Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza
kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyaombukiza katika banda la Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima
Nanenane yatakayofanyika Kitaifa mwaka
2018 mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mhe.
Mtaka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda
la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo Uwanja wa
Nananenane kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Amesema
NHIF itatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi, saratani
ya matiti, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza bure , hivyo hii ni
fursa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa itawapunguzia gharama waitumie vizuri.
Wakati huo
huoMtaka ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja na vikundi vikiwemo vyama vya
ushirika zaidi ya 390 mkoani humo kujiunga nakuwa na kadi za Bima ya Afya, ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma
wakati wowote na kupunguza gharama za matibabu.
“Mini
naamini ugonjwa hauna hodi hivyo nitoe wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa
bima ya afya na sisi kwetu bima ya afya ni kipaumbele kwa kuwa tunahitaji
mapinduzi ya kuchumi na kielimu tunayofanya ndani ya mkoa yaende sambamba na
watu kupata kadi za bima ya afya, ili waone thamani ya Serikali kuwekeza katika
sekta ya Afya” alisema.
“Katika
sherehe za nanenane za mwaka 2018 niwaombe wananchi popote walipo watumie fursa
hii ya kufikiwa na wenzetu wa Bima ya Afya,ili wawezeka kupata huduma za upimaji
magonjwa yasiyoambukiza bure na kujiunga na bima ya afya “ alisisitiza.
Naye Meneja
Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Hilipoti Lello amesema pamoja na kutoa
huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure, huduma za usajili kwa ajili
ya kupata kadi za bima ya afya ya mtu
mmoja , familia na vikundi zitatolewa ambazo zitalipiwa kulingana na aina ya
kadi itakayotolewa .
“Tutatoa
huduma za usajili na kutoa kadi za bima ya afya katika banda hili na mtu
akishasajiliwa hapa kadi zitatolewa hapa hapa, tutakuwa na kadi za watoto toto
afya kadi, tutakuwa na huduma za ktoa kadi kwa vikundi na kwa wakulima ni kwa
wale walio kwenye vyama vya ushirika(AMCOS); mtu yeyote atakayepata kadi hii
atapata matibabu Tanzania nzima kuanzia Zahanati hadi hospitali ya Rufaa”
alifafanua.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, Bw. Shabani Kiduta ametoa wito
kwa Wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya upimaji wa
magonjwa yasiyoambukiza kujua afya zao na kupata tiba, ili Mapinduzi makubwa ya
kiuchumi yanayofanywa mkoani humo yaweze kuwafikiwa wakiwa na afya njema.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Meneja
Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hilipoti
Lello akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko huo, lililopo Uwanja wa
Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari
jengo la maonesho la mkoa huo, lililojenhgwa katika Uwanja wa Nanenane Halmashauri
ya Mji wa Bariadi leo, ambalo lipo katika hatua za ukamilishaji.
0 comments:
Post a Comment