Waziri wa Kilimo,
Dkt. Charles Tizeba amewataka Waandaaji wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za
Wakulima Nanenane hapa nchini kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka 2019 wanaandaa
maonesho hayo katika sura mpya itakayoleta mabadiliko chanya kwa wakulima,
wafugaji na wavuvi ili waweze kuzalisha kwa tija.
.
Waziri Tizeba
ameyasema hayo Agosti 03, 2018 katika Uwanja wa Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki, uliopo Nyakabindi Bariadi, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 yanayofanyika Mkoani Simiyu.
Amesema ni vema
waandaaji hao wakatoka katika maonesho ya mazoea ya kuwaonesha wakulima na
wadau vipando mbalimbali pasipo kuwapa
elimu ya namna yakufikia uzalishaji wanaouona katika maonesho, badala yake
maonesho hayo yatumike kuwafundisha wananchi na kubadilishana uzoefu.
“Kuanzia nanenane
ya mwaka huu na zinazofuata, wandaaji wazipe sura mpya hata tunapowaomba wadau
mbalimbali kuchangia maandalizi wawe wananamini kuwa tutakachokifanya kitaleta mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na
wavuvi wa nchi hii”alisema Tizaba.
Aidha, Dkt. Tizeba
amekubaliana na mpango wa viongozi wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga
kufanya maonesho kila baada ya miezi mitatu katika Uwanja wa Nyakabindi ili
kuwapa fursa wananchi ya kuendelea kujifunza badala ya kusubiri kila wiki ya
nanenane kila mwaka.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya Mkoa huo na kanda ya Ziwa ya
Mashariki ni kuendelea kufanya maonesho Teknojia za Kilimo Biashara katika Uwanja wa Nyakabindi jambo
ambalo litawapunguzia Watanzania kwenda nje ya nchi kujifunza teknolojia hizo.
“Tutafanya maonesho
hapa kila baada ya miezi mitatu, kupitia maonesho yatakayofanyika eneo hili, tutawapunguzia
wananchi safari za kwenda nje ya nchi kufuata teknolojia za kilimo Biashara” alisema
Mtaka.
Katika hatua
nyingine Mtaka amesema Waoneshaji waliopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi wameomba
kuongezewa siku mpaka kufikia Agosti 11 badala ya Agosti 08 kama ilivyo
kawaida, jambo ambalo lilikubaliwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles
Tizeba.
Naye Mkuu wa Mkoa
wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya viongozi wa Kanda ya Ziwa
Mashariki ni kuyafanya maonesho ya nanenane kanda hiyo kuwa mnara wa mafanikio
katika sayansi na teknolojia na namna ambavyo kilimo kinachozingatia kanuni bora
kinavyochangia mabadiliko chanya ya mfumo wa Watanzania waanotegemea kilimo.
Naibu Waziri wa
Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wananchi kufika Uwanja wa Maonesho ya
Nanenane Nyakabindi ili kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kwa kuwa kwa
sasa waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wapo uwanjani hapo.
Maadhimisho ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za
Wakulima Nanenane mwaka 2018 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu ni ya 25
kufanyika hapa nchini na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amesema maonesho
hayo yatafanyika miaka mitatu mfululizo, mwaka 2018, mwaka 2019 na mwaka 2020.
MWISHO
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akipewa maelezo kuhusu teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba alipotembelea mabanda ya Wizara ya
Mifugo na Uvuvi kwenye ufunguzi wa maonesho
ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya
Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wataalam wa Kilimo wa JKT alipotembelea mabanda ya JKT ya maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akizungumza na
wananchi wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe
za Nanenane Kitaifa mwaka 2018, katika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa wakati wa ufunguzi wa maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa
Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akiangalia namna
mashine hiyo pichani inavyochuja mafuta, mara baada ya kutembelea mabanda ya
maonesho ya Mkoa wa Mara, wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa
mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Malima akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa
Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akipokea maelezo
kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani
Mara, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani
Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia ) na viongzo wengine wakishangilia
jambo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani
Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba(wa pili kulia)
akipewa maelezo juu ya samani iliyotengenezwa na VETA, baada ya kutembelea
banda la Maonesho la VETA, wakati wa
ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika
Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba(mwenye skafu) na
viongozi wengine wakielekea kwenye mabanda
ya maonesho wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa
Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akipokea maelezo
mara baada ya kutembelea banda la Maonesho la NBC , wakati wa ufunguzi wa
maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adamu Malima (aliyenyosha mkono
kuelkea mazao) akizungumza jambo wakati walipotembelea Kitalu cha Kilimo cha
Wizara ya Kilimo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018
Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba (katikati )
akizungumza na Wataaamu wa MWIBA HOLDINGS LTD , wakati alipotembea banda
la Mwekezaji huyo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akiangalia teknoljia
ya ufugaji wa samaki alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi , kwenye ufunguzi wa maonesho ya NaneNane
Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Dkt.
Charles Tizeba (katikati) akiwa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa
Mashariki kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018
Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akipokea maelezo mara
baada ya kutembelea banda la Maonesho la NMB, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa
Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akinywa maziwa ya
Meatu, mara baada ya kutembelea Jengo
la Maonesho la Mkoa wa Simiyu,
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Kwaya
ya AICT Bariadi ikiimba wimbo maalum kwa ajili ya Nanenane, wakati wa ufunguzi
wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Baadhi ya
Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakitunza Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na kumpongeza kwa utendaji wake,
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Kikundi cha Ngoma za
Asili cha BASEKI kikitoa burudani , wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa
Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
:-Mbunge wa Jimbo la
Maswa Magharibi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi
wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mbunge wa Jimbo la
Itilima, Mhe. Njalu Silanga akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa
maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) akicheza pamoja na wasanii wa Eliza Band, wakati wa
ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika
Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akifuatilia jambo, wakati wa ufunguzi wa maoneshoya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa
Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi Mhe. Andrew Chenge akizungumza
na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani
Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, mhe. Enock Yakobo, akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa
maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa
maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa
maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe
akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka
2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki
uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Agosti 03, 2018.
Baadhi ya wananchi na
madiwani wakisikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, wakati wa
ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika
Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Baadhi ya
Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakitunza Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na kumpongeza kwa utendaji wake,
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya
Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa
Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa
maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa
Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba(wa sita kulia mbele)
katika piccah ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali baada ya
kufungua Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 yanayofanyika mkoani
Simiyu.
0 comments:
Post a Comment