Naibu Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametoa
wito kwa akina mama wajawazito kuona
umuhimu wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma
za afya ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Dkt. Ndugulile
ameyasema hayo Julai 22,2018 katika nyakati tofauti wakati akiwa katika ziara
yake katika Wilaya ya Bariadi na Itilima mkoani Simiyu.
Amesema Serikali imefanya jitihada kubwa
katika kujenga vituo vya kutolea huduma za afya, majengo ya upasuaji na wodi za
wazazi hivyo ni vema wananchi wakatumia vituo hivyo ili idadi ya wanawake
wanaojifungulia majumbani ipungue na idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi pia
iendelee kupungua.
“Huduma tumewasogezea karibu mzitumie,
hususani wakina mama wajawazito, ujauzito siyo ugonjwa na wala mwanamke
hatakiwi kufariki sababu ya ujauzito, tuhakikishe wakina mama wanahudhuria
kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma, tunataka vifo vya akina
mama na watoto viwe historia” alisema Dk. Ndugulile.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akisoma taarifa ya Mkoa kwa Naibu waziri, amesema idadi ya akina mama wanaojifungulia katika
vituo vya kutolea huduma za Afya imeongezeka kutoka asilimia 54 mwaka 2016 na
kufikia asilimia 81 mwaka 2017, huku idadi ya vifo ikiongezeka kufikia vifo 48
kutokana na sababu mbalimbali.
Kutokana na takwimu kuonesha idadi ya
vifo kuongezeka Naibu Waziri Dkt. Ndugulile
amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa na idara ya Afya mkoa wa Simiyu kuangalia
chanzo cha ongezeko hilo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya vifo hivyo ili
kukomesha kabisa vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi.
Aidha, Dkt. Ndugulile ameuomba uongozi
wa mkoa wa Simiyu kufuatilia watu zaidi ya 10000 walioonekana kuacha kutumia
dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) ili kuweza kukabiliana na maambukizi
mapya.
Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile
ametoa wito kwa viongozi na jamii mkoani Simiyu kuendelea kupambana na mimba za
utotoni kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wote wa kike wanakwenda shule
na kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika kuwapa wanafunzi mimba kwani
mimba za utotoni pia zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya akina mama
wajawazito.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka amesema Serikali mkoani humo imeendelea kuchukua hatua kali dhidi ya
wanaume wanaobainika kuwapa mimba wanafunzi ambapo amebainisha kuwa hadi sasa
ni takribani watu 9 wameshachukuliwa hatua.
Kuhusu suala la VVU Mhe. Mtaka amesema
Serikali mkoani humo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwahimiza
wananchi kupima VVU huku akibainisha kuwa idara ya afya itafanya mpango wa
kuweka huduma za ushauri na kupima VVU pamoja na magonjwa yasiyoambukiza katika
Viwanja vya Maonesho ya Nanenane kwa kuwa itahusisha watu kutoka maeneo
mbalimbali.
Mhe. Dkt. Ndugulile akiwa wilaya
ya Bariadi na Itilima ametembelea Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD)la Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa, Jengo la Kituo cha Afya Ikindilo, Wodi ya Wazazi katika zahanati
ya Nangale na Migato ambapo amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi iliyofanyika
na thamani ya fedha iliyotumika
Akiwa katika wilaya ya Itilima
ameahidi kulifanyia kazi ombi la Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga, Mkuu wa
Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi na
Diwani wa Kata ya Migato Mhe. Mbuga Ntobi la kujenga kituo cha Afya katika Kata
ya Migato kwa kulipeleka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ili wannachi
waweze kusogezewa huduma jirani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akimjulia hali mgonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, wakati alipotembea hospitali hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akimjulia hali mgonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, wakati alipotembea hospitali hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile
akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kutembelea Jengo la
Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakati wa ziara yake mkoani humo
Julai 22, 2018.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Dkt. Mageda Kihulya (kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(kulia)
kuelekea katika wodi katika Hospitali Teule ya mkoa, wakati akiwa katika ziara
yake mkoani humo, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile akiweka
jiwe la msingi la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Migato Wilayani Itilima,
wakati wa ziara yake wilayanihumo mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(kushoto), akiwaonesha Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mabula nembo maalum zilizopo
katika dawa zote za Serikali, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu,Julai 22,
2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(kulia)
akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) na
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, mara baada ya kupokea taarifa
ya mkoa wakati wa ziara yake mkoani humo, Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(katikati) akitoka kuweka jiwe la msingi katika Wodi ya wazazi katika
Zahanati za Migato wakati wa ziara yake mkoani humo, Julai 22, 2018.
