Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku
magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance ) kubeba watu au kitu chochote tofauti na
wagonjwa na akawaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini, kusimamia matumizi ya magari hayo na
kuhakikisha yanatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa mujibu wa mwongozo.
Waziri Ummy ametoa
agizo hilo Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la
kuunganisha jamii hasa zile zilizo mbali na vituo vya tiba, ambao umezinduliwa
katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ambao
umelenga kupunguza vifo vya mama na Mtoto mkoani SIMIYU.
“Nimesikitishwa
sana na kitendo cha gari la kubebea wagonjwa la Halmashauri ya Mji wa Tarime
mkoani Mara kubeba dawa za kulevya, ninakemea jambo hili kwa nguvu zangu zote
na ninawataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia matumizi
ya magari ya kubebea wagonjwa “ alisema Waziri Ummy Mwalimu
“
Ni marufuku gari la kubebea wagonjwa kubeba kitu tofauti na mgonjwa, yeyote
ambaye tumemkabidhi gari la kubebea wagonjwa tutamchukulia hatua kali pale
ambapo atakiuka mwongozo wa matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa, nalipongeza
sana jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua na ninamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri
husika kuwasimamisha kazi mara moja dereva na wote waliohusika na gari hilo
kubeba mirungi” alisisitiza.
Akizundua
mradi wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waziri Ummy amewashukuru
wafadhili wa mradi huu Amref Health Africa Tanzania chini ya
Ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Irish aid ambao utatekelezwa kwa kushirikiana na
Benjamin Mkapa Foundation na Halmashauri za Itilima na Misungwi(Mwanza) ukiwa
na lengo la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amezitaka halmashauri zote nchini
kuhakikisha zinaajiri Wahudumu wa Afya
ngazi ya Jamii kutoka katika Halmashauri au wilaya husika na si vinginevyo.
Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga ameomba Zahanati ya Lagangabili
ipandishe hadhi kuwa kituo cha afya kusogeza huduma kwa wananchi, jambo ambalo
limefafanuliwa na Mhe.Waziri kuwa zahanati hiyo haitapandishwa hadhi mpaka
itakapojengewa miundombinu muhimu na akaahidi kutafuta shilingi milioni 400 kwa
kushirikiana na wadau, ili kuwezesha ujenzi wa wodi ya wazazi, mama na mtoto na
jengo la upasuaji.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga amesema viongozi wa Mkoa wa Simiyu wanaunga mkono juhudi za
Serikali na wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya Afya nchini, na
kumhakikishia Waziri Ummy kuwa fedha yoyote itakayotolewa katika Mkoa huo itasimamiwa
ipasavyo na kuleta matokeo chanya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Amref Dkt Aisa Muya amesema mradi huo
utasaidia kuunganisha wananchi walio
mbali na vituo vya tiba kupunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano,
kutoa huduma za awali kwa jamii, kutoa elimu kuhusu njia bora za kuepukana na
magonjwa, kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na kukusanya takwimu
mbalimbali za afya ya jamii vijijini.
Akizungumza kwa niaba ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii Nkwimba Edward
amesema wahudumu hao wako tayari kuhudumia jamii kwa kutoa elimu kuhusu mambo
mbalimbali ya afya na akaomba Serikali na wadau waone namna ya kuwawezesha
kupata usafiri wa kuwafikia wananchi.
Mradi huu utatekelezwa katika
kipindi cha miaka miwili katika Wilaya
mbili ambazo ni Wilaya ya Itilima inayotarajia kuwa na wahudumu wa afya ngazi
ya jamii 102 na Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza itakayokuwa na wahudumu wa afya
ngazi ya jamii 113.
MWISHO
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe
ishara ya uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya , katika Wilaya ya
Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akisalimiana na
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Donatus Weginah mara baada ya
kuwasilis Mjini Bariadi, kwa ajili ya kuzindua mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya,
katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akisaini kitabu
cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mjini
Bariadi, kwa ajili ya kuzindua mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya
Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya
ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw.Donatus Weginah akiwasilisha tarifa ya Mkoa kwa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu mara baada
ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kuzindua mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya
Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Kutoka kulia Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe. Daudi Nyalamu, Mbunge wa Itilima,
mhe.Njalu Silanga na Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Hellen
Senkoro wakiteta jambo wakati wa
uzinduzi wa mradi wa wa TUWATUMIE
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya
Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu na Viongozi
wengine wakiwa katika picha na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanaotarajia
kuhudumia Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa
TUWATUMIE wenye lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa huduma
kwa jamii, uliofanyika katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Kaimu Mkurugenzi wa
AMREF, Dkt. Aisa Muya (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu(kushoto), katika uzinduzi wa
Mradi wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye
lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya (katikati) ni
Mwakilishi Balozi wa Ireland hapa nchini.
Baadhi ya Wananchi wa
Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo pichani) katika uzinduzi wa Mradi wa
TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo
kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya
Mkuu wa Wilaya
Mhe.Benson Kilangi akimuongoza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee
na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu(mwenye skafu) kuelekea eneo la kufanya uzinduzi wa
Mradi wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye
lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu(mwenye skafu) na Mbunge wa
Itilima, mhe.Njalu Silanga wakicheza na kufurahi pamoja na kwaya ya Mabatini
wilayani Itilima, katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo kuwatumia Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya.
Baadhi ya wahudumu wa
Afya ngazi ya Jamii wakiimba shairi mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo pichani) katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo kuwatumia Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akisalimiana na Mwenyekiti
wa UWT Mkoa wa Simiyu, Mhe.Mariam Manyangu, mara baada ya kwasili Mjini
Bariadi, kwa ajili ya uzinduzi wa Mradi
wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo
kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ambao umezinduliwa
wilayani Itilima.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Mkoa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu(kulia) mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi,
kwa ajili ya uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE
Julai 12, 2018 wenye lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya
ambao umezinduliwa wilayani Itilima.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali, mashiriko yasiyo ya kiserikali na watendaji wa Serikali katika ngazi
ya Halmashauri na Mkoa wa Simiyu wakifuatilia taarifa ya Mkoa iliyowasilishwa
na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Donatus Weginah aliyowasilisha kwa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu
alipowasili mjini Bariadi, kwa ajili ya kuzindua mradi wa TUWATUMIE wenye lengo
la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, ambao
umefanyika katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12,2018.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima katika Kijiji cha Lagangabilili
wakati wa uzinduzi wa wa Mradi wa TUWATUMIE
Julai 12, 2018 wenye lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya
ambao umezinduliwa wilayani humo.
Mbunge wa Itilima,
Mhe.Njalu Silanga(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi
wakizungumza na :- Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe.Ummy Mwalimu mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ajili ya kuzindua
mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya
, ambao umezinduliwa Julai 12, 2018 wilayani humo.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa
mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Bariadi mkoani
Simiyu, kwa ajili ya kuzindua mradi wa TUWATUMIE,
wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya,
ambao umezinduliwa Julai 12, 2018 wilayani humo.
Mbunge wa Itilima,
Mhe.Njalu Silanga(kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation
, Dkt. Hellen Senkoro zawadi ya asali katika uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE,
wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya,
ambao umezinduliwa Julai 12, 2018.
Mbunge wa Itilima,
Mhe.Njalu Silanga(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Enock Yakobo zawadi ya asali katika
uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE, wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi
ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya,
ambao umezinduliwa Julai 12, 2018
Mbunge wa Itilima,
Mhe.Njalu Silanga(kushoto) akimkabidhi zawadi ya asali Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mradi
wa TUWATUMIE, wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha
jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya,
ambao umezinduliwa Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu (katikati) na viongozi
wengine wakishuhudia wasanii wa Ngoma yaUtamaduni ya Wagoyangi wanaocheza na
nyoka (hawapo pichani), mara baada ya kuzindua mradi wa TUWATUMIE, wenye lengo
la kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, ambao
umezinduliwa Julai 12, 2018 wilayani Itilima.
Mmoja wa wanautamaduni wa Wagoyangi akionesha umahiri wake wa
kucheza na nyoka, mara baada ya mradi wa TUWATUMIE, wenye lengo la kuwatumia
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya, uliozinduliwa rasmi
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy
Mwalimu Julai 12, 2018 wilayani Itilima.
Mwakilishi wa Balozi wa
Ireland hapa nchini akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa wa Mradi wa
TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo
kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo
magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ambao umezinduliwa
wilayani Itilima.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu na viongozi wakishangilia
mara baada ya mradi wa TUWATUMIE, wenye lengo la kuwatumia Wahudumu wa Afya
Ngazi ya Jamii, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ulozinduliwa rasmi na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu Julai
12, 2018 wilayani Itilima.
Mkuu wa Wilaya Bariadi,
Mhe.Festo Kiswaga akitoa salamu za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka wakati wa uzinduzi wa wa Mradi wa TUWATUMIE Julai 12, 2018 wenye lengo kuwatumia Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu
kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ambao umefanyika
wilayani Itilima.
0 comments:
Post a Comment