Serikali imetenga kiasi cha
shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu Julai 12, 2018, mara baada
ya kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu,
ambapo ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo.
Waziri Ummy amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Simiyu
kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 na wadau wengine wameahidi kutoa
shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha wodi ya mama na mtoto.
“Simiyu katika bajeti ya Serikali imetengewa shilingi
bilioni 1.5 lakini tumepata pia shilingi bilioni 1.1 kutoka kwa wafadhili kwa
ajili ya ujenzi waWodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu,
lengo letu ni kukamilisha ujenzi haraka ili tuiwezeshe Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, kuchukua majengo ambayo yanatumika sasa hivi kama Hospitali Teule ya
mkoa” alisema.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema baada ya
kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Serikali ina mpango wa
kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki Mkoani Simiyu, itakayohudumia
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili
kuipunguzia mzigo Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambayo inahudumia mikoa
takribani minane.
Ameongeza kuwa pamoja na kuwa na mpango wa kujenga Hospitali
ya hiyo Rufaa ya Kanda Simiyu, Serikali imekusudia kujenga Hospitali za Kanda
tatu ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambayo imeanza kujengwa
Mtwara, nyingine itajengwa Tabora Kanda ya Magharibi ili wananchi wapate
matibabu ya kibingwa katika maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali
kwa kutoa fedha za kujenga jengo hilo, ambazo zitasaidia kuboresha huduma za
afya katika mkoa wa Simiyu .
Aidha, Mtaka amesema ardhi kwa ajili ya kujenga Hospitali
ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki itatolewa bure na akamhakikishia Waziri
Ummy ushirikiano wa asilimia 100 kila watakapokuwa wakihitajika kwa namna moja
au nyingine ili kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo.
Pamoja na Serikali kuahidi kutoa
shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU, pia Waziri
Ummy amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali
yaWilaya ya Itilima.
MWISHO
Meneja
wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu.Mhandisi.Likimaitare Naunga (wa
pili kulia) akimuonesha Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(katikati) ramani ya
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, mara baada ya Waziri Ummy kutembelea na kuona
maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali hiyo Mjini Bariadi,
Julai12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akimuongoza Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , wakati
alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi
wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,
Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha
wageni wakati alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la
Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Julai
12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea na kuona
maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la
Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,
Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(wa nne kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumaliza ziara
yake ya kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(katikati) akifurahia jambo
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la
Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,
Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na viongozi wa Mkoa wa
Simiyu wakitoka katika Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Simiyu, mara baada Waziri Ummy kutembelea
na kuona maendeleo ya Ujenzi wa jengo hilo Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa
Foundation, Dkt. Hellen Senkoro wakati ziara
ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la
Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi
Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea na kuona
maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akimuongoza Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , wakati
alipotembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi
wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,
Julai 12, 2018.
0 comments:
Post a Comment