Monday, July 30, 2018

KAMATI YA SIASA YA CCM SIMIYU YAELEZA KURIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Simiyu imeelezea kuridhishwa na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)  yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 Mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo, kutembelea Uwanja wa Nanenane Nyakabindi na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho ya Nanenane uwanjani hapo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, amesema kamati hiyo imeridhishwa na maandalizi hayo na kuwaomba wananchi kujitokeza ili kupata elimu kuhusiana na teknolojia ya kisasa ya kilimo na ufugaji.

“ Maandalizi yako vizuri, wananchi watakaofika hapa nina uhakika watafaidika na elimu ya ufugaji,  kilimo, matumizi ya zana bora za kilimo, wataona bidhaa mbalimbali za viwanda zinazolishwa  lakini pia watapata motisha wa kwenda kufanya vizuri kwenye maeneo yao” alisema Mhe. Enock

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT Meja Peter  Sebyiga amesema Jeshi hilo limejiaandaa vizuri katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi , hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujifunza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  maandalizi ya nane nane yamekamilika kwa asilimia 100, ambapo amebainisha kuwa Taasisi, Mashirika na makampuni yatakayoonesha teknolojia za kilimo, mifugo na uvuvi, wasindikaji na waongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi wameshafika kwa wingi.

Aidha, amewakaribisha wananchi wote hususani wa Mkoa wa Simiyu kufika katika maonesho hayo huku akibainisha kuwa kufika kwa wananchi katika maonesho hayo kutakidhi malengo ya mkoa  ya kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kupitia mafunzo watakayoyapata katika maonesho hayo.

Ameongeza kuwa kupitia Nanenane hii wananchi watapata fursa ya kuona kwa macho teknolojia mbalimbali zitakazowahamisha kutoka kwenye kile walichonacho katika maisha yao ya kila siku kuja kwenye teknolojia za kisasa.

“Matarajio yangu ni kwamba Nanenane hii itakuwa ni mahali sahihi kwa wananchi wa Simiyu kama wenyeji kubadilisha masha yao kutoka katika kufanya shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi kwa mazoea kwenda kuzifanya shughuli hizo kisasa zaidi” alisema Mtaka.

Kauli mbiu ya Nanenane mwaka 2018 ni “WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

MWISHO

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akiwaongoza  Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kutembelea mashamba darasa la JKT katika uwanja wa Nanenane Nyakabindi  wakati wa ziara yao ya kujionea maandalizi ya maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Luteni Joseph Lyakurya Meneja wa Mradi Sumaponics (kulia) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu  juu ya teknolojia ya ufugaji wa samaki kupitia matanki ambayo itaoneshwa kwa wananchi wakati wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Naibu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu ya eneo la jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nayakabindi wakati wa ziara yao katika Uwanja huo kujione maandalizi ya Maonesho ya nanenane, yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa ya CCM Mkoani Simiyu walipotembelea Uwanja wa Nanenane kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia baadhi ya zana bora za Kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo itakayooneshwa na SUMA JKT katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia baadhi za viwanda  zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ( wtatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akisaini Kitabu cha wageni  katika Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu katika uwanja wa Nanenane Nyakabindi  kujionea maandalizi ya maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa ya CCM Mkoani Simiyu walipotembelea Uwanja wa Nanenane kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia)  akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa SUMA  JKT kuhusu zana bora za kilimo zitakazooneshwa na SUMA JKT  katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane)Kitaifa katika Uwanja wa Nyakabindi  Mkoani humo, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto)  akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea jengo la maonesho ya nanenane la Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018  katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akiangalia maji ya kunywa ya UHURU PEAK yanayotengenezwa na JKT wakati wa wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Simiyu, katika Uwanja Nanenane Nyakabindi Bariadi kujionea maandalizi yaMaonesho ya nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu. 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!