Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema mkoa huo umedhamiria kuongeza ufaulu na kufikia nafasi ya kwanza
hadi ya tisa (single digit) katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka
2018.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao kati
yake na Wakuu wa Shule za Sekondari mkoani Simiyu chenye lengo la kuweka
mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne baada ya kufanya vizuri katika
matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.
“Ni lazima twende kwenye ‘single digit’ matokeo
ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, haiwezekani tufanye vizuri kidato cha
sita tushindwe kufanya vizuri kidato cha nne, uthubutu tuliuonesha kuwa tunataka
kuwa mkoa unaofanya vizuri kielimu tumaanishe, mwaka jana watu walikuwa
wanahamisha watoto wao lakini mwaka huu wanaomba kuhamia” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewashauri wazazi
kuwapunguzia kazi wanafunzi wa madarasa yote ya mitihani kwa shule za msingi na
sekondari mkoani humo, ili kuwapa nafasi ya kupata muda mwingi wa kujisomea na
kujiandaa na mitihani.
Wakati huo huo amewaagiza Wakuu wa Shule
zote za Serikali za bweni mkoani Simiyu Sekondari kuongeza muda wa kuzima taa
usiku kutoka saa nne usiku hadi saa sita kwa wanafunzi wa Kidato cha nne na
sita, ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kupata
muda mwingi wa kujisomea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi
wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kulipokea agizo lake la kuzitaka Shule zote za Serikali za Sekondari kuongeza
muda wa kuzima taa usiku kutoka saa nne usiku hadi saa sita kwa wanafunzi wa
Kidato cha nne na sita ili waweze kupata muda mwingi wa kujisomea.
“Tunamshukuru Mkuu wa mkoa kwa kuagiza wanafunzi wasizimiwe taa hadi saa
sita usiku, hapa shuleni kwetu ratiba ya kujisomea inaanza 11:00 hadi saa 12:00
asubuhi, baadae tunaanza vipindi, usiku tunaanza kusoma kuanzia saa 2:00 usiku
hadi saa 6:00 usiku, hii inatupa muda zaidi wa kujisomea” alisema Erick Kamala
mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi.
Katika hatua nyingine wanafunzi wameomba kambi za Kitaaluma kwa madarasa ya
mtihani ziwe ajenda ya kudumu ya Mkoa kwa
kuwa wamekiri kambi zilizopita zimechangia mkoa huo kuwa na matokeo mazuri.
“ Tunaomba kambi ziendelee kuwepo kwa madarasa ya mitihani, mwezi wa sita
tulipokuwa kambi mimi nilijifunza vitu vingi kwa walimu na wanafunzi wa shule
za jirani tuliokuwa nao kambini, naomba tuwekewe tena kambi mwezi wa tisa kabla
ya mtihani wa Taifa” alisema Faudhia Haruni mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Bariadi.
“Kambi za kitaaluma zitatusaidia kubadilishana uzoefu na mbinu za kujibu mitihani
na kukabiliana na (topic) mada zenye changamoto, tumeona wenzetu zimewasaidia
sana nanina uhakika na sisi tutafanya vizuri zaidi ya mwaka huu” alisema
William Charles mwanafunzi wa kidato cha
sita shule ya sekondari Bariadi.
Aidha, katika kikao cha wakuu wa shule na mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wakuu wa
shule walieleza mikakati yao katika kuhakikisha mkoa huo unafanya vizuri katika
Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne kama ilivyokuwa kwa Kidato cha Sita mwaka
2018, ikiwa ni pamoja na kuendeleza kambi hizo za kitaaluma.
“ Kambi za Kitaaluma zinawasaidia sana wanafunzi na ni suala ambalo wazazi wanalikubali,
mwaka jana niliwatoa wanafunzi wangu kuwapeleka shule ya Itinje wengine
Mwamalole lakini wazazi ndiyo waliochangia” alisema Mkuu wa Shule ya Sekondari
Mwamalole, Mwl.Marco Mwendamkono.
“ Sisi tumelipokea wazo lako Mkuu na hatuna muda wa kupoteza, kila siku saa
12:00 asubuhi, wanafunzi wanaanza kujisomea saa 12:30 asubuhi mwalimu anatoa
swali la siku baaada ya hapo ni usafi, saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:50 wanakuwa
darasani, baada ya kula saa 10:00 jioni tena wanaingia darasani hadi saa 12:00
jioni; baada ya chakula ni ibada na kuanzia saa 2:00 hadi saa 6:00 usiku
kujisomea lakini wanaohitaji kuendelea baada ya hapo hawazuiwi” Mkuu wa Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Konga Jackson.
Mkoa wa Simiyu katika matokeo ya mtihani waTaifa kidato cha sita mwaka 2018
umefanya vizuri na kushika nafasi ya 10 kifaifa kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017,
huku kambi za kitaaluma zikitajwa na wadau mbalimbali kuwa miongoni mwa
mikakati iliyoifikisha katika nafasi hiyo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa wa Kidato cha nne na sita Shule
ya Sekondari Bariadi mara baada ya kufunga kikao chake na wakuu wa shule
kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya
ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akizungumza
na Wakuu wa Shule kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Erick Kamala mwanafunzi wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi
akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Mkula akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa
lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha
nne mwaka 2018.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Deus Toga akizungumza na katika kikao kati
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika shuleni hapo Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Shule ya
Itilima, akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa
lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha
nne mwaka 2018.
Mwanafunzi
wa Kidato cha Sita, Shule ya
Sekondari Bariadi akichangia hoja katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo
pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Faudhia
Haruni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bariadi, akichangia hoja
katika kikao katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Afisa
Taaluma wa Mkoa, Mwl.Onesmo Simime akizungumza na wanafunzi katika kikao cha
Mkuu wa Mkoa huo na wanafunzi wa Kidato cha Nne na Sita wa Shule ya Sekondari
Bariadi, kilichofanyika shuleni hapo.
Baadhi
ya wanafunzi wa kidato cha nne na Sita wakishangilia baada ya kupokea agizo la
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa Wakuu wa Shule za Sekondari za
Serikali(za bweni) kuwataka wasiwazimie taa wanafunzi hadi saa sita usiku ii
kuwaongezea muda wa kujisomea, katika kikao kilichfanyika shuleni hapo.
Mwanafunzi
wa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari Bariadi akichangia hoja katika kikao
katika wanafunzi wa shule hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa wa Kidato cha nne na sita Shule
ya Sekondari Bariadi mara baada ya kufunga kikao chake na wakuu wa shule
kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya
ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwamalole, Mwl.Marco Mwendamkono. akichangia hoja katika kikao kati ya Wakuu wa Shule na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) kilichofanyika Mjini Bariadi, kwa
lengo la kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha
nne mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment