Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wametakiwa
kuwakumbusha wazazi na walezi kuwanunulia watoto wao sare za shule na kuchangia
chakula mashuleni ili watoto wao waweze kusoma kwa utuivu na umakini wanapokuwa shuleni
na kuzuia utoro .
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles
Kabeho wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera yaliyofanyika
katika Kijiji cha Mkula wilayani humo.
Kabeho amesema Serikali ya awamu ya tano imefuta ada
na michango mbalimbali iliyokuwa kero kwa wananchi ili kila mtoto wa Kitanzania
apate haki ya Elimu kuanzia darasa la awali mpaka Kidato cha nne bila malipo ,
hivyo wazazi na
walezi wanapaswa kuwanunulia watoto wao sare za shule pamoja na mahitaji yao mengine
ya shule ikiwa ni pamoja na daftari na kalamu.
“ Kwa sasa wazazi hamlipi tena ada wala michango wajibu wenu ni kununua sare za shule na kununua
mahitaji mengine kama kalamu, daftari na mabegi ,Serikali inaendelea
kuhamasisha mtimize wajibu wenu, lakini pia namuomba Mkurugenzi awaeleze Walimu
wakuu sare za Halmashauri yake ni zipi ili nao wawakumbushe wazazi kwanunulia
watoto wao sare hizo” alisema.
Aidha, Kabeho amesema ni vema wazazi
na walezi wakachangia chakula shuleni ili kuwafanya wanafunzi waweze kusoma
kwa utuivu na umakini wanapokuwa shuleni na kuzuia utoro .
“Tunaomba pia mtimize wajibu wenu kuchangia chakula
shuleni kwa sababu unapotoa chakula shuleni tunapunguza utoro , tunaongeza
umakini na ufuatiliaji kwa wanafunzi pale wanapofundishwa, wanafunzi wengi wao
wanatoroka pale wanapohisi njaa na wakiondoka baadhi yao hawarudi” alisema
Kabeho.
Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Busega na kupitia
miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 900 katika sekta mbalimbali
ikiwemo Afya, Elimu na Viwanda.
Akizungumza mara baada ya kufungua vyumba vitatu vya madarasa na matundu matano
ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nasa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2018, Ndg. Charles Kabeho ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya
ujenzi wa miundombinu ya elimu ambayo itasaidia kuboresha mazingira ya
kufundishia na kujifunzia.
Akizungumza na Wananchi baada ya kufungua Wodi ya wazazi katika Kituo cha
Afya cha Nasa Kabeho amewashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea nguvu kazi
katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika Kituo hicho cha
Afya cha Nasa.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Wodi hiyo ya wazazi, Katibu wa Afya
Wilaya wa Wilaya ya Busega Huruma Temu amesema kuwa wodi hiyo katika kituo cha
Afya Nassa hadi kukamilika kwake imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 109
ikiwa ni fedha za wafadhili kutoka UNFPA.
Haruna alibainisha kuwa lengo kuu la kujenga wodi hiyo ya wazazi ni
kuboresha afya ya uzazi na kupunguza idadi ya vifo vya akinamama na watoto
Wilayani Busega.
MWISHO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akitoa Ujumbe wa Mwenge wa
Uhuru mwaka 2018 katika Kijiji cha Mkula
wilayani Busega, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 18, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikagua Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya
Sekondari Nasa wilayani Busega kabla ya
kuvifungua, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 18, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(kulia) na
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakikabidhiana Mwengewa Uhuru
tayari kwa ajili kuanza mbio zake wilayani Busega Agosti, 2018.
Mkurugenzi wa Nassa Alovera Proccesors , Bw. Venance
Mdunga (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho(wa
pili kulia), wakati alipofika kukagua shamba lake ambalo linatoa malighafi ya
kutengeneza bidhaa zitokanazo na Alovera.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(kushoto)
akisalimiana na Kiongozi wa Mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, mara baada ya Mwenge
wa Uhuru, kufika wilayani Busega, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda
cha Kukoboa Mpunga na kupanga madaraja kilichopo Lamadi Bariadi, Agosti 17, 2018.
Askari wa FFU na Mkimbiza
Mwenge wa Uhuru Kitaifa Riziki Hassan Ali wakiondoka na Mwenge wa Uhuru katika Viwanja vya Shule
Sekondari Nassa wilayani Busega, wakati ukiwa
katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018
Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Kwa Mkimbiza
Mwenge Kitaifa Riziki Hassan Ali kutoka
Mkoa wa Kusini Unguja, kwa ajili ya kuanza ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani
humo, Agosti 18, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikagua Wodi ya Mama na Mtoto iliyopo katika Kituo cha
Afya cha Nasa wilayani Busega, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,
Agosti 18, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeyo(katikati) akiteta jambo na
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson
Njiginya, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 18, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akisalimiana na Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Mickness Mahela, wakati wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 18, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akisalimiana
na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya wakati
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 18, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akipewa maelezo na Mfanyakazi
wa Kiwanda cha Nassa Alovera Proccesors juu ya namna
wanavyotengeneza bidhaa mbalimbali na dawa zinazozalishwa zinazozalishwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiangalia mchele ulikobolewa
ukiwa katika hatua za mwisho kupangwa na kuwekwa wenye madaraja, kabla ya kukiwekea kiwanda
hicho jiwe la msingi, wakati Mwenge ukiwa katika Mbizo zake wilayani humo Agosti
17, 2018. .
0 comments:
Post a Comment