajua kuwepo JKT kutasadia kuwabadilisha vijana wa hapa kwa kuwa kuna vijana
wanamaliza darasa la saba au kidato cha nne hawana pa kushika na sisi tuna
vikundi vingi vya vijana , tuko tayari kuleta vikundi vyetu vya vijana kuja
kujifunza hapa” alisisitiza Mtaka.
Naye Mbunge wa Itilima amesema maonesho hayo yatawasaidia wananchi kupata elimu
itakayowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija ikiwemo ufugaji wa kisasa na
kilimo bora
MWISHO
Mkurugenzi wa Kilimo na
Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu Mabanda ya
miifugo yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane
yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji
Bariadi .
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin Busungu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu
kabla ya viongozi hao kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya
maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi
wa Mkoa huo kabla ya kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili
ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akizungumza na
viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kutembelea
eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo
katika Uwanja wa Nanenane uliopo Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiangalia moja ya mabwawa ya
samaki yaliyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya
Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa
mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin Busungu akisaini vitabu vya wageni vya Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza kutembelea eneo la jeshi hilo
lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani
humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja
wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri
ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao kati ya viongozi
wa Mkoa huo na viongozi wa JKT wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu katika eneo la
jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika
kitaifa mkoani humo Agosti 2018,
lililopo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Viongozi
wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiangalia
baadhi ya vipando(mashamba darasa)
vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya
Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa
mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakielekea kwenye mashamba
darasa na vipando vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya
maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Agosti 2018, katika Uwanja wa
Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin Busungu akisisitiza jambo katika kikao kati ya
viongozi wa Mkoa huo na viongozi wa JKT wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu katika eneo la
jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika
kitaifa mkoani humo Agosti 2018,
lililopo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakielekea kwenye mashamba
darasa na vipando vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya
maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Agosti 2018, katika Uwanja wa
Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin Busungu(wa nne kulia) na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ( wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa JKT, Kabla ya kwenda kuangalia mashamba darasa(vipando)
na maeneo mengine yaliyoandaliwa na JKT kwa ajili ya maonesho ya nanenane
yatakayofanyika Kitaifa Agosti 2018,
katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akisalimiana na Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali
Peter Lushika mara baada ya kuwasili eneo la JKT katika Uwanja wa maonesho ya
nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki ambayo yatafanyika Kitaifa Agosti 1-8, 2018
katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu(wa pili kulia) na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto), Mabanda ya miifugo yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi
Mkurugenzi wa Kilimo na
Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu ufugaji wa
samaki kupitia teknolojia ya matanki yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya
maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika
Halmashauri ya mji Bariadi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin akifurahia jambo katika kikao kati ya Viongozi
wa JKT na mkoa wa Simiyu kabla ya
kuelekea kwenye mashamba darasa na vipando vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga
Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Agosti
2018, katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
JKT na mkoa wa Simiyu wakiwa
wanafuatilia hoja mbalimbali katika
kikaokabla ya kutembelea mabanda ya mifugo, vipando na mabwawa
vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya
Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Agosti 2018, katika Uwanja wa Nanenane wa
kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiwa kwenye mashamba darasa
na vipando vilivyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho
ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Agosti 2018, katika Uwanja wa Nanenane wa
kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akisisitiza jambo katika kikao kati ya viongozi wa
Mkoa huo na viongozi wa JKT wakati wa ziara ya Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)
Meja Jenerali Martin Busungu katika eneo la jeshi hilo lililoandaliwa
kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo
Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa
Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya mji wa
Bariadi mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment