Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika ameziagiza halmashauri
zote nchini kutenga maeneo ya uanzishwaji vituo vya urasimishaji biashara
kwa wananchi ili waweze kuondokana na umasikini.
Agizo hilo limetolewa na kwa naiba yake na Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi Festo Kiswaga katika uzinduzi wa kituo kimoja cha urasimishaji
na uendelezaji biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Amesema MKURABITA ndio nyenzo muhimu ya kuwawezesha, kuibua na kuendeleza
uwezo wa wananchi kuwa wawekezaji wa ndani wanaowajibika kutengeneza mtaji,
soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi, hivyo ipo haja
kwa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya vituo vya urasimishaji biashara ili kuwasaidia wananchi.
“ Ni matumaini yangu kuwa vituo vya kurasimisha biashara vitatumika pia
kutambua na kuzitumia fursa za uwekezaji ambazo zinatengenezwa na kuimarishwa,
nitumie fursa hii kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya
uanzishwaji wa vituo hivi katika kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda
vinavyomilikiwa na wananchi” alisema Kiswaga akisoma hotuba ya Waziri Mkuchika
.
Aidha, amewahamasisha wafanyabiashara na wananchi wote mkoani Simiyu
kutumia huduma zipatikanazo katika vituo vya kusajili na kuendeleza biashara
zao, huku akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo kama mamalishe, wamachinga na
waendesha bodaboda kutumia Kituo cha Bariadi, ili waweze kujiondoa katika mfumo
usio rasmi na kuingia katika mfumo rasmi wa uchumi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Daniel Ole Njoolay ameiomba
Serikali kutoa nyenzo za kutosha za kusukuma urasimishaji na uendelezaji wa
biashara kukuza mitaji ya wafanyabiashara kwa kuwa hadi sasa utafiti unaonesha
kuwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya biashara si rasmi.
Mwenyekiti Mstaafu wa mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA) John Chiligati ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu
hususani Bariadi kutumia hati miliki za kimila kama dhamana ya kupata mikopo ya
kuendeleza kilimo, kuanzisha viwanda na biashara.
Mtendaji mkuu wa MKURABITA Seraphia
Mgembe amewashukuru wote
waliopata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara na kuahidi
kuwafuatilia na kuhakikisha kuwa miaka ijayo waweze kufanikiwa kiuchumi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara
wameishukuru Serikali kwa mpango huo kuanzisha mradi wa kituo kimoja cha urasimishaji
na uendelezaji biashara, kupitia MKURABITA na kuomba waendelee kupewa mafunzo
ili wawze kunufaika na biashara zao.
“Tunaomba tuendelee kupigwa msasa zaidi na zaidi ili tuweze kutunza
mahesabu ya biashara zetu vizuri, tuweze kulipa kodi na kuendeleza biashara
zetu katika mfumo ulio rasmi” alisema Mashaka Than mfanyabiashara kutoka
Bariadi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck
Humbe Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichofunguliwa
Julai 26, 2018 kitatoa huduma za leseni za biashara, usajili wa biashara,
huduma za kibenki, TRA, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, wakala wa vipimo na huduma
za kampuni binafsi ya GODTEC.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
ambaye alifungua kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Kapt.George Mkuchika Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya
MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na
wafanyabiasha katika hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akisoma
hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt.George Mkuchika, katika
hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mwakilishi wa kampuni
sita ya Mjini Bariadi ambazo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na
uendelezaji biashara kutoka MKURABITA , Bw. Elimringi Lyimo akisoma risala katika hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi
iliyofanyika Julai 26, 2018.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akiteta jambo na Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia
Mgembe katika hafla ufunguzi wa wa Kituo
Kimoja cha Urasimishaji na
Uendelezaji Biashara katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi iliyofanyika Julai 26, 2018.
Baadhi ya Maafisa
Biashara wa Halmashauri 21 zinazounda Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na
Shinyanga), wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Baadhi ya
wafanyabiashara kutoka wa Makampuni sita ya Mjini Bariadi ambayo watu wake
walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa
hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye suti ya rangi ya bluu bahari mbele)
akiwaongoza Viongozi na wajumbe wa Bodi ya MKURABITA kwenda kwenye ufunguzi
wa ufunguzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, uliofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tano kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na wafanyabiashara kutoka wa Makampuni sita ya Mjini Bariadi ambayo watu
wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA
, baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Baadhi ya Vijana waliopewa mafunzo na walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mwenyekiti Mstaafu wa
Bodi ya MKURABITA akizungumza na
viongozi, katika hafla ufunguzi wa wa
Kituo Kimoja cha Urasimishaji na
Uendelezaji Biashara katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai
26, 2018.
Katibu Tawala wa
Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi na wafanyabiashara katika
hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck
Humbe akiwa siliha taarifa ya Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kilichofunguliwa rasmi katika
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) akimpongeza Mwakilishi wa kampuni sita za
Mjini Bariadi ambazo watu wake walipata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji
biashara kutoka MKURABITA, Bw. Elimringi Lyimo
baada ya kusoma risala na kumkabidhi, katika hafla ya ufunguzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi
iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mratibu wa MKURABITA
Bi. Seraphia Mgembe akizungumza na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara
katika hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja
cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Urambo, Mhe. Angelina Kwinga akizungumza na viongozi mbalimbali na
wafanyabiashara katika hafla ufunguzi wa
wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na
Uendelezaji Biashara katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai
26, 2018.
Mtaalam kutoka Kampuni
ya GOD TEC akitoa malezo juu ya manufaa ya Kituo cha Urasimishaji na
uendelezaji biashara kwa viongozi mbalimbali waliofika katika hafla ya ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya
MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na
wafanyabiasha katika hafla ya ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya
MKURABITA Mhe. Daniel Ole Njoolay akizungumza viongozi mbalimbali na
wafanyabiasha katika hafla ufunguzi wa wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, iliyofanyika Julai 26, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na viogozi wengine wakifurahia ufunguzi wa kituo
Kimoja cha Urasimishaji na
Uendelezaji Biashara katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, iliyofanyika Julai
26, 2018.
0 comments:
Post a Comment