Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya
ya Busega na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu zinawakaribisha
wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza kwenye jumla ya viwanja 3758
vilivyopimwa na vinavyotarajiwa kupimwa kwa nyakati tofauti.
Hayo yamebainishwa na Viongozi wa Halmashauri hizo
katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane
yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi,watumishi na wadau mbalimbali waliofanikisha, kilichofanyika Agosti
20, Mjini Bariadi.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo amesema Halmashauri yake
inatarajia kupima viwanja 758 katika eneo la Maperani, huku Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akibainisha kuwa
Halmashauri hiyo kuanzia Septemba Mosi, 2018 itaanza kupima viwanja 1000 katika
eneo la Malampaka.
Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko
amesema Halmashauri hiyo imeanza kupima viwanja 2000 Agosti 20, 2018 katika eneo ambalo liko umbali wa chini ya kilomita
moja kutoka Ziwa Victoria, pia imetenga ekari zaidi ya 2000 kwa ajili ya uwekezaji
na akasisitiza kuwa ardhi itatolewa bure kwa wawekezaji watakaotaka kujenga
viwanda.
Viongozi hao wametoa wito kwa wafanyabiashara,
wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa wa Simiyu,Taasisi, mashirika, makampuni na
wananchi kujitokeza kununua viwanja hivyo kwa ajili ya kuviendeleza kwa
uwekezaji na kubainisha kuwa maeneo yote yanayotarajiwa kupimwa Bariadi, Maswa
na Busega ni ya kimkakati katika uwekezaji.
"Kuanzia tarehe 01 Septemba, tutaanza kupima
viwanja 1000 katika eneo la Malampaka Maswa, ni eneo la kimkakati katika
uwekezaji kwa sababu patapitiwa na Standard Gauge(Reli ya Kisasa) na patajengwa
dry port (bandari kavu), nitoe wito kwa wafanyabiashara kuja kununua viwanja
Malampaka kwa ajili ya kufanya uwekezaji mbalimbali; kwa wale wawekezaji watakaotaka
kujenga viwanda sisi Maswa tutatoa ardhi bure" alisema Dkt. Sagamiko.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito
kwa Wafanyabiashara wa Mkoa huo kuwekeza katika Ujenzi wa Hoteli, Nyumba za
kulala wageni na kumbi za mikutano hususani katika Eneo la Uwanja wa Nanenane
Nyabindi na maeneo mengine, ili kukabiliana na changamoto ya malazi kwa kuwa
Simiyu imepewa heshima ya kuwa Mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane kwa miaka
mitatu mfululizo.
Amesema pamoja na kuwa mwenyeji wa Maonesho Nanenane
Kitaifa yapo matukio mengine yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ikiwa ni
pamoja na Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 2018, Maadhimisho ya Kimataifa
ya siku ya watu wenye Ulemavu Desemba 2018, Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa
Mikoa na Wilaya hapa nchini mwaka 2019 na mengine mengi yatafuata baada ya hapo
hivyo maandalizi ni muhimu..
Amesema Serikali mkoani humo kupitia Halmashauri
zake imedhamiria kuwekeza katika ujenzi wa sehemu za malazi lakini
inaendelea kuweka msukumo kwa wafanyabishara kuwekeza si tu katika ujenzi wa nyumba
za kulala wageni na hoteli, bali katika ujenzi wa vituo vya mafuta, maeneo ya
utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za chakula na huduma za kibenki.
Mmoja wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu Bw. Malongo
Midimu amesema wako tayari kuwekeza mkoani hapa na akaomba Serikali
pamoja Taasisi za Kifedha zikiwemo Benki kuondoa vikwazo na urasimu pale
wanapohitaji masuala hayo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo
ametoa wito kwa Wafanyabiashara kujipanga katika uwekezaji kwa kuwa Simiyu
inabadilika na inaendelea kufunguka ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa
Ujenzi wa miundombinu kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Igegu wilaya ya
Bariadi, barabara ya Maswa-Bariadi kutachangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa.
Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za
Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018, Uwanja wa Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kiliwahusisha Viongozi na Watendaji wa Chama na
Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Watumishi na Wadau mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara
wa Mkoa wa Simiyu kikiwa na lengo la kushukuru na kutambua mchango wa wadau
wote muhimu waliofanikisha maonesho hayo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko
akizungumza katika Kikao cha Tathmini
Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na
kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali,
wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali,
Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika
Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara na
Mjumbe wa NEC Taifa kupitia Mkoa wa
Simiyu Bw. Gungu Silanga akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara wa Mjini
Bariadi, Bw. Clement Mlanda akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima Mhe. Benson Kilangi akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu wa Umoja wa
Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya akizungumza katika
kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali,
Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi
Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa
mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru
Viongozi na watendaji wa Chama na
Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi..
0 comments:
Post a Comment