Wananchi na
viongozi kutoka katika vijiji saba vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori (WMA) ya Makao hususani Kijiji cha Makao wilayani Meatu Mkoani
Simiyu, wamekiri kuwa uhusiano kati yao na Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD, ambaye
amewekeza katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao kwa
ajili ya kuendeleza uhifadhi na uwindaji wa kitalii umeimarika tofauti na
awali.
Hayo yalibainishwa
na wananchi hao wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu
ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa
wa Simiyu, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Enock Yakobo katika baadhi ya
miradi na maeneo ya uwekezaji ya mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji
cha Makao.
Wamesema
awali kulikuwa na mgogoro ambao ulisababisha uhusiano kati wananchi na
mwekezaji kuvunjika, lakini baadaye
Serikali ya Wilaya na Mkoa ziliingilia kati changamoto zote zilijadiliwa
na mapungufu yote yaliyobainika yakafanyiwa kazi, ili pande zote ziweze
kunufaika na uwekezaji huo.
“
Uhusiano kati ya Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD sasa hivi uko vizuri, migogoro
iliyokuwepo haipo tena, sasa hivi tunaendelea kuelimishana sisi kwa sisi, ili
tusiingize mifugo kwenye eneo lilohifadhiwa kwa utalii maana linatusaidia na
tunaendelea kuhamasishana kupambana na ujangili” alisema Andrea Yakobo Mkazi wa
Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
“Uhusiano
uko vizuri, zamani wakati kuna mgogoro tulikuwa tunashuhudia mizoga ya tembo
lakini sasa hivi baada ya mwekezaji kushirikiana na wananchi kila mmoja wetu
amekuwa mlinzi wa wanyama walio kwenye Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA, ajira
watoto wetu wanapata kama tulivyokubaliana, wantusaidie kwenye elimu, afya na
mengine” alisema Amosi Sitta kutoka Kijiji cha Makao.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Makao ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwangudo, Mhe. Anthony
Philipo amesema kijiji cha Makao kimenufaika sana kutokana na uwepo wa
mwekezaji huyo, hivyo ni vema masuala yote yanayoashiria kuleta migogoro yakadhibitiwa
ili wananchi waweze kunufaika na uwekezaji huo.
Naye
Mzee maarufu kutoka Kijiji cha makao Bw. Lucas Malyalya amesema pamoja na uhusiano
kati ya mwekezaji na wananchi kuwa mzuri wananchi wanaomba suala la mgogoro wa
mpaka katika yaWilaya ya Meatu na Wilaya yaNgorongoro(Arusha) katika Kijiji cha
Makao lifanyiwe kazi, jambo ambalo liliahidiwa kufanyiwa kazi na Serikali.
Naye
Afisa Uhusiano wa MWIBA Holdings Ltd, Bw. Alfred Mwakivike amesema Kampuni hiyo
itaendelea kufanya mambo yanayogusa maendeleo ya jamii ikiwemo afya na elimu
ambapo amebainisha kuwa kuanzia mwaka huu wameanza kuwasaidia watoto wenye
vichwa vikubwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Sereani iliyoko jijini
Arusha.
Aidha,
amesema wameanza kuunda vikundi vya vijana kutoka katika Vijini vinavyoizungua
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao na Rachi ya MWIBA na kuvisajili kwa
ajili ya kuwaanzishia miradi ya kuwaingizia kipato ili wasijiingize katika
vitendo vya ujangili, badala yake wafikirie pia kuhamasishana ili kuunda
vikundi vinavotekeleza miradi itakayosaidia uhifadhi.
Mkurugenzi
wa MWIBA HOLDINGS LTD Bw. Abdulkadiri Mohamed ameushukuru uongozi wa Mkoa wa
Simiyu kwa kusaidia kumaliza mgogoro kati ya mwekezaji na wananchi na akaomba
pia uweze kushirikiana nao katika kutokomeza ujangili na kumaliza suala la
mgogoro wa Ardhi na Wilaya ya Ngorongoro ili waweze kufikia lengo la kuendeleza
utalii na uhifadhi kama walivyokusudia.
Akizungumza
na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili cha MWIBA HOLDINGS LTD Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amewaka askari hao kufanya kazi zao kwa weledi,
kuzingatia sheriana taratibu na kuepuka vitendo vyovyote vya unyanyasaji wa
wananchi.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo aliwataka MWIBA HOLDINGS LTD kuajiri
watumishi waadilifu pia akawaomba viongozi wote wahamasishe na kutoa elimu kwa
wananchi kufuata sheria na taratibu ikiwa ni pamoja na kutoingiza mifugo katika
eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA
MWISHO
Mkurugenzi wa Mwiba
Holdings Ltd Bw. Abdulkadiri Mohamed akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati yaUlinzi
na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu
wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha
Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoawa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akikagua kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi ya
Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (kushoto akizungumza jambo na Mkurugenzi wa MWIBA
HOLDINGS LTD Bw. Abdulkadiri Mohamed wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu
katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao,
Mhe.Anthony Philipo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu
katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi
ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga akizungumza jambo wakati
wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati
ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori ya
MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akiomba maelezo ya baadhi ya vitu katika
moja ya hoteli za Kitalii za Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD, wakati wa ziara ya wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha
Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa
wa Simiyu, Viongozi wa MWIBA HOLDINGS LTD wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya
Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Viongozi na Watumishi wa MWIBA HOLDINGS LTD
wakati wa ziara ya kamati hizo katika Hifadhi
ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na mmoja wa watumishi wa MWIBA HOLDINGS
LTD wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu
na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori
ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwibuli akizungumza jambo katika ziara ya wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha
Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha
Makao wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Mariam Manyangu akisisitiza jambo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi
ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kulia) akizungumza na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili katika
Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa
ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa
ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Lumen Mathias akisisitiza jambo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi
ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
0 comments:
Post a Comment