Mbunge
wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akisoma jiwe la msingi lililowekwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile( wapilikushoto) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani
Itilima mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile (kushoto) akimjulia hali mgonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa
Simiyu, wakati alipotembea hospitali hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
humo, Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile akiangali mfumo wa GoTHoMIS unavyofanya kazi katika katika Hospitali
Teule ya Mkoa wa Simiyu, wakati alipotembea hospitali hiyo akiwa katika ziara
ya kikazi mkoani humo, Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(kushoto) na Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga wakiteta jambo
wakatika wa ziara ya Naibu Waziri huyo Wilayani Itilima, Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili
Mkoani humo Julai 22, 2018.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akimuonesha Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(wa pili
kushoto) eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, wakati alipotembelea na
kukagua Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) la hospitali hiyo, Julai 22,
2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa
Simiyu na wataalam kutoka Wizara ya Afya mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo
la wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, wakati wa ziara yake
Julai 22, 2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu mara baada ya kuwasili wilayani Itilima kwa ajili
ya ziara ya kikazi wilayani humo, Julai 22, 2018.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt.
Faustine Ndugulile(kulia) mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya
ziara yake ya siku mbili Mkoani humo Julai 22, 2018.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(kulia) mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi na kupokea taarifa ya
Mkoa, wakati wa ziarayake Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(wa tatu
kushoto) na viongozi wengine wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu
wakishangilia baada ya jiwe la msingi la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya
Migato Wilayani Itilima kuwekwa na Naibu waziri huyo, wakati wa ziara yake
wilayani humo mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(kulia)
akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga kwa zawadi waliyompa mara baada ya kumaliza
ziara wilayani humo mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile(kulia)
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato, wakati wa ziara yake Julai 22,
2018 mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(kushoto) akikagua Jengo la Wagonjwa wa Njela Hopsitali ya Rufaa ya
Mkoa wakati wa ziara yake Julai 22, 2018 mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi
mara baada ya kumaliza ziara wilayani humo mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile(katikati) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Itilima wakati
alipoanza ziara yake wilayani humo Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile akitoa
maelekezo wakati akitembelea na kukagua jengo la Kituo cha Afya cha Ikindilo
wilayani Itilima wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Julai 22, 2018.
Katibu Tawala wa mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile katika
kukagua Jengo la Wagonjwa wa Nje wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Julai 22,
2018.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine
Ndugulile (kulia) akimsikiliza Mganga
Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Matoke Muyenjwa, mara baada ya kukagua
Jengo la Wagonjwa wa Nje wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Julai 22, 2018..
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile (kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha maabara katika Hopsitali Teule ya Mkoa, Bibi.
Elizabeth Mgongo, alipotembelea hospitali hiyo, wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile (kulia)
akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuwa wanauguza ndugu zao waliolazwa
katika hospitali Teule ya mkoa kujiridha na hali ya utoaji huduma,
alipotembelea hospitali hiyo, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Julai 22,
2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile
akisalimiana na Afisa Tawala wa Wilaya ya Itilima, Bw. Dinno Mwigune, mara
baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile
akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, mhe. Daudi
Nyalamu, mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi
Julai 22, 2018.
Wananchi wa Kijiji cha
Ikindilo wilayani Itilima wakimsikilia Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani)
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile
akifurahia pamoja na wananchi wa kijiji cha Nangale kata ya Ndolelezi baada ya
kuweka jiwe la msingi la Wodi ya wazazi ya Zahanati ya Nangale wakati wa ziara
yake wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
Mbunge
wa Jimbo la Itilima, mhe. Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ikindilo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile, wakati wa ziara yake wilaya ya
Itilima Mkoani Simiyu, Julai 22, 2018.
0 comments:
Post a Comment