Wednesday, July 11, 2018

SIMIYU YAFANIKIWA KUSAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO 337,662

Mkoa wa Simiyu umeweza kusajili jumla ya watoto 337,662 kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita sawa na asilimia 91.7 ya watoto waliotarajiwa kusajiliwa, chini ya mpango wa Usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Katiba na Sheria (RITA), Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau wengine UNICEF na DFATD.


Akizungumza katika  kikao cha Tathmini  kuhusu utekelezaji wa mpango wa usajili wa vizazi kwa watoto wa umri  chini ya miaka mitano, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.  Emmy Hudson alisema kupitia mpango huo Mkoa wa Simiyu umeweza kutoka katika asilimia 5 na kufikia asilimia 91.7 ya usajili na utoaji vyeti.

“Kwa mujibu wa takwimu mpaka sasa Mpango huu katika Mkoa wa Simiyu umeweza kusajili watoto 337,662 ambao ni sawa na asilimia 91.7 ya watoto wote waliotarajiwa kusajiliwa...hii ni dhahiri kuwa ni mafanikio makubwa kwani kabla ya kuanza kwa mpango kulikuwa na asilimia 5 tu ya watoto waliokuwa wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa”...Alisema

Aidha, Hudson alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yaliyopatikana  ni lazima kila Halmashauri inatakiwa kuendeleza mpango huo  kwani bila hivyo watakuwa wanarudisha  nyuma jitihada za serikali la kufikia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw.  Jumanne Sagini  alisema kuwa pamoja na kufikia asilimia hiyo 91 ,ni vema sasa halmashauri zikajitahidikufikisha lengo la usajili kwa asilimia 100.

Sagini pia alizitaka Halmashauri zote ziweke mipango mikakati ya namna ya kuendeleza usajili huo wa watoto chini ya miaka mitano na kuweka katika mipango ya bajeti kwani hawataweza kufadhiliwa miaka yote.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuwa zoezi la usajili katika wilaya yake lilienda na kuendeshwa vizuri ingawa kulikuwa na changamoto kadhaa ambazo kadri zoezi litakavyoendelea watajitahidi kuzitatua.

Kiswaga ameeleza kuwa kupitia matokeo hayo ya mpango wa usajili ndani ya miezi mitatu utasaidia kubadilisha maendeleo na kuchochea uchumi wa Mkoa  na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza aliwapongeza RITA kwa kusimamia mpango huo ambao utasaidia kuboresha na kupanga mikakati ya Serikali hususani katika sekta ya afya kwa kuwezesha upatikanaji wa takwimu za watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“naamini kuwa kwa sasa tutaweza kupanga mipango yetu vema kwani mwanzoni tulikuwa tunapata shida sana  wakati wa kupanga mipango ya afya, hususani katika ugawaji wa chanjo kwa watoto, kutokana na kukosa takwimu sahihi za watoto...”Alisema Manoza.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu walikusudia kuwafikia watoto 68,000  lakini waliofikiwa ni 63,000 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua ambayo ilisababisha baadhi ya maeneo kutokufikika, huku akibainisha mkakati wa kuendeleza usajili kupitia Ofisi za Vijiji.

Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano ulianza kutekelezwa Mwezi Machi 14 mwaka huu mkoani Simiyu,  ambapo kwa mikoa ya Mara na Simiyu, ulizinduliwa rasmi na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Mjini Musoma Mkoani Mara Machi 20, 2018.
MWISHO


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.  Emmy Hudson akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango huo mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa huo pamoja na viongozi na watendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA),juu ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani humo, kilichofanyika jana mjini Bariadi.Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi na watendaji katika mkoawa Simiyu wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani humo, kilichofanyika jana mjini Bariadi.Meneja Uhusiano na Masoko wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) akifafanua jambokatika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (katikati walioketi),  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) Bi.  Emmy Hudson (kulia) ,Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo baada ya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani humo, kilichofanyika jana mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (katikati walioketi) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) Bi.  Emmy Hudson (kulia) ,Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Idara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, baada ya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani humo, kilichofanyika jana mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakiteta jambo katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Mwakilishi kutoka Shirika la UNICEF ambalo ni moja ya wafadhili wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango huo mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (wa pili kushoto walioketi) (wa pili kushoto walioketi), , Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.  Emmy Hudson (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kushoto), na mwakilishi kutoka UNICEF,  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (wa pili kushoto walioketi), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.  Emmy Hudson (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kushoto), na mwakilishi kutoka UNICEF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa Maendeleo ya Jamii  na Waganga Wakuu wa Wilaya, baada ya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (wa pili kushoto walioketi), , Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi.  Emmy Hudson (wa pilikulia walioketi)Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kushoto), na mwakilishi kutoka UNICEF  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari na Afisa Habari Mkoa(wa pili kulia waliosimama) , baada ya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu, kilichofanyika jana mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!