Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt.Mary Mwanjelwa ametoa wito kwa wakulima kote nchini kulima kilimo chenye tija kwa
kutumia zana bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kupata mavuno mengi na bora.
Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo Agosti
Mosi, mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya Kilimo katika Uwanja wa
Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Bariadi, katika Maonesho
ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.
Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali kupitia Mfuko
wa pembejeo unatoa mkopo wa pembejeo kwa riba ndogo sana, hivyo akatoa wito kwa
wakulima wote nchini kwenda katika Halmashuri zao na kupata utaratibu wa kuomba
mikopo hiyo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kununua zana bora za
kilimo.
“ Nitoe wito kwa wakulima wote nchini wajitahidi
sana kwenda kwenye kulima kilimo cha
kisasa kilimo chenye tija, sisi kama Serikali tuna mfuko wetu wa pembejeo
unaotoa mikopo kwa riba ndogo sana, hivyo wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo
na kwenda kununua pembejeo bora za Kilimo” alisema Dkt. Mwanjelwa.
Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewataka
maafisa ugani kuwafuata wakulima shambani badala ya kukaa ofisini, ili kuwapa
elimu ya kilimo bora na kuwawezesha wakulima kufikia lengo la kulima kilimo chenye tija.
Naye Baraka Itemu mkulima wa Mpunga kutoka
Geita ametoa wito kwa wakulima wenzake
kote nchini kuachana na matumizi ya jembe la mkono na jembe la kukokotwa na ng’ombe
kwa kuwa ni teknolojia iliyopitwa na wakati na haina tija katika uzalishaji.
“ Mimi ni mkulima wa mpunga binafsi
matrekta yamenisaidia sana maana naweza
kulima eneo kubwa kwa muda mfupi na nikapata mazao mengi, natoa wito kwa
wenzangu wanaotumia majembe ya mkono na ya kukokotwa na ng’ombe waache waende
kwenye makampuni ya matrekta wakakope, ili
waweze kuzalisha mazao kwa wingi” alisema Baraka.
Nao wauzaji wa zana bora za kilimo
waliofika katika maonesho ya Nanenane Bariadi mkoani Simiyu wamesema wako
tayari kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha wanapata zana hizo, huku
wakibainisha kuwa wakulima wasiokuwa na uwezo wa kununua zana hizo kwa fedha
taslimu wako tayari kuwakopesha.
Maonesho ya Nananane mwaka 2018
yanafanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ambapo yameanza leo na yatahitimishwa Agosti
08, 2018.
MWISHO
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Mary
Mwanjelwa akikagua mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane
Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi
leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani
Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt. Mary
Mwanjelwa akisalimiana na Katibu Tawala
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada kuwasili katika Uwanja wa
Nanenane wa Nyakabindi Bariadi, kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za
maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu.
Bw. Baraka Itemu mkulima wa Mpunga
kutoka Geita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha pichani) katika Uwanja wa
nanenane Nyakabindi Bariadi, yanayofanyika kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu.
Mtaalam wa kutoka Jeshi la Magereza
akitoa maelezo kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa wakati
walipotembelea mabanda ya maonesho ya mifugo ya Jeshi hilo katika Uwanja wa
Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi, katika maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa Ufugaji wa Samaki kutoka JKT,
Luteni Joseph Lyakurwa(kulia) akitoa
maelezo kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu
kushoto) na Mhe. Omary Mgumba (kushoto) wakati
walipotembelea mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji Bariadi, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa Jeshi la Magereza akitoa
maelezo ya namna ya kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mimea kwa
Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kulia) na Mhe. Omary Mgumba (wa pili kulia) wakati
walipotembelea mabanda ya maonesho ya Jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya
Mji Bariadi, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani
Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Mary
Mwanjelwa akipewa maelezo kuhusu zana na mashine za kisasa na wataalam wa JKT katika Uwanja wa Nanenane
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu kwa
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa mara baada kuwasili katika
Uwanja wa Nanenane wa Nyakabindi Bariadi, kwa ajili ya kujionea shughuli
mbalimbali za maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani
Simiyu.
0 comments:
Post a Comment