Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa
zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la
mazao ya wakulima hapa nchini.
Mhe. Mkapa amesema hayo katika
Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi
akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli.
“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa
Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la
mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa
kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.
Aidha, amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote
kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia
usalama wa chakula katika kaya zao.
Mkapa pia amesema Serikali ina mkakati
wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi
kufikia tani milioni moja mwaka 2020.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa
Maonesho ya Nane nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika
kanda mpya Kanda ya Ziwa Mashariki katika
Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike
Kimataifa kwa kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu utaendelea kulipa kiupaumbele zao la Pamba na mwaka ujao
uzalishaji utaongezeka kutoka kilo milioni 70 hadi kufikia kilo 150.
“Simiyu
tunajivunia wananchi wachapa kazi wenye uthubutu na Simiyu inajengwa na
Wanasimiyu, mwaka jana tumezalisha kilo milioni 70 za pamba, kwa mwaka huu sasa
hivi msimu ukiwa umefikia katikati tuna kilo milioni 85, mwakani tunatarajia
kuzalisha kilo zaidi ya 150” alisema
Ameongeza
kuwa wananchi wamelima chakula cha kuwatosheleza si watu wa kuomba chakula cha msaada
huku akiupambanua Mkoa wa Simiyu kuwa ni mkoa pekee ambao watu wake wanafanya
biashara saa 24.
Maonesho
ya Nanenane Mwaka 2018 yaliwashindanisha wakulima na wafugaji mmoja mmoja,
Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma na Binafsi, Wizara pamoja na Halmashauri 21
za Mikoa ya Simiyu Mara na Shinyanga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
imekuwa ya tatu kati ya hizo 21.
Kauli
mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 “ WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
KWA MAENDELEO YA VIWANDA”
MWISHO
Rais Mstaafu
wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa
akizungumza na wananchi katika Kilele
cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa Simiyu ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji
wa Bariadi.
Meneja wa
TANESCO Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Rehema
Mashinji akipokea cheti ikiwa ni miongozi mwa mashirika yaliyofanya vizuri
katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa
Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Rais Mstaafu
wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa
akisalimiana na Mbunge wa Bariadi, Mhe Andrew Chenge baada ya kuwasili Bariadi
katika Uwanja wa Nyakabindi kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018.
Kutoka
kushoto, Waziri wa Kilimo,Mhe.Dkt. Tizeba, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiungan na viongozi na wananchi kuimba wimbo wa
TAIFA, katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa
Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Mtaalam
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Kilimo akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa kuhusu Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki
kupitia Vizimba, katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika
uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Kanali Hassan
Mabena(kushoto) akipokea kikombe cha JKT kuwa mshindi wa jumla kutoka kwa Rais
Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin
William Mkapa, kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Martin Busungu, katika Kilele
cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji
wa Bariadi.
Vijana wa
JKT Lwamkoma mkoani Mara wakifurahi Ushindi wa Jeshi hilo kupata kombe la mshindi
wa kwanza wa jumla, katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika
uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Rais Mstaafu
wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa
akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Serikali ya Msumbiji, mara baada ya
kuhitimisha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa
Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa
Bariadi.
Waziri wa
kilimo, Mhe.Dkt. Charles Tizeba akitoa maelezo juu ya masuala ya ufugaji wa ng’ombe kisasa kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Benjamin William Mkapa(wa pili kushoto) katika Kilele cha Nanenane
Kutoka
kushoto, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally., Waziri wa Kilimo,Mhe.Dkt.
Tizeba, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Benjamin William Mkapa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakiungana na viongozi na wananchi kuimba
wimbo wa TAIFA, katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika
uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
0 comments:
Post a Comment